Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, July 10, 2013

WATU 11 WALIJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI AINA YA TAQWA HUKO MBARALI


Juu na chini ni  Muonekano wa Basi la Kampuni ya   Taqwa baada ya kupata ajali na Watu  11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi  hilo walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.



Hapo ni abiria wa Basi hilo la Taqwa wakisubiria Masaada  ili waendelee na safari yao.


  Muonekano wa Basi la Kampuni ya   Taqwa baada ya kupata ajali na Watu  11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi  hilo walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.

Juu na chini ni  Muonekano wa Basi la Kampuni ya   Taqwa baada ya kupata ajali na


Watu  11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi  hilo walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.
Watu  11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Taqwa walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.

Ajali hiyo mbaya ilitokea juzi majira ya saa 2:00 usiku katika mtelemko wa mlima Mambi katika barabara Kuu ya Mbeya –Iringa wilayani Mbarali ikihusisha basi la Kampni ya Taqwa lenye namba za usajili T 396 AXZ na lori aina ya Center lenye namba za usajili T 175 BRA.


Baadhi ya watu walikuwa ndani ya basi hilo walisema kuwa wakati basi hilo likiwa kwenye mwendo mkali katika mteremko huo, lori aina ya Center ambalo lilikuwa likipandisha lilijaribu kupita gari lingine lilikuwa limesimama kando ya barabara, ndipo magari hayo yalipogongana uso kwa uso na kusababisha basi hilo kupoteza mwelekeo na kupinduka mtaroni.


Getruda Kambale ambaye ni raia wa Congo, ni miongoni mwa abiria walionusurika kwenye ajali hiyo ambaye alisema kuwa licha ya basi lao kubondeka vibaya, hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya abiria wameumia vibaya.


“Tunashukuru Mungu hakuna mtu amekufa hapa, lakini dereva wetu ameumia vibaya wamemchukua na kumkimbiza Hospitali,” alisema Kambale.


Alisema wakati yeye akiwa amewa amechoka baada ya kusafiri kwa siku mbili akitokea Nairobi, alishtikia basi likiyumba kasha akasikia kishindo kikubwa na ndipo alijikuta akitolewa kwenye gari hilo kupitia dirishani.


Daktari Msaidizi wa Hospitali ya Misheni Chimala, Peter Seif Kigombola alisema kuwa hospitali hiyo imepokea majeruhi 11, kati yao 10 walikuwa ji abiria wa basi la Taqwa na mmoja alikuwa ni dereva wa lori aina ya Center.


Alisema abiria hao tisa hali zao zinaendelea vizuri, lakini wawili ambao ni dereva wa basin a kondakta wake hali zao ni mbaya na kuwa wamepewa rufaa ya kwenda katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.


Alisema kuwa dereva na kondakta wake walivunjika viungo mbalimbali vya miili yao kama vile mikono na miguu na kupata majeraha mengine kichwani, hali ambayo imesababisha hali zao kuwa mbaya.


Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo pamoja na  kukusanya taarifa za majeruhi na kuwa atatoa taarifa ya ajali hiyo baadaye.

Sema Sina Pesa SIO HAtuna Pesa::Milionea akodi ‘private jet’ kwa shilingi milioni 162 kumsafirisha paka wake kutoka Urusi hadi Marekani

Paka mwenye jina Marsik wa Urusi amesafirishwa na ndege binafsi ya Paramount Business Jets (PBJ), kutoka Urusi hadi Marekani kwa gharama ya dola laki moja ambazo ni sawa na shilingi milioni 162 za Tanzania.
Akisafiri kutoka Urusi hadi Marekani, Marsik anadaiwa kupata huduma ya nguvu kabla hajapanda na ndani ya ndege hiyo.
Vyeti vyake vya afya vinavyoonesha chanjo alizopata alivipata saa 24 kabla ya safari kuanza.
Tajiri huyo anadai kutumia kiasi chote hicho ili kuhakikisha kuwa paka wake anafika Marekani salama na kuepuka kunyanyasika ama kifo kwakuwa baadhi ya wanyama wanaosafiri kwa ndege za kawaida huwekwa kwenye sehemu ya mizigo hupoteza maisha.
Source: prweb.com

BABA YAKE JOYCE KIRIA AMEFARIKI DUNIA, MUNGU AMPUMZISHE MAHALI PEMA PEPONI


 
BABA MZAZI WA JOYCE KIRIA .. Michael Francis Iwambo Kiria wa kibosho dakau nganyeni amefariki huko mkoani Tanga ambako alikuwa akiishi. Kesho ni safari ya kuelekea moshi kwa ajili ya taratibu za mazishi.

NYOTA WA ZAMANI WA MACHESTER UNITED FORTUNE AITEMBELEA AZAM FC TAZAMA PICHA.

Quinton Fortune (kulia) akiongea na Kocha Mkuu wa Azam FCStewart Hall.
...Akionyeshwa swimming pool.
Fortune akihojiwa na mwanahabari kutoka EATV.
Quinton Fortune (mwenye tisheti nyeusi na kaptura) akiongea na Sterwart Hall wakati akionyeshwa mandhari ya Chamazi Complex.
..Akiwa katika gym ya Azam FC.
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Atletico Madrid, Bolton Wanderers na nyinginezo, Quinton Fortune, ambaye kwa sasa anasomea fani ya ualimu wa soka kwenye Klabu ya Manchester United, leo alitembelea Azam FC Chamazi kwa mwaliko wa DHL.
Fortune alishangazwa na ubora wa Center ya Azam FC na kusema hajawahi kuona kitu kama hiki kinachomilikiwa na klabu hata kwenye nchi yake ya Afrika ya Kusini.
(Picha na Azam FC)

MHANDISI WA MAJI LUDEWA KORTINI KWA UBADHILIFU WA SHILINGI MILIONI 4.2

dsc07978
Na Bazil Makungu Ludewa
TAASISI ya kuzuia na kupambana rushwa wilayani Ludewa (Takukuru) imempandisha kizimbani mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Atanasio Munge kwa makosa ya ubadhilifu wa jumla ya shilingi 4.2 milioni mali ya halmashauri ya wilaya hiyo.
Mbele ya hakimu mkazi mheshimiwa JUMA HASSANI katika mahakama ya mkoa Iringa mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Imani Mitume akaiambia mahakama kuwa mshtakiwa anakabililiwa na makosa manne ikiwemo matumizi ya nyaraka kosa linaloangukia kwenye kifungu namba 22 ya sheria ya kuzuiaz na kupambana na rushwa namba 11/2007.
Makosa mengine ni ufujaji na ubadhirifu wa fedha za umma chini ya namba 28(2) sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na 11 ya mwaka 2007, kosa lingine ni kuibabishia hasara serikali shilingi milioni 4 makosa chini ya kifungu namba 10(1) jedwari la 57(1) na jedwari la 60(2).
Pamoja na mhandisi Atanasio Munge mshtakiwa wa pili ni mfanyabiashara wa mgahawa Videa Kayombo maarufu kama (mama hadija) ambaye jina,saini na mgahawa wake vilitumika kutoa stakadhi zinazoonesha kuwa alitoa huduma hewa ya chakula chenye thamani ya shilingi m.4.2 kwa wananchi wa vijijini katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji wilayani Ludewa inayofadhiriwa na Benki ya dunia.
Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Imani Mitume alisema watuhumiwa wote wawili walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2010 na 2012 na kwamba Vedea Kayombo alitoa risiti za uongo huku akijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Kufuatia tukio hilo Kamanda wa TAKUKURU wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Edings Mwakambonja ametoa rai kwa wananchi wilayani humo kutoa ushirikiano na ofisi yake kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa lakini pia akawahimiza kusimamia miradi inayopelekwa na serikali katika maeneo yao.
Mwakambonja pia amewataka watumishi wa umma kuwa waadlilifu katika kazi zao ili kuiepushia serikali hasara na kusababisha kuzorota kwa huduma bora za kijamii jambo linalosababishwa na watumishi wasio na uzalendo na nchi yao.

UGANDA CRANES KUTUA DAR KESHO KUIKABILI STARS JUMAMOSI.

uganda-cranes-versus-zambiaTimu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Julai 11 mwaka huu) tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

The Cranes itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda ambapo itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo.

Waamuzi wa mechi hiyo ambao wanatoka Burundi nao watawasili kesho saa 9.35 kwa ndege ya Kenya Airways. Naye Kamishna wa mechi hiyo Tesfaye Gebreyesus kutoka Eritrea atatua nchini keshokutwa alfajiri kwa ndege ya EgyptAir.

Maofisa wote hao wa mechi hiyo watafikia hoteli ya New Africa. Mkutano wa maandalizi ya mechi utafanyika Ijumaa saa 10 jioni Uwanja wa Taifa, na utakuwa chini ya Gebreyesus.

KAULI YA JESHI LA POLISI KUHUSU CHADEMA KUANZISHA KIKUNDI CHA KUJIHAMI



Mnamo tarehe 09/07/2013, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Freeman Mbowe alitoa kauli kwamba wanaunda kikundi chao cha kuwalinda ambacho watakipatia mafunzo ya ukakamavu.
Kitendo cha chama chochote cha siasa ikiwemo CHADEMA kuanzisha kikundi cha kujihami ni kinyume cha sheria za nchi na endapo watafanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kufuatia kauli hiyo, Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi na litachukua hatua kulingana na ushahidi utakaopatikana. Aidha, Jeshi la Polisi litamshughulikia mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria bila kujali wadhifa wake.

Imetolewa na:-

Advera Senso-SSP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.

JK AHUTUBIA MIAKA 50 YA JKT ASEMA CHANGAMOTO BADO ZIPO NYINGI



Mheshimi wa Shamsi Vuai Nahodha (Mb), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa;
Mheshimiwa Gril Haskel, Balozi wa Israel;
Meja Jenerali Raphael Muhuga,Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa,
Makamanda, Wapiganaji na Vijana;
Wageni Waalikwa;
Ndugu Wananchi;
Mabibi na Mabwana;
Pongezi
Nakushukuru sana Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga kwa kunishirikisha kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhai wa Jeshi la Kujenga Taifa. Nawapongeza sana kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizi ambazo hakika zimefana sana.  Gwaride lilikuwa zuri na tumeburudika vya kutosha kutoka vikundi vya ngoma, ngonjera na nyimbo.
Kwa niaba yangu, ya Serikali na ya Watanzania wote nawapongeza kwa dhati Maafisa Wakuu, Maafisa Wadogo, wapiganaji na vijana wa JKT popote pale walipo kwa kusherehekea Jubilei ya Dhahabu ya uhai wa JKT.  Mnastahili kuwa na furaha na kusherehekea kama tulivyoshuhudia sote.



Historia ya JKT
Ndugu Wananchi;
Miaka 50 iliyopita, tarehe kama ya leo, yaani tarehe 10 Julai, 1963 Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa rasmi.  Huu ulikuwa ni utekelezaji wa Azimio la Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika tarehe 19 Aprili, 1963 chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Tanganyika. Wazo la kuanzishwa kwa JKT lilitokana na mapendekezo ya busara ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU Youth League), uliofanyika mkoani Tabora mwaka 1958. Wazo hili lilitolewa na Katibu Mkuu wa TANU Youth League wakati ule Ndugu Joseph Nyerere ambaye sasa ni marehemu.  Lengo kuu la kutaka kuundwa kwa JKT lilikuwa ni kuwandaa vijana kuwa raia wema, wawe na moyo wa uzalendo, na wawe tayari kulitumikia taifa lao kwa nguvu na uwezo wao wote.
Ndugu Wananchi;
            Jeshi la Kujenga Taifa lilianza na Vijana 11 kutoka Wilaya 11nchini.  Hao ndio walikuwa wa kwanza kupata mafunzo katika Kambi ya JKT Mgulani, Jijini Dar es Salaam.  Vijana hao walikuwa ni Makatibu wa Umoja wa Vijana wa TANU na wengine walimu.  Niruhusuni niwatambue watu hao kuwa ni Bi Zainabu Kiango, Bw. Sebastian Chale, Bw. Peter Lwegarulira, Bw. Rupho Kamba, Bw. Hashim Ngaliwason, Bw. John Ndimugangwo, Bw. Said Desai, Bw. Dismas Msilu (Brigedia Mstaafu), Bw. Athumani Msonge (Brigedia Jenerali Mstaafu), Bw. Reginald Mitande na Bw. Eslei Mwakyambiki.
Kati ya hao 11, walio hai ni Bi Zainabu Kiango na Brig. Jenerali Dismass Msillu ambao wapo nasi siku ya leo.  Waliosalia wameshatangulia mbele ya haki.  Mwenyezi Mungu awarehemu.  Kundi la pili liliwajumuisha Bi. M. Mhando, Bw. E. Simkone, Bw. Mwanimlele (Asst Master) Bw. AA Moyo (Asst Master) ambao walijiunga na kupata mafunzo ya uongozi.
Sheria Iliyoanzisha JKT
Ndugu Wananchi;
Mwaka 1964, Bunge lilitunga Sheria ya Kuanzisha JKT iliyoupa nguvu ya kisheria uamuzi wa mwaka 1963 wa Baraza la Mawaziri wa kuanzishwa kwa Jeshi hilo.  Kwa mujibu wa Sheria ile, kujiunga na JKT ilikuwa jambo la kujitolea kwa mapenzi ya mtu. Lakini mwaka 1966, Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho na kuanzisha utaratibu wa kujiunga na JKT kwa mujibu wa Sheria.
  Utaratibu huu uliwahusu vijana waliohitimu vyuo vikuu, vyuo vya elimu ya juu, kidato cha sita na waliomaliza kidato cha nne ambao wamepata mafunzo kwenye vyuo vya taaluma mbalimbali kama vile ualimu, uganga, uuguzi na kadhalika.    Mkurugenzi wa JKT aliwezeshwa kisheria kuwaita vijana hao kujiunga na JKT.  Mwezi Julai 1967, kikundi cha kwanza cha vijana wasomi 64 kilijiunga na JKT katika Operesheni Azimio.
            Katika kuunga mkono uamuzi wa Serikali kuhusu kuanzishwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa, viongozi na wasomi wengine waliohitimu zamani waliamua kujiunga na mafunzo ya JKT.  Mwezi Januari, 1968, kwa mfano, aliyekuwa Makamu wa Pili wa Rais, Mheshimiwa Rashid Kawawa, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa Aboud Jumbe, aliyekuwa Spika wa Bunge Chifu Adam Sapi Mkwawa pamoja na baadhi ya Wabunge na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa.  Wote walikuwa katika kambi ya Ruvu ambapo walipatiwa mafunzo ya uongozi.
Ndugu Wananchi;
Mwaka 1975 JKT iliunganishwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na hivyo kuwa sehemu kamili ya JWTZ.  Kuanzia wakati ule, Maafisa na Askari wa JKT wakawa ni wa JWTZ na kutambulika kwa vyeo vya JWTZ.  Jeshi la Kujenga Taifa liliendelea na majukumu yake ya kutoa mafunzo kwa vijana wa kujitolea na wa mujibu wa sheria.  Hata hivyo, mambo mawili ya msingi yalisisitizwa au kuongezwa katika majukumu ya JKT.  Kwanza kwamba, kuwa Divisheni ya Uzalishaji ya JWTZ yenye dhamana ya kulipatia Jeshi mahitaji yake ya chakula, mavazi na mengineyo.  Pili, kwamba JKT ndipo mahali pa kutolea mafunzo ya awali ya kijeshi na kwamba JWTZ itaajiri kutokana na wanaohitimu JKT.
Katika dhamira ya kutimiza wajibu wa kwanza kwa ufanisi, mwaka 1982 Shirika la Uzalishaji Mali la JKT (SUMAJKT) liliundwa.   Shabaha kuu ilikuwa ni kuwa na chombo madhubuti cha kupanga, kusimamia, kuratibu na kutekeleza majukumu ya uzalishaji mali na kiuchumi katika JKT kazi ambayo shirika linaendelea kuifanya hadi sasa.
Kusitishwa kwa Mafunzo ya JKT
Ndugu Wananchi
Tunapoangalia nyuma, katika historia ya miaka 50 ya kuzaliwa na uhai wa JKT tunaona wazi kuwa yamepatikana mafanikio makubwa.  Tena ni mafanikio ya kutia moyo na kujivunia.  Ninaposema hivyo, napenda nisieleweke vibaya kuwa sitambui ukweli kwamba kulikuwepo vipindi vigumu vyenye changamoto za namna mbalimbali.  Zilikuwepo changamoto kubwa na ndogo na zilizokuwa ngumu na nyepesi kuzipatia ufumbuzi. Aidha, natambua kuwa bado zipo changamoto kadhaa tunazoendelea kukabiliana nazo.  Jambo la msingi na la faraja ni kwamba pamoja na changamoto hii tumefanikiwa sana.
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa mafunzo kwa vijana, kwa mfano, zaidi ya vijana305,625 wamepitia JKT na kupatiwa mafunzo ya kijeshi na ya stadi mbalimbali za maisha katika fani na nyanja mbalimbali.  Tangu mwaka 1963 mpaka sasa yameshapita makundi (kwa jina maarufu Operesheni)102.
Bahati mbaya kwa sababu ya hali mbaya ya uchumi iliyoikabili nchi yetu kuanzia nusu ya pili ya miaka ya 1970 na kuwa mbaya zaidi miaka ya 1980 na mwanzoni mwa 1990, hali ya utoaji wa mafunzo kwa vijana katika JKT iliathirika sana.  Upatikanaji wa huduma na mahitaji kwa ajili ya mafunzo na kuendesha kambi na JKT kwa jumla ukawa mgumu.
Pengine ni vyema nikaeleza kuwa kupanda sana kwa bei ya mafuta duniani, kuanguka kwa bei za mazao yetu tunayouza nje na gharama kubwa ya vita dhidi ya Idi Amin wa Uganda ndivyo vilivyosababisha uchumi wa nchi yetu kutetereka.   Hali hii ilipunguza sana uwezo wa Serikali kutimiza majukumu yake ya msingi katika sekta, karibu zote nchini.
Ndugu Wananchi;
Kwa sababu hiyo, kwa upande wa JKT mwaka 1993, Serikali ililazimika kusimamisha mafunzo kwa vijana wa kujitolea na mwaka 1994 ilifanyika hivyo kwa vijana wa mujibu wa Sheria.  Kwa kweli baada ya mwaka 1994 shughuli za msingi za JKT zilidorora sana na kubakiza za kulinda kambi na zile Shirika la Uchumi (SUMAJKT).  Hata hizo nazo hazikuwa zinafanyika kwa kiwango kikubwa wala hazikuwa kwa ufanisi mkubwa kwa sababu ya kutokupata fedha za kutosha kutoka Serikalini. Fedha za uendeshaji wa shughuli zake zilikuwa kidogo.
Ndugu Wananchi;
            Kuifufua JKT ilikuwa ni moja ya mambo niliyoyapa kipaumbele cha juu nilichojiwekea katika mipango ya kazi baada ya kupewa heshima kubwa ya kuliongoza taifa letu Desemba 21, 2005.  Mtakumbuka kuwa katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge tarehe 30 Desemba, 2005, nilipozungumzia kufanya kila tuwezalo kujenga moyo wa utaifa na uzalendo miongoni mwa vijana, nilikuwa nazungumzia kufufua na kuimarisha Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na kuwepo kwa shule za kitaifa hasa za sekondari.
Ni ukweli ulio wazi kwamba JKT imefanya kazi kubwa na nzuri ya kujenga moyo wa utaifa na uzalendo miongoni mwa vijana waliopitia Jeshi hilo.  Hapa ni mahali ambapo vijana wa rangi zote, makabila yote, dini zote hukutana, kuishi pamoja na kufanya mafunzo na kazi kama ndugu wa nchi moja.  Hakuna chombo chochote cha malezi ya vijana kilichoizidi JKT katika kazi hiyo.  Kwangu mimi na wenzangu katika Serikali ninayoiongoza kufufua mafunzo ya vijana wa kujitolea na mujibu wa sheria lilikuwa suala kubwa na muhimu sana kulitekeleza.
Ndugu Wananchi;
            Bahati nzuri sikuwa peke yangu mwenye fikira na matamanio hayo. Watu wengi ndani ya Serikali, nje ya Serikali na miongoni mwa raia na Bungeni walikuwa wanaunga mkono mawazo hayo.  Sababu kubwa ni kuwa athari za kusimamishwa mafunzo ya JKT ziliwagusa wengi na ndiyo maana kumekuwepo na madai ya kutaka mafunzo yarudishwe.
Kule Bungeni kauli yangu kuhusu JKT iligeuka kuwa deni kubwa kwangu na kwa Serikali.  Madai ya kutaka Serikali irejeshe mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria yalikuwa yanajitokeza mara kwa mara na mwangi wake ulikuwa unaongezeka ukali kila mwaka.  Nafurahi kwamba hatimaye tarehe 26 Machi, 2013 tulifanikiwa kutimiza dhamira na ahadi yetu nilipozindua kuanza upya kwa mafunzo hayo katika kambi ya Ruvu. Kundi la kwanza limemaliza mafunzo yake na la pili limeshafika katika makambi na tayari wameanza mafunzo.
            Kama ilivyokuwa mwaka 1964 JKT ilipoanza, na mwaka 1968 baada ya mafunzo ya mujibu wa Sheria kuanzishwa, viongozi wa kitaifa waliongoza kwa mfano; safari hii Wabunge wetu alionesha.  Mwaka huu Wabunge 22 wamefanya na kumaliza mafunzo ya uongozi.  Baadhi yao wako nasi siku ya leo.  Niruhusuni nirudie kutoa pongezi zangu za dhati kwao kwa kuwa viongozi wa mfano.


Ndugu Wananchi;
            Taarifa nilizonazo ni kuwa wamefanya na kumaliza mafunzo yao vizuri.  Walikuwa na nidhamu nzuri, utii na moyo wa kujituma. Wamemaliza wakiwa ni askari wakakamavu na wenye mtazamo mpya na bora zaidi kuhusu masuala ya utaifa, uzalendo na mustakabali wa taifa letu na watu wake.
Ndugu Wananchi;
            Kwa upande wa shughuli za kiuchumi zinazofanywa na JKT tuliazimia kuwa, tutafanya kila tuwezalo kuimarisha SUMAJKT. Tumefanya mambo kadhaa kwa ajili hiyo na tumekuwa tunapata mafanikio ingawaje bado tunayo safari ndefu ya kulijenga shirika hili mpaka liwe bora kwa shughuli lizifanyazo.  Naamini tutafika pale tunapopatarajia.
 Tuliamua kutoa upendeleo maalum kwa JKT kwa kutoa shughuli na miradi kadhaa ya Serikali waitekeleze wao.  Kwa mfano, ujenzi wa nyumba na majengo kadhaa ya Serikali pamoja na ujenzi wa barabara, mabwawa ya maji na miradi ya kilimo cha umwagiliaji na kadhalika. Tumewapa JKT kazi ya kuzalisha mbegu bora kwa wakulima.  Vile vile, Serikali imechukua mkopo wa dola za Marekani milioni 40 kutoka Serikali ya India uliotumika kununua matrekta 1,846 kutoka Serikali ya India na kuipa SUMAJKT kuuza kwa wakulima kama biashara yao.
Hivi sasa mchakato unaandaliwa wa kupata mkopo mwingine wadola za Marekani milioni 92 kwa ajili hiyo.  Tumefanya yote hayo kwa makusudi mazima ya kuliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa kuwa na shirika lililoimara na linalotekeleza kwa ufanisi majukumu yake.  Halikadhalika itawezesha JKT kudumisha sifa yake nzuri katika kilimo, ufugaji, uvuvi na ujenzi.
Ndugu Wananchi;
            Napenda kuchukua nafasi hii, kuwashukuru kwa dhati ya moyo wangu, Wakuu wa JKT kumi, waliotangulia pamoja na Meja Jenerali Muhuga aliyepo sasa.  Tunawapongeza kwa utumishi wao uliotukuka na moyo wao wa upendo kwa nchi yetu na watu wake.   Mafanikio haya tunayojivunia leo yametokana na juhudi kubwa za viongozi hawa wakishirikiana na maafisa, askari na wafanyakazi raia katika kubuni na kusimamia utekelezaji wa shughuli za JKT.
Mimi na Watanzania wenzangu wote hatuna neno lingine zuri la kuwaonesha upendo wetu na shukrani zetu zaidi ya kusema asanteni sana. Tunatambua na kuthamini mchango wenu.  Tutauenzi daima.
Changamoto na Dira
Mheshimiwa Waziri;
        Pamoja na mafanikio ya kutia moyo, naelewa kuwa bado safari iliyo mbele yetu ni ndefu na imejawa na changamoto nyingi ambazo hatuna budi kuzipatia majawabu.  Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa makazi ya maafisa na askari, upungufu wa wataalamu katika miradi mbalimbali, upungufu wa vitendea kazi na vyombo vya usafiri. Baadhi ya makambi hayana miundombinu mizuri ya kutoa kwa uhakika huduma muhimu kama vile maji, umeme na kadhalika.
Napenda kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na JKT katika kutafuta njia mbalimbali za kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo. Tutaendelea kuongeza bajeti ya JKT kila mwaka na kuidhamini SUMAJKT ipate mikopo ya kutekeleza miradi yake na shughuli zake.  Tutaendelea kutoa upendeleo kwa Jeshi na JKT katika kutekeleza baadhi ya miradi ya Serikali.  Hata hivyo, nawaomba mzingatie ubora wa kazi muifanyayo ili kulinda heshima ya JKT na  kutulinda sisi tunaoamua kuwapa upendeleo.
Ndugu Wananchi;
Tunafanya haya kwa dhamira moja kubwa ya kutaka kulifufua Jeshi la Kujenga Taifa na kulifikisha mahali panapostahili na kuwa chombo madhubuti cha kutumainiwa na taifa.  Nataka JKT liwe Jeshi la kisasa zaidi, linaloenda na wakati na kutimiza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu.  Tunapenda mafunzo yanayotolewa kwa vijana wanaojiunga na JKT yaendeshwe vizuri.  Tunataka JKT itoe wazalendo wa kweli, wanaothamini utaifa, umoja na mshikamano wa Watanzania.  Vijana wanaopenda kufanya kazi kwa moyo wa kujituma na kujitolea.  Tunataka JKT izalishe askari walio hodari na wanaoweza kulinda nchi yao kwa ujasiri mkubwa.  Aidha, wanapoajiriwa na vyombo vya ulinzi na usalama na kwingineko, idhihirishe wazi kuwa vijana waliopitia JKT ni bora.  Ni watu walioiva, wa kuaminika na kutumainiwa.
Hali kadhalika, kwa wale wanaorudi uraiani kufanya shughuli nyingine wawe ni watu waliokamilika na wenye uwezo wa kusimama wenyewe na kuendesha maisha yao.  Kinachotakiwa ni kuwepo kwa utaratibu mzuri kuwasaidia wanaojiajiri waweze kuanzisha shughuli za kuwaingizia mapato kwa kutumia ujuzi na maarifa waliyoyapata.  Namna ya kuwawezesha vijana wanaomaliza JKT waanze maisha ya kujitegemea ni jambo ambalo hatuna budi kulitafakari.  Lakini leteni mapendekezo yenu tuone namna ya kuyatekeleza.
Ndugu Wananchi;
Mpaka sasa bado JKT haijafanikiwa ipasavyo kuwa divisheni ya uzalishaji ya JWTZ kama ilivyotarajiwa.  Bado haizalishi chakula cha kutosheleza mahitaji ya JWTZ.  Aidha, bado hawajaweza kutosheleza mahitaji mengine ya JWTZ kama vile mavazi na kadhalika.  Sasa wakati umefika wa kujipanga vizuri kutekeleza jukumu hilo.  JKT itumie sherehe hizi kufunga nadhiri ya kupanga na kuanza safari ya dhati ya kufanya hivyo.  Lakini, wasiishie hapo tu, JKT iweke nia ya kuzalisha ziada ya kuuza nchini na hata nje ya nchi.  Inawezekana, jipangeni vizuri ili mtimize wajibu wenu.
Rai kwa Makamanda wa JKT
Ndugu Mkuu wa JKT, Makamanda, Maafisa na Askari;
        Ni jambo linalotia faraja kubwa kwamba sote tunatambua kuwa katika miaka 50 iliyopita Jeshi la Kujenga Taifa limepata mafanikio ya kutia moyo ingawaje safari ilikuwa na vikwazo mbalimbali.  Hata huko mbele muendako hatutegemei kuwa mambo yatakuwa rahisi, changamoto mbalimbali zitaendelea kujitokeza.  Hivyo basi, kinachohitajika ni kuendelea kuwa wabunifu kufanya kazi ya ziada, tena kwa bidii zaidi, maarifa na moyo wa kujituma na kujitolea.  Hizi ni sifa ambazo mnazo, hivyo naomba muendelee kuzidumisha na kuziendeleza.
 Endeleeni kuwa chuo mahiri cha kuwafunda vijana wetu wawe na moyo wa utaifa, uzalendo, kujituma na kupenda kufanya kazi.  Wawe raia wema na wawe tayari kutoa mchango stahiki katika kujenga taifa lao.  JKT inategemewa kuendelea kuwa kitovu cha shughuli za uzalishaji mali, mafunzo ya stadi za kazi na ujasiriamali kwa vijana wetu.  Endeleeni kuimarisha JKT.
  Nawaomba mtimize wajibu wenu huo kwa ukamilifu. Msituangushe.  Nawaomba endeleeni kuwa na moyo wa kuchapa kazi, muwe  makini na waaminifu katika utendaji wenu wa kazi za kila siku. Tafadhali zingatieni sana viapo vyenu vya utumishi jeshini kwa kila ngazi ya uongozi.  Muwe na nidhamu siku zote kama mwanajeshi anavyotakiwa kuwa.  Mkifanya hivyo, nina imani kuwa katika miaka michache ijayo JKT itapiga hatua kubwa ya maendeleo.  Taifa litanufaika sana.
Shukrani kwa Israel
Ndugu Wananchi;
Nitakuwa mwizi wa fadhila kama sitatambua na kuwashukuru marafiki zetu wa Israel.  Nchi ya Israel ndiyo iliyotupatia wakufunzi wa kwanza waliotusaidia katika kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa.  Aidha, walitoa mafunzo kwa viongozi wetu kadhaa waasisi wa JKT nchini Israel. Serikali ya Israel imewakilishwa hapa leo na Balozi wake nchini Mheshimiwa Gril Haskel.  Naomba Balozi atufikishie salamu zetu nyingi za shukrani kwa Rais Shimon Peres, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na watu wote wa Israel kwa mchango wao muhimu walioutoa katika kuanzisha na kujenga Jeshi la Kujenga Taifa.  Hatasahau kamwe.

Mwisho
Ndugu Wananchi;
            Mwisho, nawashukuru, kwa mara nyingine tena, Mheshimiwa Waziri Shamsi Nahodha na Meja Jenerali Muhuga kwa kunialika. Nawashukuru wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa kwa kuja kwa wingi kushiriki katika sherehe za siku ya leo.  Na, kwa namna ya pekee nawashukuru wananchi wote waliotembelea maonesho ya shughuli zinazofanywa na JKT.    Mmejionea wenyewe na kusikia faida za kuwepo kwa JKT.  Basi tuendelee kuliunga mkono Jeshi letu, lipate mafanikio makubwa zaidi miaka 50 ijayo.
Asanteni kwa kunisikiliza

HUU NDO USHAHIDI WA KUA ODAMA WA BONGO MOVIE HUTOA PICHA ZA UONGO KUA YUPO NJE YA NCHI. TAZAMA PICHA HIZI UJIONEE MWENYEWE

EDITOR WA PICHA HII ALISAHAU KUKATA VIZURI NA KUONDOA BACKGROUND NYEUPE KWENYE ENEO LA NYWELE LILILOZUNGUSHIWA DUARA
Kuna habari tumeletewa na msomaji wa tovuti yetu ya bongo movies kumhusu mwanadada wetu muigizaji wa Filamu aliyepata tuzo hivi karibuni, Jennifer Kyaka al-maarufu kama Odama kuhusu safari zake za kwenda nje ya nchi.
Habari au tuhuma hizi tuziite, zinasema kuwa mwanadada huyo huwa haendi nje ya nchi kama anavyowaambia fans wake kupitia blog yake ya odama1.blogspot.com kuwa anasafiri kwenda nje kikazi zaidi, na badala yake inasememekana eti huwa anabaki hapa hapa nchini akizuga yupo nje ya nchi lengo ni kutafuta “KIKI” ama umaarufu kama watoto wa mjini wanavyosema.
Mdau aliyetutumia habari hizi amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha na katutumia picha mbalimbali toka kwenye mtandao mmoja wa kijamii ambako staa huyo yupo zikimuonesha akiwa maeneo mbalimbali ya “duniani huko” ambayo kwa kuangalia picha hizo anasema kuwa ni feki na zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia tuu ya ku-“edit” picha maarufu kama PHOTOSHOP
Swali ni je, hili suala ni la kweli?  Tunaomba wadau wenye majibu na utaalamu wa picha watusaidie kwa kutazama picha hizi na kutuambia kama habari hii ina ukweli wowote.
Habari kwa hisani ya Teddy Kibs
CHANZO : BONGOMOVIES.COM
ANGALIA UBORA WA PICHA YA ODAMA NI TOFAUTI KABISA NA UBORA WA PICHA YA BACKGROUND ILIYO NA MAGOROFA. PIA ANGALIA HILO BOMBA LILITAKIWA LIONEKANE VIZURI KWA SABABU LIPO KARIBU NA CAMERA LAKINI HAIKUA HIVYO. KOSA LA PILI LA EDITOR

KATIKA PICHA HII EDITOR KAKOSEA KULETA UHALISIA HAPO ODAMA KAWA MREFU SANA





VIDEO:: MADEE AMPAGAWISHA MLEVI NA KUAMUA KUVUA NGUO NA KUANZA KUCHEZA NYIMBO YA'' NANI KWAMWAGA POMBE YANGU''CHECK HAPA

Z-Anto afiwa na mama yake.




Msanii Z-Anto amefiwa na mama yake mzazi mchana huu wa leo na msiba unafanyikia nyumbani kwao maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. Tunampa pole kwa msiba huo

Lema asomewa Mashtaka mbele ya Hakimu Devota Msofe.



LEMA
Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema.
Na. Mahmoud Ahmed Arusha.
Mbunge wa Arusha mjini Mh.Godbless Lema leo amefikishwa katika mahakama kuu kanda ya Arusha kwa kosa linalomkabili la kutoa maneno ya uchochezi kwa mkuu wa mkoa Arusha,tukio lililo tokea mnamo tarehe 24 mwezi wa Aprili katika chuo cha uhasibu Njiro ambapo wanafunzi hao walikuwa wamekusanyika katika eneo hilo wakitaka kuonana mkuu wa mkoa pamoja na RPC ili kuzungumzia usalama chuoni hapo.
Akisomewa  shitaka hilo mahakamani hapo ,wakili wa serikali  Bi. Elianeny Njiro amesema mstakiwa Lema alifika chuoni hapo siku ya tukio na kuongea  maneno kwa kutumia lugha ya uchochezi  kwamba ‘amekuja kama anakwenda kwenye sendoff kauli hiyo ilichochea vurugu  kwa wanafunzi kwa kupelekea wanafunzi hao kurusha mawe, chupa, wakati huo mkuu wa mkoa alipokuwa akitoa hotuba ,hali hiyo ilipelekea uvunjifu wa amani.

Aidha tukio hilo linatokana na mauaji ya mwanafunazi Henry Koga aliyefariki  23/4 kwa kuchomwa kisu na watu wasiofahamika na  liliripotiwa polisi ambapo  polisi waliweza kufika  eneo la tukio kwa na kufanya upelelezi upelelezi  ambapo upelezi huo uliendelea na mshtakiwa  kufikishwa mahakamani  katika maelezo hayo wakili wa mshtakiwa bwana Method Kimomogoro alisema maelezo yanayokubalika  na kwamba mshtakiwa tarehe 24/4/2013 alikuwepo chuoni hapo lakini maneno yaliyosalia kwamba alitoa maneno ya uchochezi sio ya kweli.
 Hakimu aliyeendesha kesi Bi Devota Msofe alisema shauri la kesi hiyo litatajwa kwa siku tatu mfululizo  ambazo ni tarehe 20,21,22 mwezi wa nane huku kukiwa na mashahidi kwa upande wa serikali ambao ni SSP Gilles Muloto wa polisi arusha,  Inspecta Jane mkaguzi wa polisi arusha ,inspeta Benard nyambanya,PC Godfrey johachimu Wiliamu mahanyi wa polisi, Faraji kasidi  wa chuo cha uhasibu njiro ,John Joseph wa chuo cha uhasibu njiro,Benjamini simkanga wa chuo, na naibu hamidu, hata hivyo  mahakama iliridhia na shauri lililotajwa pamoja na mashahidi na dhamana kwa mshtakiwa inaendelea.

JUST IN::SOMA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO- 2013


 
 Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kuanzia mwaka huu 2013 itaanza mwezi Julai. 


Wanafunzi wamepangwa katika shule zenye miundombinu na walimu kwa masomo husika. 


Aidha, kama baadae upungufu utajitokeza, wakuu wa shule wameelekezwa kufanya taratibu za kuazima walimu wa muda na kutoa taarifa kwa uongozi wa halmashauri husika kuhusu upungufu wa walimu uliopo. 


Kwa nafasi hii, ninaagiza wanafunzi wote kuripoti katika shule walizopangwa tarehe 29 Julai, 2013. Kama kutakuwa na sababu yoyote ya msingi ya kuhamia shule nyingine, uhamisho wa kawaida utafanywa baada ya kuripoti shuleni kupitia kwa mkuu wa shule husika, Mkurugenzi wa Halmashuri/Manispaa na Katibu Tawala wa Mkoa.

 (Wizara haitabadilisha shule walizopangwa wanafunzi)

Wanaporipoti wanatakiwa kuwa na:
   Original Result slip na Living Cerificate


PHILIPO A. MULUGO (MB)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
10 Julai, 2013



WASICHANA....<<<  BOFYA  HAPA>>


WAVULANA....<< BOFYA  HAPA>>> 

 >>Ukitaka  kuya  download  bofya  hapo chini

WASICHANA:  << DOWNLOAD>>

WAVULANA:  << DOWNLOAD>>

NITAENDELEA KUPAMBANA NA WABISHI WASIOTAKA KUHAMA ILI KUPISHA MIRADI YA UJENZI"...MAGUFULI



WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ameapa kupambana kwa kuwabomolea au kuwakomesha kwa njia nyingine, watu waliogoma kuhama kwa ajili ya kupisha miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na wizara yake.
Katika hilo, tayari amekwishatangaza uamuzi mzito wa kuruhusu kampuni ya ujenzi ya Jaspal Singh, kujenga barabara kwa kiwango cha lami kwa kuzizunguka nyumba za wakazi waliogoma kuhama na kukimbilia mahakamani akiamini kuwa wataondolewa kwa kugongwa na malori yatakayokuwa yakipita baada ya barabara hiyo kukamilika.
Pamoja na hilo, Dk. Magufuli amesema atazibomoa bila kulipa fidia nyumba za wananchi nane waliokataa kufanyiwa tathmini ili kupisha mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, endapo hawatabadili msimamo wao huo.

Uamuzi huo aliutangaza jana baada ya kufanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo alibaini kuwa miradi mingi inakwamishwa na wananchi wa maeneo husika.
Akiwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Kigogo hadi Jangwani yenye kilomita 2.7, alishangazwa kuona mradi umesimama huku vifaa vikionekana kuwa na kutu kitendo ambacho kilimlazimisha ahoji.
Mhandisi Mshauri wa mradi huo, Mussa Ali pamoja na Mkandarasi Jaspal Hungh, walimueleza Magufuli kwamba kuna wananchi wenye nyumba 16 wamechukua fidia na kufungua kesi mahakamani kwa kudai kiasi walichopewa ni kidogo.
Aliongeza kuwa kesi hiyo imechukua zaidi ya miaka miwili bila kutolewa hukumu na kusababisha mradi kukwama.

TAMKO LA KIGOGO

Akizungumzia hilo Magufuli alisema: “Naomba tusiingilie mahakama lakini naagiza kuanzia leo (jana), anzeni kujenga barabara ya lami kwa kuzizungushia lami nyumba hizo na kuruhusu gari zipite, nadhani haitapita wiki kabla hazijagongwa na malori ya mchanga, sitaki kusikia Serikali inadaiwa fidia ya ucheleweshaji wa mradi.

“Pia naagiza kwamba mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki kwamba meneja wa mradi fungua kesi dhidi ya wananchi hao waliochukua fedha za fidia na kwenda mahakamani, huo ni wizi.

“Serikali ikishinda kesi ya madai yao ya fidia ndogo, wao ndio watawajibika kujenga sehemu ya nyumba zao, hatuwezi kuchezea fedha kwani kuwafidia Sh bilioni 3.8 ambapo mradi wenyewe unagharimu Sh bilioni 7.6.

“Kuna mazoea yameibuka ya watu kuchezea Serikali na mahakama, sasa nasema katika miradi ya wizara yangu nitapambana nao watu wenye kiburi cha kuchezea vyombo hivyo,” alisema.

DARAJA L A KIGAMBONI

Awali akitembelea eneo la Kigamboni uliko mradi wa daraja la Kigamboni, Magufuli aliwataka wananchi nane waliokataa kufanyiwa tathmini ya nyumba zao ili kupisha mradi huo, kubadili msimamo wao haraka kabla ya Serikali haijazibomoa nyumba hizo kwa nguvu tena bila kulipwa.

Jumla ya watu 121 walitakiwa kuhama kupisha mradi huo ambapo kati yao 113 walikubali kufanyiwa tathmini na kulipwa jumla ya Sh bilioni 11.7, lakini nane walikataa.

“Nasema Serikali ikiamua kufanya ukorofi utakuwa mkubwa kuliko msimamo wako, sasa nasema hao waliokataa kufidiwa naomba wasiambulie patupu kabla hatua hazijachukuliwa, wakubali kuchukua kiasi kitakachothaminiwa haraka, sisi tukija tutabomoa na hatukulipi na mradi utaendelea.

“Naomba daraja hili likamilike na kukabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete Januari 31, 2015 na kulifungua, sitaki kuona linafunguliwa na rais mwingine ambaye anaweza kusema yeye ndiye aliyejenga wakati ni uongo, aliyeweka jiwe la msingi ndiye atakayefungua,” alisema.

Mradi wa daraja la Kigamboni unagharimu Sh bilioni 214 na kati hizo asilimia 40 zinatolewa na Serikali wakati Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), unachangia asilimia 60.

Mbali na hilo, Dk. Magufuli ameagiza kuondolewa haraka wakazi wa eneo la Davis Corner, Temeke ambao licha ya kulipwa fidia ili kupisha ujenzi wa barabara ya Jet Corner hadi Temeke, wameshindwa kuhama mpaka sasa na badala yake kutumia fedha hizo kuendeleza ujenzi na kudai malipo mengine.

Magufuli alishangazwa kuona wananchi hao ambao wamegoma hadi sasa wamelipwa fidia Sh 15.8 huku mradi wenyewe ukiwa Sh bilioni 12 na barabara ikiwa haijakamilika.

Mradi wa mabasi ya kasi

Akikagua mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam (DARTS), Magufuli alifurahishwa na kasi pamoja na kiwango cha ujenzi wa mradi huo, ambao utapunguza msongamano wa magari.

Meneja wa mradi wa Darts, Baraka Ally alimweleza Dk. Magufuli kwamba mradi unaendelea vizuri na utakamilika kwa wakati uliopangwa.

Hata hivyo alisema changamoto kubwa inayoukabili mradi huo ni uvamizi wa wafanyabishara ambao wamekuwa wakiweka biashara zao barabarani huku wenye teksi na magari mengine wakiegesha eneo la mradi.

Vile vile alisema kuwa kuna hatari kubwa ya Jiji la Dar es Salaam kukumbwa na harufu kali kutokana na wakazi wanaoishi karibu na barabara kujiunganishia kinyemela mabomba ya maji machafu na mifereji ya mvua.

Magufuli aliagiza watu wote wanaokwamisha mradi huo kuchukuliwa hatua kali, ikiwa ni pamoja na halmashauri kuwajibika katika hilo.

MTANZANIA

NEW HIT SONG::miss_yuner_ft_Dream-hoi Download Na Sikiliza Hapa

NEW HIT SONG: STEVE RNB FT MR BLUE-HUYU DEMU DOWNLOAD NA SIKILIZA HAPA

MAKINDA - "VYOMBO VYA HABARI VINAHONGWA NA WAPINZANI ILI VIWAANDIKE VIZURI"



Spika wa Bunge, Anne Makinda, ameibuka na kauli yenye utata mkubwa akivituhumu vyombo vya habari kwamba vinahongwa na wabunge wa kambi ya upinzani ili viandike habari zao vizuri.

Bila kufafanua ni kwa jinsi gani wabunge hao wanatoa hongo hiyo mbali tu ya kusema wanatoa kitu kidogo ili waandikwe vizuri, pia alikana kuwakandamiza wabunge wa kambi hiyo na kuwabeba wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wako upande wa serikali.

Alisema hana upendeleo katika uendeshaji wa vikao vya Bunge kama anavyoshambuliwa na baadhi ya watu na kwamba lawama zinazoelekezwa kwake zinatokana na watu kuangalia upande mmoja.

Spika Makinda alitoa ufafanuzi huo jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu vurugu mbalimbali zinazotokea katika vikao vya Bunge mjini Dodoma na hasa juu ya kuporwa au kugeuzwa kwa hoja za upinzani.

Spika Makinda alikuwa ametoka kuzungumza na Spika wa Korea Kusini, Kang Chang Hee.

"Ndiyo najua mnapewa 'kitu kidogo' na hawa wanaoanzisha vurugu bungeni, lakini kusema Spika anapendelea hili siyo kweli hata kidogo,"
aliongeza Spika.

Alisema iwapo angekuwa na kawaida ya kuwakandamiza wabunge wa upinzani kwa kiasi kinachosemwa wengi wa wabunge hao wa upinzani wasingekuwapo bungeni.

“Mimi siwapendelei wabunge wa CCM, ningekuwa hivyo hawa wapinzani wasingekuwapo bungeni,” alisema Makinda muda mfupi baada ya kuzungumza na ujumbe wa Bunge la Korea Kusini uliomtembelea ofisini kwake.

Makinda alisema wakati wa kuendesha vikao vya Bunge haitakiwi kuwa na itikadi za vyama na kwamba kufanya hivyo kunaweza kusababisha vurugu.

Wakati Spika akitoa utetezi huo, wabunge wa upinzani kwa nyakati tofauti wamekuwa wakimtupia lawama za wazi hususani wanapokuwa katika vikao vya Bunge kwamba anawapendelea wabunge wa CCM.

Miongoni mwa mambo ambayo Spika Makinda amekuwa akilaumiwa ni pamoja na kukalia zaidi ya taarifa 10 za ushahidi juu ya kauli za wabunge wa upinzani zilizowasilishwa kwake na yeye kuzikalia kwa muda wote bila kusema lolote.

Miongoni mwa ushahidi huo, umo wa mawaziri kusema uongo bungeni.

Pia Spika amekuwa akilaumiwa jinsi mjadala wa hoja binafsi za wabunge wa upinzani ‘zilivyoporwa’ na serikali, kama ile ya Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, kuhusu mitalaa ya elimu; ya mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es Salaam, na hata ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari, kuhusu ardhi ya Meru.

Zote hizi ama ziligeuzwa na kupoteza maana yake hali iliyosababisha mvutano mkali bungeni ukiacha picha ya upendeleo wa dhahiri kwa baadhi wafuatiliaji wa mijadala ya Bunge.

Akizungumzia mchakato wa kupata Katiba mpya, Spika Makinda alisema Bunge la Katiba litakutana Novemba, mwaka huu na  litawajumuisha wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na wajumbe 160 ambao hata hivyo alisema sheria haijasema wanapatikana vipi.

Alisema mwezi ujao serikali inatarajia kupeleka muswada wa sheria ili kufanya marekebisho ya namna ya kupata wajumbe hao 160 ambao siyo wabunge.

Spika alisema katika Bunge hilo, yeye hatakuwa mwenyekiti na kwamba wajumbe wenyewe watachagua kiongozi atakayewaongoza.

Kauli ya Makinda iliwahi kusemwa pia na Naibu wake, Job Ndugai, mara baada ya kuahirisha kikao cha Bunge kwenye mkutano uliopita, kufuatia vurugu zilizotokea baada ya hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Wizara ya Mambo ya Nje, Ezekiah Wenje, kutamka kuwa Chama cha Wananchi (CUF) kina uhusiano na vyama vinavyounga mkono mashoga.

Wakati vurugu zikiendelea nje ya viwanja vya Bunge kwa wabunge wa CUF na Chadema kuzozana, Ndugai alipita ndipo aliulizwa na waandishi Kulikoni, lakini katika hali ya kushangaza, alivituhumu vyombo vya habari kwamba ndivyo vimesababisha hali hiyo.

“Haya yote mmesababisha ninyi waandishi, mnawadekeza sana wabunge wa upinzani, hata wangefanya nini mnawapamba pamba, lakini mkumbuke siku wakiingia madarakani watafanya haya haya wanayofanya leo,” alisema Ndugai bila kufafanua kauli yake.

Kwenye mazungumzo yake na ujumbe wa Bunge la Korea uliomtembelea ofisini kwake, Spika alisema unalenga kudumisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwamo za uwekezaji na kuendeleza uchumi wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Spika wa Korea, Chang Hee alisema nchi yake imepiga hatua kubwa ya maendeleo ingawa haina chanzo chochote cha kuzalisha nishati ya umeme ikilinganishwa na Tanzania.

Alisema Bunge la Tanzania linafanya vizuri kwa upande wa nafasi za viti maalum ikilinganishwa na Korea Kusini ambayo idadi ya wanawake bungeni ni ndogo.


Nipashe:

MAOFISA NA ASKARI WA JESHI LA MAGEREZA WALIOSHIRIKI MAONESHO YA 37 YA BIASHARA YA KIMATAIFA WAPONGEZWA KWA KUFANIKISHA USHINDI WA PILI KWA UPANDE WA UBORA WA SAMANI ZA MAJUMBANI


photoKamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Ally Malewa akitoa hotuba kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja katika hafla ya kuwapongeza Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza walioshiriki na kufanikisha Ushindi wa Pili kwa upande wa Samani za Majumbani(Home Furnitures) kwenye Maonesho ya Kibiashara ya 37(SASABA) 2013. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
photo (1)Kamishna wa Sheria na Uendeshaji  wa Magereza, Dkt. Juma Ally Malewa( wa kwanza) akifungua Muziki wakati wa Hafla fupi ya kuwapongeza Makamanda wa Jeshi la Magereza kwa kupata Ushindi wa Pili Kwenye Maonesho ya 37 ya Kibiashara ya Mwaka huu 2013. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
photo (2)Baadhi ya Makamanda wa Jeshi la Magereza Walioshiriki Maonesho ya Kibiashara ya SABASABA  wakisakata muziki  katika Hafla fupi iliyoandaliwa na Uongozi wa Jeshi la Magereza ya kuwapongeza  kupata ushindi wa pili katika Maonesho ya Kibiashara ya Mwaka huu. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam( Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
……………………….
MAOFISA NA ASKARI WA JESHI LA MAGEREZA WALIOSHIRIKI MAONESHO YA 37 YA BIASHARA YA KIMATAIFA WAPONGEZWA KWA KUFANIKISHA USHINDI WA PILI KWA UPANDE WA UBORA WA SAMANI ZA MAJUMBANI
photoKamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Ally Malewa akitoa hotuba kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja katika hafla ya kuwapongeza Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza walioshiriki na kufanikisha Ushindi wa Pili kwa upande wa Samani za Majumbani(Home Furnitures) kwenye Maonesho ya Kibiashara ya 37(SASABA) 2013. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
photo (1)Kamishna wa Sheria na Uendeshaji  wa Magereza, Dkt. Juma Ally Malewa( wa kwanza) akifungua Muziki wakati wa Hafla fupi ya kuwapongeza Makamanda wa Jeshi la Magereza kwa kupata Ushindi wa Pili Kwenye Maonesho ya 37 ya Kibiashara ya Mwaka huu 2013. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
photo (2)Baadhi ya Makamanda wa Jeshi la Magereza Walioshiriki Maonesho ya Kibiashara ya SABASABA  wakisakata muziki  katika Hafla fupi iliyoandaliwa na Uongozi wa Jeshi la Magereza ya kuwapongeza  kupata ushindi wa pili katika Maonesho ya Kibiashara ya Mwaka huu. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam( Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
……………………….
Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza walioshiriki kikamilifu kwenye Maonesho ya Kibiashara ya 37(SASABA) Mwaka 2013 wamepongezwa na Uongozi wa Jeshi la Magereza kwa kufanikisha Ushindi wa Pili katika Maonesho ya Kibishara ya Mwaka huu.
Akizungumza na Washiriki hao kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Jumna Ally Malewa amesema kuwa Ushindi huo ni wa kujivunia kwa sababu mpambano ulikuwa mkubwa na Makampuni yaliyoshiriki mengi yana uzoefu mkubwa likiwemo Kampuni la Furniture Centre, Zanzibar Furniture, Maridadi Timber Works na Jeshi la kujenga Taifa.
“Nachukua fursa hii kuwapongeza kwa kazi nzuri mliyoifanya Mwaka huu, Ushindi huu wa nafasi ya pili umetokana na kupokea maelekezo yaliyokuwa yakitolewa mara kwa mara kutoka Ofisi ya Makao Makuu kwamba vifaa vya Maonesho viwe na unadhifu wa hali ya juu, Ubunifu mkubwa na umaliziaji bora”.
Aidha Kamishna Malewa amesisitiza kwamba pamoja na kazi hiyo nzuri waliyoifanya kwa Mwaka huu ya kuonesha Ubunifu hadi kufanikiwa nafasi ya Ushindi wa pili, nafasi hiyo  iwe ni changamoto kubwa itumike kujipanga kwa Mwaka ujao wa 2014 ili Jeshi la Magereza liweze kurudi katika nafasi yake ya Kwanza.
Kwa upande wao Washiriki wa Maonesho ya Kibiashara ya Mwaka huu 2013 wameushukru Uongozi mzima wa Jeshi la Magereza ukiongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja kwa kuwawezesha na kufanikisha ushiriki wao katika Maonesho ya Mwaka huu ikiwa ni pamoja na kupitisha Bajeti ya kutosha ya maandalizi hali iliyoleta hamasa kubwa kwa washiriki hao katika Maonesho hayo ya Kibiashara ya 37(SABASABA) Mwaka 2013.
Hata hivyo, Washiriki hao  wameahidi kuendelea kufanya kazi zao kwa juhudi na maarifa ili kujenga na kulinda sifa ya Jeshi la Magereza na Nchi yetu kwa ujumla pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo ambazo tayari Uongozi wa Jeshi la Magereza unaendelea kuzipatia ufumbuzi kadri inavyowezekana.
 

WADAU MANENO YENU HAPA HIZI NI PICHA ZA WEMA SEPETU MASHABIKI WANASEMA KAHARIBIKA NGOZI NYIE MWAONAJE?

Habari Mpya :







Amber Rose na Wiz Khalifa Rasmi Wafunga Ndoa

Wiz K & Amber
Mwanamitindo mrembo na mwenye mvuto wa kipekee, Amber Rose, 29 na baba wa mtoto wake, Wiz Khalifa, 25, ambaye pia ni rapa mkali wa ngoma ya Black and Yellow wamefunga pingu za misha.

Kwa sasa wawili haoa wana mtoto wa kiume aitwaye Sebastian 'The Bash' Taylor Thomaz.

Angalia picha na tweets  zao hapo chini....