Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, July 12, 2013

HATIMAYE PESA ZA RESEARCH KWA WANAFUNZI WA MWAKA WA 3 CHUO KIKUU TEOFILO KISANJI (TEKU) KULIPWA PESA ZAO KUANZIA KESHO.

  

Vice Chancellor wa TEKU Prof. Dr. Tuli Kassimoto
Huu ni uthbitisho wa kupokea Fedha hizo leo na sio kama walivyo kuwa wakidai wanafunzi kuwa Chuo kilitunza Fedha zao katika (Fixed deposit)
Huu ni uthibitisho kutoka Bodi ya Mikopo wakati walipo anza kufanya malipo kwa ajili ya wanafunzi .

IMETOLEWA NA
UTAWALA
CHUO KIKUU CHA TEOFILO KISANJI
 
credits: Mbeya Yetu

NEW VIDEO::Izzo Bizness feat Barnaba & Shaa Tazama hapa

Toka Kenya:::Waendeshaji Matatu watoa huduma ya bure ya intaneti isiyotumia waya kwa abiria,Tanzania vp Tumejipangaje?


Dereva wa matatu akijaribu kupata intaneti isiyotumia waya katika simu yake ya mkononi. [Na Rajab Ramah/Sabahi]
Magari ya usafiri wa umma mjini Nairobi -- yanayojulikana kwa mziki wake wa sauti kubwa, kupiga honi na uendeshaji mbaya -- yanabadilisha mwenendo.
Waendeshaji wa mabasi madogo na magari madogo ya kuchukua abiria, kienyeji yanayojulikana kama matatu, yanaifanya safari ya abiria kuwa ya kufurahia na wa rahisi zaidi baada ya kuanzisha huduma za intaneti bure bila ya kutumia waya ndani ya mabasi.
"Tumekuwa tukijulikana kwa mambo yote mabaya," alisema Daniel Masava, dereva anayefanya kazi njia No. 125 kutoka katikati ya jiji la Nairobi kuelekea kitongoji cha Ongata Rongai.
"Tunaitwa madereva jeuri ambao tunapuuza sheria za barabarani na kutojali," aliiambia Sabahi. "Lakini tangu kuingizwa kwa Wi-Fi katika magari yetu, sasa tunaonekana kama kibanda cha intaneti kinachotembea tukiwa na mchango kwa uchumi."

Huduma ya Vuma Online inatangazwa nyuma ya matatu mjini Nairobi. Huduma hiyo ni ya bure kwa mabasi ya abiria na shilingi 1,500 kwa mwezi kwa waendeshaji mabasi. [Na Rajab Ramah/Sabahi]

Hapo tarehe 14 Juni, kampuni ya utoaji wa mawasiliano ya simu Safaricom Limited ilitoa huduma za intaneti bila ya kutumia waya, inayoitwa "Vuma Online", kwa kushirikiana na waendesha matatu mjini Nairobi.
Huduma hii itawapa abiria intaneti ya bure bila kutumia waya kwa matatu 200. Magari madogo yanayotumiwa kwa usafiri wa umma kwa kawaida huchukua abiria 14 wakati mabasi madogo yanaweza kuchukua hadi abiria 32.
Huduma hii iliibuka kama mpango wa majaribio ambayo ilijaribu matumizi ya intaneti bila ya kutumia waya na mwitiko wa watumiaji kwa magari 20 ya usafiri wa umma. Sasa, waendeshaji wa mabasi madogo na magari madogo ya abiria wanaweza kujiandikisha kwa huduma hii na kulipa shilingi 1,500 (dola 17) kwa mwezi, ikiwa ni pamoja na kifaa kisiyotumia waya ya kuleta intaneti.

"Wakati wa programu ya majaribio, tuligundua kwamba wateja wetu wanaotumia zaidi matatu kama njia yao ya usafiri ya kila siku wanayoipenda, walitaka wawe mtandaoni, hata pale wanapokuwa wanasafiri," alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Safaricom Bob Collymore.

"Kwa hivyo, kwa sisi kusisitiza hadithi ya intaneti na kuifanya kuwa ni njia ya maisha, ilitubidi tuwapelekee intaneti hiyo kwa kuwapatia Wi-Fi bure katika njia yao za usafiri."

Mpango huu ni wa kwanza wa aina yake barani Afrika na una dhamiri ya kuunganisha mgawanyiko wa kidigitali nchini Kenya, Collymore alisema. Vuma Online inawaruhusu watu wasioweza kumudu huduma za intaneti majumbani kwao kuweza kutumia intaneti kupitia simu zao za mkononi wakati wanasafiri, alisema.

Safaricom pia itategemea uunganishaji wa intaneti isiyotumia waya ndani ya mabasi ili kutoa habari za barabarani na kufuatilia iwapo mabasi ya umma na magari madogo yanakwenda kwa mujibu wa ratiba, Collymore.

Utoaji wa huduma za intaneti kwa vyombo vya usafiri wa umma unaongeza thamani kwa sekta hii, Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Matatu Simon Kimutai alisema, akikana wasiwasi kwamba hii itapelekea kupanda kwa ada.

"Nairobi ni mji wenye matatizo ya msongamano wa magari. Watu [wanaweza] kutumia masaa matatu barabarani, na hii imekuwa ikiwaudhi wasafiri," aliiambia Sabahi. "Lakini sasa hii imebadilika. Wanaweza kuzungumza wakiwa kwenye Facebook, kutuma ujumbe na kutumia intaneti jambo linalowafanya safari yao iwe imejaa furaha."

"Kwa sisi, ni wakati wa kusisimua kwa magari ya umma," Kimutai. "Tuna mageuzi mengi yanayoendelea nchini, lakini mbali na uvumbuzi huu mara hii kuwa unafaa sana kwa abiria, unatufanya tuwe sehemu ya safari ya kuigeuza nchi kuwa ya dijitali."

Wasafiri watathmini huduma hiyo mpya
Kwa Caroline Omondi, mwenye umri wa miaka 26, intaneti bila ya waya ndani ya matatu inamweka mbele kwa siku yake ya kazi na inamruhusu kupata masaa ya ziada ya kulala asubuhi.

Omondi alisema alikuwa anaamka saa tatu mapema zaidi ili kusafiri kutoka Kayole hadi kazini kwake mjini Nairobi kama opereta wa safari na utalii ili aweze kujibu barua pepe za kampuni kabla ya kufika saa ya harakati nyingi.

"Sasa ninaondoka nyumbani saa 2 asubuhi, na wakati ninapokuwa ofisini kiasi cha saa 3:30 asubuhi, ninatumia intaneti inayotolewa na matatu ili kujibu mahitaji yangu yote," alisema. "Kwa sasa sina wasiwasi tena wa kuamka nimechelewa."

Omar Said, mwanafunzi wa sheria mwenye umri wa miaka 23 katika Chuo Kikuu cha Nairobi, anatumia huduma za intaneti bila ya kutumia waya ndani ya basi kwa kupakua programu za matumizi kwa ajili ya simu na kompyuta yake, miongoni mwa shughuli nyengine ambazo zinamfanya awe na harakati wakati wa safari yake baina ya nyumbani na shule.

"Ninatumia angalau saa nne kwa siku katika gari la umma," aliiambia Sabahi. "Katika muda huu, ninafanya utafiti wangu na kupakua nyaraka mtandaoni ambazo ninazitumia kujenga mradi wangu ambao unatakikana mwezi ujao."

Hata hivyo, Viola Maingi, 22, alikuwa mmoja wa wasafiri walioeleza wasiwasi wao kwa huduma hii mpya, alisema ilisababisha kuongezeka kwa wizi wa simu.

"Wiki iliyopita, simu yangu iliporwa na mtu aliyejidai kuwa mtembea kwa miguu katika Barabara ya Jogoo. Simu yangu ilikuwa kiganjani na madirisha ya gari yalikuwa wazi," aliiambia Sabahi. "Woga huu ni wa kweli na ni jukumu ya wasimamizi wa matatu kuhakikisha usalama wetu ili huduma hii iweze kuwa yenye mafanikio."

Chanzo - sabahionline.com

UTUMISHI WAELEZEA MCHAKATO WA AJIRA UNAVYOKUWA NA WABAINI VYETI FEKI 677


FKB_2087FKB_2082
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,Ofisi ya Rais Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari nchini juu ya Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma, kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO)Jijini Dar es Salaam,kulia ni Katibu Msaidizi Idara ya Ajira kutoka Ofisi hiyo Bw. Malimi Muya. 
FKB_2090Katibu Msaidizi Idara ya Ajira kutoka Ofisi ya Rais Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Malimi Muya (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma, kwenye mkutano uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo Bi. Riziki Abraham na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
…………..
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  
Anwani ya simu:  “SEKRETARIET”,                                           Ofisi ya Rais
E-mail; katibu@ajira.go.tz                                                         Sekretarieti ya Ajira
            gcu@ajira.go.tz                                                            S.L.P. 63100
Tovuti: www.ajira.go.tz                                                             Dar es Salaam-Tanzania
 Fax Na.: 2153518                                                              16 Julai, 2013        
Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Uendeshaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29 (1). Jukumu la msingi la Sekretarieti ya Ajira ni kuendesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma.  Hapa ina maana  kuwa jukumu la kuajiri, kuthibitisha watumishi kazini pamoja na masuala ya nidhamu ya Watumishi yanabaki kwa Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi katika Utumishi wa Umma  mitarafu ya Kifungu cha 6(1) (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma no 8 ya mwaka 2002. Ambapo katika kuendesha mchakato huo, Sekretarieti ya Ajira inapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, na Taratibu zilizopo ili kuhakikisha Utumishi wa Umma unapata Watumishi weledi na wenye maadili mema. Hadi sasa jumla ya waombaji 4891 tumeshaendesha mchakato wao wa ajira na kuwapangia vituo vya kazi. 
Hata hivyo, Sekretarieti ya Ajira kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilipeleka Mswada Bungeni unaopendekeza kukasimu madaraka ya kuendesha mchakato wa Ajira ili baadhi ya Waajiri wakasimiwe madaraka hayo ili kurahisisha utendaji kazi katika kushughulikia  mchakato wa ajira kwa baadhi ya kada. Huku Sekretarieti ya Ajira ikiendelea kuhakikisha kuwa jukumu hilo linaendelea kutekelezwa kwa ufanisi. Tunapoongelea suala la ufanisi hapa Kitengo cha Udhibiti na Ubora kinasimamia suala zima la uhakiki wa taarifa za mhusika, uhakiki wav yeti na uadilifu wake kwa ujumla. Ambapo hadi sasa tumeshakamata  jumla ya vyeti vya kughushi 677 ambavyo wahusika wanadai wamevipata kutoka RITA, VETA na NECTA.
Nafasi  wazi za kazi zitakazokuwa zikitangazwa na mchakato wake kuweza kukasimiwa ni pamoja na Kada ya Wasaidizi wa ofisi, Wahudumu wa afya, Madereva, Maafisa Watendaji wa Kata, Mtaa, Kijiji, Wapishi, Walinzi, Madobi, Wasaidizi watunza kumbukumbu pamoja na Makatibu Muhtasi (walio chini ya cheo cha mwandishi mwendesha ofisi)  au Kada zingine ambazo Katibu wa Sekretarieti ataona inafaa kukasimu.
Aidha, nitoe ushauri kwa wanafunzi walioko shuleni na wanaotarajia kuingia vyuoni kuchukua masomo ama kozi za fani ya Afya, Elimu, Mifugo na Kilimo maana ni maeneo ambayo bado yana fursa nyingi za ajira Serikalini na wahitimu wake pindi wamalizapo wanapangiwa vituo vya kazi moja kwa moja bila ya kupitia mchakato wetu wa ajira kutokana na uhaba wa Wataalam wa fani hizo katika soko la ajira hivi sasa.
Sekretarieti ya Ajira katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa  kwa haraka zaidi zinazohusu  mchakato wa ajira katika Utumishi  wa Umma na ili kuweza kuendana na mabadiliko ya sayansi na  teknolojia ya habari na mawasiliano nchini na duniani kwa ujumla, iliamua kuanzisha tovuti yake (www.ajira.go.tz) ambayo imerahisisha  kwa kiasi kikubwa utoaji na upokeaji wa taarifa mbalimbali  hususani  za matangazo ya fursa za ajira taarifa nyingine zinazohusu masuala ya ajira Serikalini na matangazo mengine yanayohusu shughuli za Sekretarieti ya Ajira. Tangu kuzinduliwa mwezi Aprili, 2013 imeweza kutembelewa na  wadau zaidi ya 2,900,000.
Pamoja na tovuti Sekretarieti ya Ajira imeanzisha KANZIDATA (DATABASE)  za aina tatu (3) ambazo ni Kanzidata ya Wahitimu wa Vyuo, Kanzidata ya waliofaulu usaili na Kanzidata ya waliopangiwa vituo vya kazi.
Jambo lingine ambalo ningependa mkalifahamu ni kuwa, Sekretarieti ya Ajira iko katika hatua za awali za mchakato wa kuwawezesha waombaji wa fursa za ajira kuwasilisha maombi ya kazi kwa mfumo wa kielektroniki (e-application) kwa nafasi wazi zitakazokuwa zikitangazwa katika Utumishi wa Umma ili kurahisisha kupunguza mlolongo wa uendeshaji mchakato wa ajira ulivyo hivi sasa.
Mwisho nimalizie kwa kuwataka waombaji wa fursa za ajira kutokuchagua maeneo ya kufanyia kazi, hususani wale wanaopangiwa vituo vya kazi na Sekretarieti ya ajira na hawaendi kuripoti bila ya kutoa sababu za msingi maana Sekretarieti ya Ajira inaona hili ni kosa na inaandaa utaratibu wa kutowaruhusu kufanya usaili mwingine waombaji kama hao.                   
Imetolewa na Riziki V.  Abraham, Msemaji na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma  +255-687624975

ASKARI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA ANASWA NA JINO LA TEMBO MKOANI MANYARA


Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa na jino la tembo mkoani Manyara hivi karibuni. Picha kwa hisani ya World Elephant Centre

WANAFUNZI WA TEOFELO KISANJI(TEKU) JIJINI MBEYA WAGOMA WAKISHINIKIZWA WALIPWE PESA ZAO ZA RESEARCH ZAIDI YA MIL.100


Wanafunzi wa Chuo kikuu cha  TEKU wakiwa wanajikisanya kusikia uongozi wa chuo uatoa Tamko gani, huku wakipiga kelele
 Baadhi ya wanavyuo wakiwatimua wanafunzi wenzao walio  nje na kuwambia kamahawawezi bora warejee makwao
 Wakati  Vice Chancellor wa TEKU akionge nyuma Dr. Tuli Kazimoto huku nyuma waandishi wa Habari walikuwa wakikatazwa wasichukue habari
 Depute Vice Chancellor Academic affairs  akiwa katika kikao kifupi na wanafunzi nje ya ofisi
 Hili ndilo Tamko Lililo leta utata kwa wanachuo hao wanadai pesa zao za Research
Wanafunzi wa Chuo cha TEKU waakilikataa Tamko hilo

RAIS KIKWETE AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA KUWAIT IKULU DAR ES SALAAM JULY 12, 2013


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait na Waziri wa mambo ya Nje wa Kuwait Mhe Sabah Khalifa aliyemtembelea leo Ikulu Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait na Waziri wa mambo ya Nje wa Kuwait Mhe Sabah Khalifa na ujumbe wake aliyemtembelea leo Ikulu Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait na Waziri wa mambo ya Nje wa Kuwait Mhe Sabah Khalifa na ujumbe wake aliyemtembelea leo Ikulu Dar es salaam

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA ANAYESHUGHULIKIA AFRIKA IKULU


 Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kwanza 20 na wakufunzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence College waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo July 12, 2013, ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuhitimu mafunzo yao hayo ya mwaka mmoja. Rais Kikwete aliwapongeza washiriki hao pamoja na wakufunzi wao kwa mafanikio mazuri ya chuo hicho cha kipekee kinachojumuisha washiriki kutoka vikosi vya ulinzi na usalami pamoja na taasisi za serikali
 Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya bilauli toka kwa  Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala wakati washiriki wa kwanza 20 na wakufunzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence College walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo July 12, 2013, ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuhitimu mafunzo yao hayo ya mwaka mmoja. Rais Kikwete aliwapongeza washiriki hao pamoja na wakufunzi wao kwa mafanikio mazuri ya chuo hicho cha kipekee kinachojumuisha washiriki kutoka vikosi vya ulinzi na usalami pamoja na taasisi za serikali
 Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya nembo toka kwa  Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala wakati washiriki wa kwanza 20 na wakufunzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence College walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo July 12, 2013, ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuhitimu mafunzo yao hayo ya mwaka mmoja. Rais Kikwete aliwapongeza washiriki hao pamoja na wakufunzi wao kwa mafanikio mazuri ya chuo hicho cha kipekee kinachojumuisha washiriki kutoka vikosi vya ulinzi na usalami pamoja na taasisi za serikali
Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na washiriki wa kwanza 20 na wakufunzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence College walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo July 12, 2013, ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuhitimu mafunzo yao hayo ya mwaka mmoja. Rais Kikwete aliwapongeza washiriki hao pamoja na wakufunzi wao kwa mafanikio mazuri ya chuo hicho cha kipekee kinachojumuisha washiriki kutoka vikosi vya ulinzi na usalami pamoja na taasisi za serikali.PICHA NA IKULU

Serikali yatangaza kima cha chini mishahara ya kisekta

elimu
Na Raymond Kaminyoge, Mwananchi
Dar es Salaam. 
Serikali imetangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisekta ambavyo vinatofautiana kati ya sekta moja na nyingine ambavyo ni kuanzia Sh40,000 hadi Sh400,000 kwa mwezi kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema, watakaolipwa kima kidogo zaidi cha Sh40,000 ni wafanyakazi wa nyumbani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao.
Kwa upande mwingine, katika viwango hivyo, kima kikubwa katika viwango hivyo cha Sh400,000 kitalipwa kwa wafanyakazi wa sekta za mawasiliano zikiwamo kampuni za simu, kampuni za kimataifa za nishati, madini na taasisi za fedha.
Katika viwango hivyo, mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na watu wa kawaida lakini ambao hawaishi kwenye nyumba za waajiri wao itakuwa Sh80,000.
“Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na mabalozi wa kigeni na wafanyabiashara maarufu wanatakiwa kulipwa Sh150,000 kwa mwezi,” ilisema taarifa hiyo.
Wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na maofisa wa Serikali watalipwa Sh130,000 kwa mwezi.
Kima cha chini cha mshahara katika huduma za kilimo ni Sh100,000 na huduma za afya Sh132,000.
Kwa upande wa wafanyakazi wa vyombo vya habari, posta na usafirishaji wa vifurushi ‘courier services’, kima cha chini kitaanzia Sh150,000.
Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa hoteli za kitalii kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ni Sh250,000, wakati kwa hoteli za kati ni Sh150,000 na migahawa, nyumba za wageni na baa ni Sh130,000.
Kampuni za ulinzi za kimataifa zitapaswa kulipa kiwango cha chini cha mishahara cha Sh150,000 kwa wafanyakazi wake sawa na kampuni ndogo za huduma za nishati.  Kampuni ndogo za ulinzi zitatakiwa kulipa Sh100,000.
Kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kitakuwa Sh300,000, sawa na wale wa utoaji na uingizaji wa mizigo. Wafanyakazi wanaofanya katika sekta ya usafirishaji wa majini, uvuvi na nchikavu wakitakiwa kulipwa Sh200,000.
Kima cha chini kwa kampuni za makandarasi daraja la kwanza kitakuwa Sh325,000, makandarasi daraja la pili hadi la nne Sh280,000 na makandarasi daraja la tano hadi saba Sh250,000.
HABARI HII IMEHAMISHIKA KUTOKA GAZETI LA MWANACHI LEO

PICHA ZA WEMA ZANASWA AKIBADILISHANA MATE NA JAMAA

 
Video inayomuonesha staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akidendeka na mwanaume imevuja mtandaoni...



Haikuweza kufahamika mara moja lengo la Wema na mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Aidany ‘kujishoot’ wakifanya vitendo hivyo ila wanaonekana wakiwa katika mazingira ya ki-Mr & Mrs.



Aidha, katika video hiyo, Wema anaonekana kutumia nguvu kubwa kumshawishi Aidany amsogezee mdomo lakini mwanaume huyo anasita na hata alipokubali kudendeka hakutoa ushirikiano wa asilimia 100.


Mwanaume fegi mkononi
Katika video hiyo, mwanaume huyo anaonekana kutumia muda mwingi kuvuta sigara yake huku Wema akiwa bize kumpapasa kimahaba.


Ni filamu?
Baada ya video hiyo kunaswa swali lililokuja ni je, ni sehemu ya filamu za mwanadada huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame au ni uhalisi wa mambo!

 Katika kujua ukweli, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Wema kupitia simu yake ya mkononi lakini mara nyingi imekuwa ikiita bila kupokelewa.

Aidha, mwandishi alichukua hatua ya kwenda nyumbani kwake maeneo ya Kijitonyama jijini Dar lakini alimkosa na hata alipokwenda ofisini kwake hakuweza kumpata.


Source: Gazeti la ijumaa


TAZAMA KWA UMAKINI HUYU NDIO MZEE MWENYE NGUVU SANA ANAWEZA KUBEBA MIFUKO 6 YA SIMENTI KWA MKUPUO



NEW SONG::BZQ --Shughale Remix(Producer Dayo Music)

Mtangazaji Maarufu Oprah Winfrey anatarajiwa kutua Tanzania kesho.

. 
Inaelekea President Obama kaacha upepo mzuri Tanzania manake taarifa zilizotufikia muda mfupi uliopita baada tu ya bondia Evander kuthibitishwa na yeye kuja Tanzania, mtangazaji staa wa dunia Oprah Winfrey nae anatarajiwa kufika Tanzania.
Staa huyu ambae amewahi kufanya interview na mastaa wengine kama marapper  Jay Z na 50 Cent, unaambiwa usitegemee kumuona Dar es salaam au sehemu nyingine maarufu za town, anatua Serengeti kesho July 13 2013 kwa ajili ya mapumziko tu na kuondokea hukohuko.


TANGAZO LA KAZI KUTOKA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA


Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma  

Sekretarieti ya Ajira kwa niaba ya Tanzania Dairy Board, Tanzania Institute of Accountancy, College of Business Education, National Institute of Transport, Tanzania Broadcasting Cooporation, Tanzania Institute of Education, Tanzania Library Services Board, Local Government training Institute, Institute of Finance Management, National College of Tourism Agency, Law school of Tanzania, Tanzania Metrological Agency, Moshi Unoversity college of cooperative and business Studies, Dar es Salaam Marine Institute, Kibaha Education Centre, Institute of Rural Develepment Planning, Tanzania Public Service College, Tanzania Wildlife Research institute, Institute of Accountancy Arusha na National Examination Concil of Tanzania inawatangazia furasa mbalimbali za Ajira Serikalini, Kwa maelezo zaidi fungua kwenye TOVUTI ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ambayo ni www.ajira.go.tz. 


TANGAZO LA KAZI-JULY 2013. 


Chanzo: www.ajira.go.tz.

IRENE UWOYA AFUNGUKA BAADA YA DIAMOND KUMLIPUA JANA

Kuna saa najiuliza kwanin ukimwamin mtu ndio anageuka...kwanin ukiwa muwaz watu wanakuchukulia vbaya? Leo nimeumia sanaaa kuliko skuzote...sijaamini mtu niliye mwamini kumuona kama rafiki yangu anaweza kuongea shit kuhusu mim...au najiuliza siruhusiwi kuwa na rafik wa kiume? Lakin sa nyingine nakaa chin nasema God ...u know me better” alifunguka Uwoya.
Sababu kubwa iliyodaiwa kumfanya Diamond atembee na Uwoya ni kitendo cha muigizaji huyo kudaiwa kumponda mara kwa mara na alikuwa hampendi Diamond ambaye alikuwa anafikishiwa habari hizo na marafiki zake Irine.



Kama hukufanikiwa kusoma habari hiyo iliyoripotiwa jana basi isome hapa http://audifacejackson.blogspot.com

KILA MTANZANIA NI LAZIMA ALIPIE SH. 10000 KWA AJILI YA KADI YA SIMU YAKE"....WAZIRI WA FEDHA AMESISITIZA TENA


 SERIKALI imesisitiza kuwa itatoza Sh 1,000 kwa kila kadi ya simu inayotumika lakini pia inaangalia utaratibu wa kufanya makato hayo kwa njia ambayo haitamuumiza mtumiaji wa simu.
Akizungumza jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa alisema kuwa kupitia tozo hizo wanatarajia kukusanya Sh bilioni 160 kwa mwaka.
“Kupitia wawakilishi wenu na sisi serikali kuwa sikivu, tulishauriwa na ikaonekana kwamba kuna uwezekano wa kupata chanzo kingine cha mapato kupitia kadi za simu”alisema.
Alisema katika mapendekezo yaliyokuwa yametolewa serikali ilishauriwa kutoza Sh 1,450 katika kila kadi ya simu lakini baada ya kukaa na kushauriana serikali iliona ni vyema ikatoza Sh 1,000 ili kila mwananchi aweze kumudu gharama ambapo kwa mwaka kila mmiliki wa kadi ya simu atatozwa sh 12,000.

Alisema baadae serikali ilipokea mapendekezo mbalimbali ili kuangalia kama hilo linaweza kutekelezeka na walipita ngazi zote kabla halijapelekwa katika kamati za Bunge na kushauriwa kwamba tozo hilo linaweza kufanyika kwa lengo la kukuza uchumi hasa maeneo ya vijijini.

“Tathmini zote zimefanyika kikamilifu na baadae suala hilo likafikishwa Bungeni ambapo pia napo lilikubalika... inawezekana watu wanalalamika lakini ngazi zote suala hilo lilipopita lilikubalika na ikaonekana ni sawa kutozwa sh 1,000 kwa kila kadi ya simu” alisema.
Alisema kutokana na hilo kwa kutwa nzima kadi ya simu itatozwa Sh 33.35 au Sh 100 kwa siku tatu ambapo serikali inaangalia utaratibu mzuri ambao hautamuumiza mtumiaji wa simu.

Dk Mgimwa alisema fedha hizo zitakazokusanywa zitaongeza upatikanaji wa maji vijijini, umeme pamoja na kuboresha miundombinu katika maeneo ya vijijini.


Habari Leo

ANGALIA PICHA YA CHANGUDOA" MWENYE ULEMAVU WA NGOZI ALIYE HUKUMIWA ZAIDI YA MARA TANO KWA KOSA LA "UCHANGUDOA"


Emmily Omari akiwa selo.
 MREMBO mwenye ulemavu wa ngozi, Emmily Omari, 23, mkazi Buguruni, Dar anayedaiwa kujihusisha na biashara haramu ya uchangudoa, hivi karibuni alipandishwa kizimbani kwa madai ya kufanya kosa hilo.
Emmily ambaye amekuwa akiwatesa askari polisi ambao wamekuwa wakimkamata mara kwa mara na kumfikisha mahakamani lakini haachi tabia hiyo, alipandishwa katika Mahakama ya Jiji na kusomewa mashtaka yake.
Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo, Timothy Lyon alipigwa butwaa kumuona mrembo huyo ambaye aliwahi kumhukumu zaidi ya mara tano kwa kosa la kujiuza na kumuachia huru baada ya kulipa faini.NA VITUKO VYA MTAA


Pilato huyo baada ya kumuona tena Emmily mbele yake akikabiliwa na shitaka lilelile, alimuuliza alikuwa na tatizo gani lililosababisha mara kwa mara afikishwe mahakamani hapo, mrembo huyo hakujibu chochote. “We Emmily sasa unatuletea utani, kila siku unaletwa hapa tunakupiga faini unalipa unatoka na kwenda kurudia hiyo biashara yako… sasa tunaona kama unatufanyia masihara  sasa leo hakuna cha faini wala dhamana uende Segerea ukale dona la bure labda utajifunza,” alisema Hakimu Lyon na kuwaamuru askari wampandishe kwenye Karandinga kwa ajili ya safari ya gerezani.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana juzikati zinaeleza kuwa mrembo huyo baada ya kukaa Segerea kwa wiki mbili, alipewa dhamana wakati mahakama ikiendelea kumjadili.

MAGAZETI YA LEO TAR 12.07.2013 VICHWA VIKUBWA MISHAHARA MIPYA HII HAPA,WANAINCHI WAMPORA ASKARI SILAHA NA RISASI 30 NA TANZANIA:KAGAME KAMWE ASIDHUBUTU.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
CREDIT MILLARD AYO
.