Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 5, 2013

Angalia PICHA HUU NDO MUONEKANO WA MH.MNYIKA NA MBOWE KABLA YA KUWA WABUNGE...

KESI YA MUME WA JOYCE KIRIA AITWAYE.. HENRI KILEWO NA WENZAKE YAFUTWA NA MAHAKAMA, SASA WAPO HURU


clip_image001Watuhumiwa wa Kesi  ya ugaidi  iliyokuwa inawakabili wanachama wa Chadema akiwemo Henry kilewo wameachiwa Huru Baada ya Kesi Yao kufutwa na jaji katika mahakama kuu Huko Tabora

HILI NDILO GARI LENYE THAMANI YA MILLION 150 ANALOMILIKI STAR WA BONGO IRENE UWOYA




OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Irene Uwoya ambae ni Mrs Ndikumana akiwa pia ni mama Krish hivi karibuni ameingia kwenye headlines na TV show yake mpya kabisa ambayo itaoneka @CloudsTV jumanne wiki hii,

Ni Mercedes Benz S Class 550 Sedan yenye rangi ya Black metalic ambapo japo gharama imebaki kuwa siri ukicheki kwenye mtandao wa Mercedes Benz US ndinga kama hii ikiwa mpya ina-cost $ 95,000.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA

OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA

ANGALIA PICHA::JAMBAZI LANUSURIKA KIFO MBEZI JIJINI DAR


Jambazi likiwa hoi baada ya kichapo kutoka kwa wanachi.
Jambazi hilo likihojiwa.
Mmoja wa wanausalama (mwenye tisheti yenye mistari) akiwa na bastola aliyokutwa nayo jambazi huyo.
Wananchi wakiwa eneo hilo la tukio.
Wanausalama wakishauriana jambo kabla ya kulipiga pingu jambazi na kulipeleka hospitali.
Baada ya kichapo kikali jambazi lilipelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
KIJANA mmoja ambaye hajafahamika jina lake anayedaiwa kuwa ni jambazi amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali eneo la Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es Salaam. Kijana huyo pamoja na mwenzake wakitumia pikipiki walikuwa na silaha za moto tayari kwa kwenda kufanya uhalifu lakini kabla mpango wao haujakamilika polisi waliingilia kati na kuanza kupambana nao. Haikuwa kazi rahisi kuweza kumkamata jambazi huyo kutokana na majibizano ya risasi kati yake na polisi. Baada ya jambazi lililokuwa linaendesha pikipiki kuona mwenzake anaelekea kukamatwa lilitokomea wakati mwenzake akiangukia mikononi mwa wananchi wenye hasira kali waliomshushia kipondo cha nguvu.
(PICHA NA GPL)

EXCLUSIVE: MWINYI KAZIMOTO AKIWA NA RAUL GONZALEZ BLANCO MAZOEZINI QATAR - AONGEA RASMI KUHUSU HATMA YAKE

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba Mwinyi Kazimoto akiwa na Gwiji wa soka wa Hispania na Real Madrid Raul Gonzalez huko Qatar alipokuwa ameenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa. Mtandao huu umepata nafasi ya kuongea na Kazimoto na kwa kifupi ameomba radhi kwa kutoroka - pia amesema amefanikiwa kupata timu huko alipo. Je ungependa kujua Simba imelipwa shilingi ngapi kwenye uhamisho huu wa Kazimoto???? - Endelea kutembelea mtandao huu.

UNAMKUMBUKA MBABE WA MADEREVA DALADALA NA MAKONDA DAR?HUYU HAPA DAVID MWAIBULA



a6 cd3fd

Na ubabe wa maana ni ule ubabe wa kusimamia taratibu.
David Mwaibula alikuwa ni mmoja wa wababe wa Dar es salaam kwenye kusimamia taratibu. Juzi hapa nilikutana na kuongea naye kwenye moja ya vijiwe vya jijini Dar.

Hakika, jamaa alikuwa ni msimamizi mkuu na mahiri wa masuala ya Daladala jijini. Huyu alikuwa haswa ' Mzee wa Daladala'.

Mbali ya mabadiliko mengine, ndiye aliyeasisi utaratibu wa madereva na makondakta wa daladala kuvaa sare.

Na jamaa alikuwa mbabe haswa. Akimkuta kondakta amevaa kandambili alimshusha na kumwambia arudi nyumbani akafuate viatu vyake. Maana, kwa Mwaibula, mtu lazima uheshimu kazi yako. Huwezi kwenda kazini na kandambili.

Hakika, nchi kwa ujumla inahitaji kuwa na idadi fulani ya ' Wababe' wenye ujasiri wa kuanzisha mambo mapya na wenye kuhakikisha taratibu zinafuatwa. Na hapo nchi hiyo lazima itasonga mbele kimaendeleo.
CHANZO Maggid,

majina 8,805 yakataliwa tcu

blogger-image-1885083474 9b6ea
Hussein Makame, MAELEZO
TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imekataa kuyachagua majina ya wanafunzi 8,805 walioomba kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza katika taasisi za elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2013/2014 kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza kwenye fomu zao za maombi.
hdg

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Sifuni Mchome, wanafunzi hao hawakuchaguliwa na tume hiyo kujiunga na vyuo vikuu kutokana na maombi yao ya programu zote walizochagua kushindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa.
Ilieleza taarifa hiyo kuwa sababu za kutochaguliwa kwa wanafunzi hao ni pamoja na ushindani wa wanafunzi katika programu walizochagua, wanafunzi kushindwa kuwasilisha programu walizochagua na kuchangua programu ambazo hawana sifa nazo.
Hata hivyo, taarifa hiyo imewapa nafasi nyingine wanafunzi hao kuomba tena kwa awamu ya pili kwa kuchagua programu nyingine ambazo wana sifa nazo kupitia mfumo wa udahili wa TCU ambao umeshafunguliwa tangu Julai 29 hadi Agosti 9 mwaka huu utakapofungwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwanafunzi anatakiwa kuangalia jina lake katika orodha ya wanafunzi ambao hawakuchaliwa na TUC, orodha inayopatikana kwenye tovuti ya taasisi hiyo ya www.tcu.go.tz na kufuata utaratibu uliowekwa kuomba upya.
"Baada ya mwanafunzi kuthibitisha jina lake kwenye orodha ya wanafunzi ambao hawakuchaguliwa iliyoko kwenye tovuti ya TCU, unatakiwa kufuata masharti yafuatayo, chagua program moja tu kutoka kwenye orodha ya programu inayopatikana kwenye tovuti ya TCU" alisema sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa masharti hayo, pia mwanafunzi anatakiwa kufungua muongozo wa udahili unaopatikana kwenye tovuti hiyo na kuthibitisha kwamba anayo sifa stahiki ya kujiunga na programu aliyoichagua.
Masharti hayo pia yanamtaka mwanafunzi ambaye hakuchaguliwa, kuingia kwenye sehemu ya taarifa za mwanafunzi (profile) kwa kuingiza jina analotumia na namba yake ya siri, kubofya kitufe cha kuomba, kuchagua programu moja tu, kubofya kwenye makasha ya kuthibitisha na hatimaye kuwasilisha maombi yake.
"Baada ya kuwasilisha maombi yako mfumo wenyewe utakutaarifu kuwa ama unastahiki kuomba programu hiyo au la, na uchaguzi utaegemea kwenye msingi wa wa kwanza ndiye atakayehudumiwa mwanzo"ilisisitiza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa:
"Pindi programu moja itakapojaa, haitaoneshwa kwenye orodha ya programu zinazohitaji kujazwa kwenye mfumo wa udahili, hivyo utahitajika kujaza programu nyingine"
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwisho wa kutuma tena maombi hayo ni Agosti 9 mwaka huu na iwapo mwanafunzi atapata tatizo kuhusu maombi hayo atatakiwa kuwasiliana na TCU kwa anuani au kupiga simu namba 0757 593868; 0757 594087; 0656 596822 na 0682 544832 au afike kwenye ofisi za tume zilizoko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
mwisho

Wanafunzi 5,000 washindwa kuingia vyuo vikuu

057 23c5b
Siku chache baada ya kufungwa kwa pazia la udahili kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioomba kujiunga na vyuo vikuu nchini, imebainika kuwa zaidi ya wanafunzi 5,000 wameshindwa kujiunga na vyuo hivyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo matumizi ya mtandao wa kuomba udahili. (HM)
 
Pazia la udahili huo kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka huu, lilifungwa rasmi Julai 5, mwaka huu. Hadi wakati unafika tarehe hiyo, wanafunzi waliokuwa wameomba nafasi hiyo ni 39,140.

Matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, yanaonyesha kuwa watahiniwa 50,611 walifanya mtihani huo na kati yao 44,366 sawa na watahiniwa wa shule waliofaulu ni 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya waliofanya mtihani huo.
 
Watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo walikuwa ni 7,659 na waliofaulu ni 4,124 sawa na asilimia 53.87. Kutokana na matokeo hayo, watahiniwa wote waliofaulu ni 44,366, hivyo kufanya wanafunzi walioshindwa kujiunga na vyuo vikuu kuwa 5,226.
 
Akizungumza na Mwananchi Jumamosi, Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Dk Savinus Maronga alisema, wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kuomba kujiunga na vyuo vikuu ni 39,140 na kwamba vyuo vikuu nchini vina uwezo kwa kuchukua wanafunzi 60,000.
 
Dk Maronga alisema hali hiyo inatokana na baadhi yao kutokuwa na sifa zinazotakiwa kuweza kuomba udahili wa kumwezesha kusoma elimu ya juu.
 
“Kuna baadhi hawana sifa ‘Eligibility’ za kuweza kuchaguliwa kuingia Chuo Kikuu. Hivyo ili uweze kudahiliwa kuendelea na elimu ya juu ni lazima uwe na vigezo. Kuhusu mfumo sidhani kama ulikuwa na matatizo yeyote,” alisema Dk Maronga
 
Kauli za Wanafunzi
Wanafunzi waliozungumza na gazeti hili kuhusu mfumo huo wa udahili wa mtandao, walisema una usumbufu kutokana na wengi kutokujua kuutumia.
 
Frank Mabagala aliyehitimu Shule ya Sekondari Pugu Jijini Dar es Salaam, alisema wanafunzi walio wengi wameshindwa kuutumia mfumo huo kwani una mambo mengi ya kufanya.
 
“Nilijaza fomu vizuri tu, lakini sikuwa najua kama kuna wakati nilitakiwa kwenda kuangalia ‘Eligibility’ hadi nilipoambiwa na rafiki yangu kwenda kuangalia ‘Eligibility’ na kukuta kuna nafasi imeandikwa ‘NO’ hapana vyuo vyote nilivyochagua,” alisema Mabagala.
 
Alisema hata upatikanaji wa vocha za TCU bado zilikuwa tatizo, kutokana na kupatikana sehemu moja tu ya Benki ya NBC. Hivyo kwa watu wanaoishi pembezoni mwa benki hiyo kuwawia vigumu kupata huduma hiyo kwa haraka.
 
“Mfano mimi ninaishi Tegeta lakini nilikwenda benki pale Tegeta nikakuta zimekwisha,.Nikaenda Mliman City nako nikakuta vivyo hivyo hadi nilipokwenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ndipo nikazikuta nako kulikuwa na foleni,” alisema Mabagala na kuongeza:
 
“Kama Dar es Salaam upatikanaji wa vocha inakuwa hivi, je, kwa wanaoishi pembezoni mwa mkoa ambako benki kuifikia ni kazi, watu wa aina hii watakuwa wamepata usumbufu mfano ni rafiki zangu watatu wa mkoa walinitumia fedha huku ili niwanunulie vocha na kuwatumia.”
 
Naye Zahora Miraji aliyehitimu kidato cha sita Shule ya Seminari ya Ridwaa jijini humo, alisema alijaza fomu kulingana na maelekezo yalivyokuwa, lakini katika hali ya kushangaza amekuta kile alichokijaza kimebadilishwa.
 
Miraji alisema, katika chaguo la vyuo, chaguo la kwanza na pili aliomba Chuo cha Mkwawa, la tatu na nne aliomba Chuo cha Dodoma na chaguo lake la tano aliomba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lakini alipokwenda kuangalia kwa mara ya mwisho akakuta amebadilishiwa.
 
“Nilijaza vizuri na nilipokuwa nikifungua kuona kinachoendelea ninakuta bado iko katoka ‘mchakato’ lakini nilipokwenda tena kuangalia nikakuta vyuo nilivyoomba vya Mkwawa, Dodoma na Dar es Salaam vyote vimebadilishwa sasa sikujua tatizo ni nini,” alisema Miraji na kuongeza:
 
“Nilikuta chagua la kwanza na la pili nimeandikiwa chuo cha Jordan na hata sijui kipo wapi na chaguo la tatu hadi la tano Chuo cha Usafirishaji Marrine. Nilikwenda TCU kuwaeleza kilichotokea wakanipa fomu nikaijaza kuonyesha tatizo langu sasa sijui kama watalishughulikia au la.”
 
Kauli ya Chuo
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekeza Mukandala, alisema mfumo huu ni mzuri kutokana na kuepusha usumbufu uliokuwepo awali.
 
Alisema kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ni lazima nchi ibadilike, kwa kuwa mfumo wa kujaza kwenye makaratasi ilikuwa inaongeza ufanisi.
 
“Kama kuna matatizo hakuna budi kuufanyia marekebisho ili uweze kutoa huduma kwa ufanisi lakini kweli ni mzuri na siyo mwisho, kwani TCU wataufungua tena na wanafunzi wataweza kuomba tena,” alisema Profesa Mukandala. Chanzo: mwananchi

SITA:WABUNGE WA VITI MAALUMU HAWANA UMUHIMU WOWOTE



 Spika wa Bunge wa zamani, Samuel Sitta
Wiki moja baada ya kukaririwa akisema baadhi ya wabunge wa CCM ni mizigo na kwamba hawana mchango wowote bungeni na wala hawatembelei majimbo yao wakisubiri kubebwa na chama, Spika wa Bunge wa zamani, Samuel Sitta amewageukia wabunge wa Viti Maalumu akisema hawana umuhimu wowote.
Akizungumza kwa simu juzi, Sitta ambaye sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema: “Ninakerwa sana na mfumo wa Viti Maalumu, kwanza sioni umuhimu wa mfumo huu kuendelea kuwepo katika Katiba Mpya. Hawana umuhimu wowote.”
Katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Nyamikoma, Kata ya Busega Mkoa wa Simiyu Julai 29, mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kampeni za kuimarisha uhai wa chama, Sitta aliwajia juu bila ya kuwataja baadhi ya wabunge wa CCM.
“Wanakwenda bungeni hawachangii, hawana hata hoja za kuchachafya upinzani, hawachangii, hawa ni mzigo,” alisema Sitta na kuongeza: “Wapo baadhi ya wabunge, hawajawahi hata siku moja kwenda kwenye majimbo yao kuwatembelea wananchi waliowachagua... Inawezekana hata wapiga kura wakawa wamewasahau. Hawa hawafai hata kuchaguliwa wakiomba tena kura.”
“Rais Jakaya Kikwete amejitahidi sana kuleta mabadiliko, ameleta mafanikio ya uchumi na mambo mengi. Inatakiwa wabunge waende wakawaeleze wananchi maendeleo haya, inawezekana hawayajui lakini watu hawaendi jimboni, wananchi watayafahamu vipi haya maendeleo?”
Juzi, akizungumzia wabunge wa Viti Maalumu, Sitta alisema... “Wengi wao hawachangii chochote na mbaya zaidi hakuna wa kuwahoji chochote kama wabunge wanavyorudi jimboni.
“Ikifika wakati wa posho wapo. Sisemi kama naumia wao kuchukua posho.... hawa wanachukua posho wanawajibika kwa nani? Nani anahoji utendaji wao na zaidi itakapokuja Katiba Mpya ya kuwawajibisha wabunge wazembe, hawa watawajibishwa wapi?”
“Rasimu ya Katiba Mpya isiwaruhusu hawa... hawa nao ni mzigo mwingine. Wakifika bungeni hawachangii chochote, hawawezi kuwajibishwa na yeyote kwa mfumo uliopo na pia hawawajibiki popote, sasa huu si mzigo?”
Walikwishaanza mkakati
Hata hivyo, Juni 9, mwaka huu, ikiwa ni wiki moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kutangaza Rasimu ya Katiba huku ikifuta Viti Maalumu, wabunge wanawake walianza kuweka mikakati ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa lengo la kukamata majimbo.
Kwa  mara ya kwanza, wabunge hao wa Viti Maalumu walikutana kwa siku mbili kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa, Dodoma lengo likiwa ni kujadili mikakati mbalimbali ya kupambana  jimboni.
Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake, Anna Abdallah alisema wanaweka mikakati kuwawezesha kusimama wenyewe kwenye majimbo mwaka 2015 hasa baada ya kufutwa kwa Viti Maalumu katika rasimu.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAR 5.08.2013 VICHWA VIKUBWA SITTA:WABUNGE VITI MAALUMU HAWANA UMUHIMU WOWOTE,MASHEIKH WAMSHANGAA PONDA NA 9000 WAKATALIWA VYUO VIKUU NA TCU.


DSC 6296 cdb25
DSC 6297 a4a94
DSC 6298 38684
DSC 6299 d56cf
DSC 6302 13e1f
DSC 6303 a6523

DSC 6304 2d3d2
DSC 6305 e704c
DSC 6306 13b2e
DSC 6307 2b5bd
DSC 6308 3869f
DSC 6309 d5eea
DSC 6310 92a0e
DSC 6311 3cdf3
DSC 6312 bf57a
DSC 6313 be8cc

KABLA YA KODI YA LAINI ZA SIMU KUELEWEKA,SERIKALI YAANZISHA KINYEMELA KODI YA KUHAMISHA FEDHA KUTOKA BENKI...



Wakati mvutano kati ya Serikali na wadau mbalimbali kuhusu pendekezo la kufutwa kwa tozo ya kodi ya laini za simu ‘Simcard tax’ ya Sh1,000 ukiwa haujapoa, Chama cha Wenye Mabenki nchini (TBA) kimeibuka na kuitupia lawama Serikali kwa kuanzisha kinyemela sheria ya kodi ya kuhamisha fedha kutoka benki. Taarifa iliyotolewa jana na kusainiwa na Mwenyekiti wa TBA, Dk Charles Kimei imesema kuwa Serikali kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2013 (The Financial Act 2013) ilitangaza ongezeko la tozo hiyo ya kodi kwa asilimia 0.15. Kutokana na tozo hizo, gharama za kibenki kwa wateja zitaongezeka na kumlazimisha mteja aliyekuwa anatuma Sh 10 milioni kwa njia ya Mfumo wa Malipo Makubwa na ya Haraka (TISS) kwa gharama ya Sh10,000, sasa atalazimika kutumia Sh25,000 kutuma kiwango hicho cha fedha. Alipoulizwa kwa njia ya simu jana jioni kuhusu tozo hizo Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa aliomba atafutwe baadaye kwa maelezo kuwa yupo katika kikao. Hata hivyo, alipotafutwa tena simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila majibu. Tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imethibitisha kupitishwa kwa sheria hiyo, huku Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka hiyo, Richard Kayombo akilieleza gazeti hili jana kuwa walitoa barua kwa TBA tangu Julai 16, kuwataka kuanza utekelezaji wa sheria hiyo. Sheria hiyo inasema; Kutakuwa na tozo ya kodi kwa fedha zinazohamishwa kupitia benki, taasisi ya fedha au kampuni ya simu kwa tozo ya asilimia 0.15 kwa kiwango cha fedha kinachozidi shilingi 30,000… Tozo hiyo haitahusu uhamishaji wa fedha kutoka benki moja kwenda nyingine, taasisi za fedha, Serikali na shughuli za kibalozi.” TBA inasema, Serikali imeingiza tozo hiyo kinyemela kwenye sheria na kwamba haikuwemo kwenye hotuba ya bajeti ya Wizara ya Fedha mwaka 2013/2014 wala kwenye mapendekezo ya muswada wa sheria ya fedha, kwamba ilitolewa kama mabadiliko kwenye sheria. Taarifa hiyo inaeleza kuwa iwapo tozo iliyopendekezwa itatumika kama ilivyo, kutakuwa madhara makubwa katika mzunguko wa fedha kwa kuwa asilimia 12 pekee ya watu wote nchini, ndiyo wanaotumia huduma ya benki. Shirikisho hilo lilifafanua kuwa mabenki yanatumia mfumo wa kuhamisha fedha kwa njia ya simu ili kupunguza pengo lililopo baina ya watu wanaotumia benki na wasiotumia huduma hiyo. “Tozo hilo itaongeza ufisadi na changamoto nyingine za kiuendeshaji kwa kuwa zitawapa watu nafasi ya kutafuta njia ya kukwepa kodi hiyo mpya” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo. Shirikisho hilo limebainisha kuwa limeshaiandikia barua TRA na Waziri wa Fedha, kuwataka wakutane kuzungumzia suala hilo na kwamba iwapo Serikali haitaondoa tozo hiyo wananchi wajiandae kulipa kodi hiyo mpya.

DROGBA AWATUNGUA MARA MBILI ARSENAL NA KUIPA GALATASARAY KOMBE LA EMIRATES.


 Drogba amefunga mabao dakika za lala salama Kombe la Emirates l

 Drogba akimuuza Wojciech Szczesny
  Walcott akishuhudia krosi yake ikiipa Arsenal bao la kuongoza
 Walcott akishangilia na wachezaji wenzake wa Arsenal
  Emamanuel Eboue (kulia) alikuwa Nahodha wa Galatasaray ilipomenyana na timu yake ya zamani leo, Arsenal
 Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alivyokuwa baada ya kipigo

MSHAMBULIAJI Didier Drogba ameendelea kuwa mwiba kwa Arsenal akikumbushia enzi zake alipokuwa na jezi ya Chelsea, baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 leo kufunga mabao mawili na kuiwezesha klabu yake, Galatasaray kutwaa Kombe la Emirates.
Kweli, ni mashindano ya kirafiki na hayana maana yoyote katika msimu, lakini lilikuwa kama pigo lingine kwa kikosi cha Arsene Wenger.
Mfaransa huyo aliwaka ile mbaya kana kwamba mashindano hayo yana maana yoyote. Alimfokea refa wa akiba, Andre Marriner baada ya refa Jon Moss kuwazawadia penalti wapinzani dakika 12 kabla ya filimbi ya mwisho kutokana na Ignasi’s Miquel kumsukuma mshambuliaji huyo wa Ivory Coast.
Drogba alikwenda mwenyewe kupiga penalti hiyo na kumpeleka upande tofauti kipa Wojciech Szczesny na mpira alipoupiga. 
Drogba akafunga tena zikiwa zimesalia dakika nne, baada ya kupokea pasi ya Wesley Sneijder na kumuacha Per Mertesacker, kabla ya kumtungua tena Szczesny.
Arsenal ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo huo dakika ya 38, mfungaji Theo Walcott. 
Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker, Gibbs/Miquel dk69, Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Cazorla/Zelalem dk61, Walcott na Sanogo/Giroud dk61.
Galatasaray Muslera; Semih, Riera, Chedjou, Eboue, Melo/Sarioglu dk66, Engin Baytar/Gulselam dk32,Altintop/Colak, dk45, Amrabat, Elmander/Drogba dk45, Umut Bulut/Sneijder dk45.

RIHANNA AMESAINI MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA JAY Z YA "ROC NATION "


Rihanna  amesaini mkataba mpya na Kampuni ya Jay Z ya Roc Nation ambao inasemekana ni mnono kuliko mikataba yake yote iliyopita.Rihanna akiongea na kwenye simu na Mwandishi wetu moja kwa moja kutokea NY alikataa kusema ni kiasi gani atapata kwenye mkataba huo nakusema tu (trust me i love it).

        Uchunguzi wetu ulibaini kuwa Rahanna mbali na hela ambayo ni guarantee pia atakuwa anapata asilimia ya mapato yote yatakayopatikana kutokana na mauzo ya kazi zake.


 tunaendelea kuchunguza kujua je RIhanna anaingiza kiasi gani kwenye mkataba huo mpya kwani alionekana kuwa mwenye furaha sana...kwa hbari zaidi za burudani tembelea blog yetu ya burudani yaDMK411.BLOGSPOT.COM