- Corinthia_Hotel_London_exterior
- Corinthia_Hotel_London_lobby
- corinthia-hotel-london
- Rihanna
Kikosi cha zima moto jijini London, Uingereza, kimesema mwanadada
Rihanna ni miongoni mwa watu 300 waliotolewa kwenye moto ulioubuka
mapema asubuhi jana kwenye lift ya hoteli hiyo.
Mwanamuziki huyo mwenye miaka 24, alitweet habari hiyo kwa wafuasi wake
milioni 21 kwa kuweka picha ya gari la zimamoto na maneno yasemayo:
“Roamin da streets since 6am! Fyah in da telly.”
Kikosi hicho kilisema king’ora cha hatari kililia saa 6:22 a.m. na
askari kumi wa zimamoto walifanya kazi ya kuuzima moto huo uliozuka
kwenye ghorofa ya saba ya hoteli ya kifahari ya Corinthia. Hakuna ripoti
za majeruhi kutokana na moto huo.
Rihanna yupo nchini Uingereza kwa zaidi ya wiki moja sasa ambako amekuwa
akifanya show mbalimbali ikiwa pamoja na kuwapa support Jay-Z na Kanye
West ambao wapo ziarani barani Ulaya iitwayo ‘Watch the Throne Tour’.
Rihanna, Jay-Z, David Guetta na Elton John watakuwa miongoni mwa
watumbuizaji kwenye sherehe ndefu za “London 2012 Festival’, ambazo
zimeandaliwa kote nchini Uingereza kwendana na michezo ya kiangazi ya
olimpiki mwaka huu mjini London.
Sherehe hizo ambazo zimeanza, zitaendelea hadi Sept. 9, na kujumuisha matukio na performance 12,000.
Kutakuwepo na matukio mbalimbali katika masuala ya filamu, muziki, mitindo, sanaa za majukwaa, dance na sanaa za mikono.
Website ya mtandao huo imesema hizo ni sherehe kubwa kuwahi kufanyika
nchini Uingereza zikiwa na bajeti ya takriban dola milioni 86.
SOURCE BONGO 5