Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 10, 2013

ANGALIA PICHA:AJALI MBAYA YATOKEA KABUKU TANGA


 
 

A FIRST TANZANIAN JUDGE SWORN IN AS INTERNATIONAL RESERVE JUDGE IN CAMBODIA

IMG_9765Judge Steven Bwana (centre) from Tanzania accompanied by his wife Angelika Bwana in Official tete-atete through video conference with a Panelist of Judges in Cambodia. Looking on is WFP Representative and Country Director, Mr Richard Ragan, who was acting as the UN Resident Coordinator during the Sworn in Ceremony held at WFP Headquarters in Dar es Salaam.( Photos by Zainul Mzige of Dewji Blog).
IMG_9779Above and Below is Judge Steven Bwana Officially Sworn in as International Reserve Judge in Extraordinary Chambers in the Courts of Cambodia (ECCC) through video conference today in Dar es Salaam.
IMG_9785
IMG_9760Panelist of Judges from ECCC following up the Official Sworn in of the Judge Steven Bwana through video conference.
IMG_9792Judge Steven Bwana signs the official document of the Extraordinary Chambers in the Courts of Cambodia (ECCC) after Sworn in.
IMG_9803WFP Representative and Country Director, Mr Richard Ragan, who was acting as UN Resident Coordinator signs the official document of ECCC.
IMG_9812Feeling proud to the First Tanzanian Judge to be appointed as an International Reserve Judge in ECCC.
IMG_9832Judge Steven Bwana answering questions to reporters not in pictures.
IMG_9810A group section of reporters from various media houses listens attentively the Sworn in ceremony of the Judge Steven Bwana.
By Moblog Team
Today a Tanzanian Judge Steven Bwana sworn in as an internal reserve judge in the Pre-Trial Chamber of the Extraordinary Chambers in the Courts of Cambodia (ECCC) Via video link between Phnom Penh and Dar es Salaam.
Judge Bwana gave the following oath to Mr. Knut Rosandhaug, the Coordinator for United Nations Assistance to the Khmer Rouge Trials:
“I solemnly declare that I will perform my duties and exercise my powers as a judge of the Extraordinary Chambers in the Courts of Cambodia for the Prosecution of Crimes Committed During the Period of Democratic Kampuchea honourably, faithfully, impartially and conscientiously and that I will not seek or accept instructions in regard to the performance of those duties or the exercise of those powers from any Government or from any other source,”
Following the nomination by the United Nations Secretary General Ban Ki-mooon, and the approval by the Supreme Council of the Magistracy, His Majesty King NorodomSihamoni in 2012 appointed Judge Bwana as new international reserve judge to serve in the ECCC Pre-Trial Chamber.
Judge Bwana took the oath today as he has been called upon the Pre-Trial Chamber to participate in the deliberation of a motion pending before the chamber.
The ECCC is a special Cambodian court which receives international assistance, through the United Nations Assistance to the Khmer Rouge Trials.
Under the terms of Agreement between the United Nations and the Royal Government of Cambodia, the Extraordinary Chambers will bring to trial senior leaders of Democratic Kampuchea and those who were most responsible for the crimes and serious violations of Cambodia penal law, international humanitarian law and custom and international conventions recognized by Cambodia, that were committed during the period from 17 April 1975 to 6 January 1979.
Speaking to reporters in a brief news conference, after he sworn in Judge Bwana said that is working station will be in Dar es Salaam and Cambodia but it will depend on the kinds of cases from time to time.
He said that in order to protect the African continent and the good moral leaders the region should not try to withdrawal its membership to the International Criminal Court (ICC), The Hague for the purpose of protecting human rights and enhance good governance and democracy.
“I think leaders of 54 African countries should reject the move that initiate the continent to withdrawal its membership to the IC,” he said.
Judge Bwana underscored that if the African countries will withdrawal its membership to ICC it will hinder the struggle in building strong democracy, good governance and the respect to human rights convention.

MABALOZI WA JUMUIYA YA NCHI ZA ULAYA (EU) WATEMBELEA GEREZA KUU UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM

image Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akisalimiana na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Gilberto Sebregondi ambaye aliongoza ujumbe wa Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya katika ziara yao leo Oktoba 10, 2013 Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam ili kujionea namna ambavyo Jeshi la Magereza linazingatia kikamilifu masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Uendeshaji wa Magereza hapa nchini.image (1) Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) akisoma hotuba yake fupi mbele ya Balozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Filiberto Sebregondi(aliyeketi mbele) pamoja na Mabalozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya wanaoonekana katika picha kabla ya kutembelea sehemu mbalimbali za Gereza Kuu Ukonga leo Jijini Dar es Salaam.
image (3) Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya wakiwasilikiza kwa makini Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam waliohukumiwa Adhabu ya Kunyongwa(hawapo pichani) ambapo wameiomba Jumuiya ya Ulaya kuendelea kupaza sauti na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili Adhabu hiyo hapa Nchini Tanzania iweze kuondelewa(wa pili kulia) ni Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Mhe. Dianna Melrose.image (2) Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( wa tatu kushoto mstari wa pili) akiongozana na Mabalozi mbalimbali wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya kuelekea sehemu ya Zahanati ya ndani inayohudumia Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam waliopotembelea leo Oktoba 10, 2013.image (4)Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za Gereza Kuu Ukonga leo Jijini Dar es Salaam(wa tatu kushoto) ni Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Filiberto Sebregondi ambaye aliongoza Ujumbe wa Mabalozi hao(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA:::AUAWA BAADA YA KUMUUA MWENZAKE KWA MKUMCHOMA NA KISU MKOANI MWANZA



Huyu ndiye marehemu kijana maarufu kwa jina la 'Mkandarasi' anayesadikika kufanya mauaji kwa mumchoma kijana mwenzake kisu naye aliuawa na wananchi wenye hasira katika mtaa wa Msikiti wa Ijumaa jijini Mwanza.



Maafisa polisi na wananchi wakiwa wameuzingira mwili wa marehemu Mkandarasi. 

Umati wa watu mtaa wa Msikiti wa Ijumaa. 
Mashuhuda wakiutizama mwili wa kijana aliyeuwa kwa kuchomwa kisu. 
Mwili wa kijana aliyekuwa akifanya kazi kwa mamalishe mtaa wa Msikiti wa Ijumaa ukiwa umelowa damu mara baada ya kuchomwa kisu kufuatia majibizano na jamaa (maarufu kwa jina la 'Mkandarasi') ambaye naye aliuawa na wananchi wenye hasira waliojichukulia sheria mkononi. 
Mashuhuda. 
Polisi walifika eneo la tukio na kisha wakaondoka na miili ya marehemu hao nao wengine wakibakia eneo la tukio kubaini nini chanzo. 
Mwananchi akifukia damu zilizotapakaa kwenye barabara.
Watu wawili wameuawa katika tukio la utata lililotokea jana asubuhi majira ya saa 3 na dakika kadhaa, katika eneo la barabara ya msikiti wa Ijumaa jijini Mwanza. 

Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa kilisababishwa na kijana mmoja maarufu kwa jina la Mkandarasi kumchoma kisu kijana mwenzake ambaye alikuwa mgeni akifanya kazi za usaidizi kwa mamantilie wanaopika chakula katika moja ya viunga vya ndani eneo la vichochoro vya mtaa wa Msikiti wa Ijumaa kufuatia majibizano ambayo yalisababisha kijana Maarufu kwa jina la 'Mkandarasi' amchome mwenzake kisu cha shingoni na sehemu nyingine za mwili. 
Kijana huyo alipoona amezidiwa alitafuta upenyo na kukimbia huku damu zikimchirizika, hata hivyo hakufika mbali kwani alizidiwa na hatua chache baadaye alianguka chini nakuaga dunia. 
Wananchi wenye hasira walimzingira muuaji ambaye naye alikuwa akijihami kwa kisu alichokuwa nacho mkononi na ndipo walipofanikiwa kumbwaga chini na kumshambulia kwa mawe hadi umauti. 
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linataraji kuja na taarifa kamili ya Uchunguzi wake hii leo. 


STEPHEN WASIRA "SINA UFUNGUO WA IKULU, SIWEZI MCHAGULIA RAIS NANI WA KUONANA NAYE"


 
 

WAJUMBE WA TUME YA KATIBA WAENDELEA NA UCHAMBUZI WA MAONI YA WANANCHI KUHUSU RASIMU YA KATIBA MPYA YALIYOTOLEWA KATIKA MABARAZA YA KATIBA


 
 

TAZARA YAPATA VICHWA SITA VYA TRENI,


DIGITAL CAMERAMadereva na Mafundi wa Treni za TAZARA wakiwa katika moja ya vichwa sita vipya vya Treni ambavyo vimeletwa Tanzania na wapo katika mafunzo ya jinsi ya kuvitumia. (Picha na Furaha Eliab, Mbeya) 
Na Furaha Eliab, Mbeya
SHIRIKA la reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) limepata vichwa sita vya Treni vipya kutoka nchini China vyenye uwezo wa kubeba tani 1800 kila kimoja.
Kufuatia kutolewa kwa vichwa hivyo vya Treni vipya,  madereva 160 na mafundi 80 wa karakana ya Treni Iyunga mkoani Mbeya wanapatiwa mafunzo yakakayo wawezesha kufanya kazi kwa umakini katika vichwa hivyo.
Akitoa maelezo ya ujio wa vyicho hivyo Mhandisi Mwandamizi katika karakana na Iyunga Eng. Davie Tembo alisema kuwa vichwa hivyo vya treni vyenye uwezzo wa kubeba Tani 1800 vimeletwa Juzi katika karakana hiyo.
Alisema kuwa vimetoka nchini china na ni toleo jipya ambalo linahitaji madereva na mafundi kujifunza kabla ya kuanza kutumia kwani linatumia mfumo mpya.

Tembo alisema kuwa kampuni ya CSR Qishuyan ya nchini China ndio iliyo tengeneza vichwa hivyo na inatoa mafunzo kwa madereva na mafundi jinsi ya kuvimudu vichwa hivyo.
Alisema kuwa wamevijaribu vichwa hivyo na kuviona vinafaa kwa matumizi na havina shida yoyote.
Awali akifungua mafunzo kwa madereva hao Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA,  Said Sauko alisema kuwa mafunzo hayo yatalenga kwa Wafanyakazi wa TAZARA watakao kuwa katika makundi saba ambapo kila kundi litakuwa na watu wasio pungua 40.
Alisema kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa muda wa mwezi mmoja na yamelenga kwa wafanyakazi kutoka Tanzania na Zambia.

PENNY AFUNGUKA....ASEMA NI UONGO NA UZUSHI KWAMBA KAKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUONA PICHA ZA DIAMOND NA WEMA ISHU NZIMA HII HAPA


Girl Friend wa msanii wa bongo fleva 'Diamond' leo jioni amenitumia text kunifahamisha kuwa ' Alikuwa Kazini Siku Nzima Na Kuwa Hajapata Tatizo Lolote Leo Kuhusu Afya Yake. Taarifa Zilizo Sambaa Kuwa Alizimia Na Kupelekwa Hospitalini Sio Za Kweli Kabisa. 

Viongozi watoa wito kwa Wakenya kuondoa uchochezi wa mapigano ya kidini


Viongozi wa kisiasa na kidini nchini Kenya wanatoa wito kwa pande zote kuondoa hasira za kidini ambazo ni za ukatili mkubwa kufuatia shambulio la al-Shabaab kwenye kituo cha biashara cha Westgate huko Nairobi mwezi uliopita na kuuawa kwa maulamaa wanne wa Kiislamu huko Mombasa wiki iliyopita.
  • Askari polisi akijibu moto kwenye kanisa la Jeshi la Wokovu huko  Mombasa, lililopangwa na kutekelezwa na wapingaji Ijumaa (tarehe 4 Oktoba). [Rajab Ramah/Sabahi] Askari polisi akijibu moto kwenye kanisa la Jeshi la Wokovu huko Mombasa, lililopangwa na kutekelezwa na wapingaji Ijumaa (tarehe 4 Oktoba). [Rajab Ramah/Sabahi]
  • Polisi wakiwatawanya wapingaji huko Mombasa huku magurudumu yakichomwa na kutoa moshi mweusi. [Rajab Ramah/Sabahi] Polisi wakiwatawanya wapingaji huko Mombasa huku magurudumu yakichomwa na kutoa moshi mweusi. [Rajab Ramah/Sabahi]
  • Polisi waliwakamata baadhi ya wapingaji, wengi wao wakiwa ni vijana, katika kuchukua hatua kali za kinidhamu katika jiji lote. Vijana wanne walifariki dunia katika mapambano na polisi. [Rajab Ramah/Sabahi] Polisi waliwakamata baadhi ya wapingaji, wengi wao wakiwa ni vijana, katika kuchukua hatua kali za kinidhamu katika jiji lote. Vijana wanne walifariki dunia katika mapambano na polisi. [Rajab Ramah/Sabahi]
Ghasia zilianza Ijumaa iliyopita (tarehe 4 Oktoba) huko Mombasa baada ya watu wenye silaha ambao hawajajulikana kumuua Sheikh Ibrahim Ismail na watu watatu aliokuwa nao kwa kupigwa risasi wakati akiendesha gari Alhamisi jioni.
Ismail alionekana kwa sehemu kubwa kama mrithi wa muhubiri matata Aboud Rogo Mohammed. Watu wote wawili walikuwa na mfungamano wa karibu na Msikiti wa jiji hilo wa Masjid Musa.
Wapingaji walianza machafuko katika kanisa la Jeshi la Wokovu la jiji hilo, na vijana wanne waliuawa katika kukabiliana na polisi.
Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Haki za Binadamu la Kiislamu al-Amin Kimathi aliwalaumu polisi kwa mauaji ya Ismail na kwa kushindwa kuhimili vurugu zilizofuatia baadaye.
"Polisi wanatumia faida ya mihemko ya wananchi iliyopo iliyochochewa na shambulio la kigaidi la Westgate," Kimathi aliiambia Sabahi, akitahadharisha kwamba kama "mauaji nje ya mahakama " hayatakomeshwa yatarudisha nyuma vita dhidi ya ugaidi.
"Shambulio hilo ni kinyume na aina zote za sheria katika ardhi hii na kinyume na kanuni zote za haki za binadamu," alisema. "Bila kujali kiasi cha uhalifu kilichofanywa na mtu, tuna taasisi zinazofanya kazi. Waache watuhumiwa wa jambo lolote kupelekwa mbele ya sheria."
Mkuu wa Polisi wa kaunti ya Mombasa Robert Kitur alikana kwamba polisi walihusika na chochote katika kufyatua risasi.
"Hatukuhusika kabisa na mauaji hayo. Hivyo sivyo tunavyofanya kazi. [sheria ya polisi] ni kuwakamata washukiwa wowote na kuwafikisha mbele ya mahakama zetu, sio kuwaua," Kitur aliiambia Sabahi.
Kitur alisema polisi walikuwa wanachunguza mauaji na wameimarisha ulinzi ili kuzuia kutokea tena kwa fujo siku zijazo, na kwamba hali ya kawaida imerejea Mombasa.

Viongozi wa Kiislamu walaani vurugu, kuchomwa kwa kanisa

Wawakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu la Kenya (SUPKEM), Kamati ya Msikiti wa Jamia, Majlis Ulamaa Kenya, Baraza la Maimamu la Kenya na Ulamaa, na Jukwaa la Waislamu la Haki za Binadamu wameshutumu mauaji ya muhubiri wa dini, pamoja na uchomaji wa kanisa.
Katibu Mkuu wa SUPKEM Adan Wachu aliiambia Sabahi kwamba mauaji yalilenga kutisha na kudhoofisha hali ya usalama nchini Kenya ambayo inahitaji kushughulikiwa haraka ili kuhakikisha kwamba sheria na utulivu vinatawala.
"Ingawa tunarudia kutoa shutuma zetu za mauaji ya watu wengi ya Westgate, pia tunashtushwa na vurugu ambazo zilijitokeza katika matokeo ya mauaji yasiyoidhinishwa ya wahubiri wanne wa kiislamu siku ya Alhamisi, mashambulizi yasiyo na sababu katika kanisa na mali binafsi huko Mombasa baada ya swala ya Ijumaa," Wachu alisema.
Shambulizi la Westgate na mauaji huko Mombasa yanalenga kuchochea uhasama baina ya dini nchini, alisema.
"Tunatoa wito kwa wapenda amani wote wa Kenya kutokubali kuangukia katika mitego ya mambo hayo ya wahalifu wanaolenga katika kuchochea chuki baina ya Wakenya," Wachu alisema.
"Wale wanaohusika na uchomaji wa kanisa la Jeshi la Wokovu ni wahalifu ambao hawaiheshimu dini," alisema." Uislamu hauruhusu tabia kama hiyo ya kuchukiza na hata katika nyakati za migogoro, maadili ya Kiislamu yako wazi kwamba nyumba za ibada na wanaozitumia hazipaswi kushambuliwa au kuharibiwa kwa namna yoyote."
Seneta wa chama cha National Alliance Emma Mbura, anayewakilisha Kaunti ya Mombasa, alitoa wito kwa mashirika ya ulinzi kuboresha mbinu za kipolisi kutotegemea mauaji ya nje ya mahakama, ambayo alisema yanaweza kuongeza mvutano baina ya dini.
"Kila mmoja anapaswa kuchukuliwa hana makosa hadi hapo atakapothibitika kuwa na kosa, kwa kuwa kuua hakuwapi watuhumiwa siku zao katika mahakama," aliiambia Sabahi. "Kinachofuata ni kwamba watu wasio na hatia wanaweza kuwa waathirika, na wale wanaoachiwa wakawa na hasira na wanaweza wakaingia katika kulipiza kisasi."
Mbura alionya kwamba mauaji kama hayo yanaweza kusababisha vijana kuwaunga mkono al-Shabaab na hata kuwashawishi kujiunga na wanamgambo, lakini kuwapeleka watuhumiwa wa ugaidi mahakamani kunauruhusu umma kutambua makosa ya wanaotuhumiwa.

Kubatilisha agizo la polisi la 'kupiga risasi na kuua'

Wakati huo, baadhi ya waangalizi wanamuomba Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo kubatilisha maagizo ya upigaji risasi na kuua aliyoyatoa mwezi Septemba, akisema kwamba mashirika ya usalama yamesikiliza maelekezo kwa kutumia nguvu ya ziada.
"Inapotokea maisha ya ofisa au mtu mwingine yanakuwa hatarini, polisi lazima watumie risasi za moto kwa ufanisi. Na hili ni agizo kwa maofisa polisi wote nchini Kenya," Kimaiyo alisema tarehe 13 Septemba wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya huduma za polisi na serikali ya Kaunti ya Mombasa.
Alisema hilo agizo lilikusudia "kushughulikia kikamilifu wahalifu ambao pia wanahatarisha maisha ya wengine".
Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar Hassan alisema mauaji ya maulamaa hao yaliyotokea wiki iliyopita huko Mombasa yalikuwa ni matokeo ya maelekezo ya Kimaiyo.
"Agizo hilo, ambalo bado linafuatwa hata baada ya tukio la Westgate linahatarisha usalama wa pamoja wa baadhi ya jamii," alisema, akiongeza kwamba Kimaiyo anapaswa kuzingatia tena agizo hilo katika kipindi hiki kibaya.
"Kama polisi wanaweza kusikiliza agizo la kiongozi wao la 'kupiga risasi na kuua', kimsingi wanaweza kusikiliza agizo la kiongozi wao la kukamata na kushtaki. Wana uwezo huo," aliiambia Sabahi.
Maagizo ya Kimaiyo yanakwenda kinyume na katiba ya nchi, kwa sababu sheria inawaruhusu maofisa polisi tu kupiga risasi kwa kujilinda, kwa mujibu wa Mratibu Mtendaji wa Kituo cha Kuhamasisha na Kulinda Haki Odhiambo Oyoko.
Hata hapo, polisi wanatarajiwa kupiga risasi na kulemaza, alisema, akiongeza kwamba agizo lililorekebishwa litafungua ukurasa mpya wa "mauaji rasmi ya kutumia nguvu".
Agizo linaonyesha kutokuwa na msimamo kwa jeshi la polisi kufanya mauaji, alisema Simiyu Werunga, kapteni mstaafu wa Jeshi la Kenya ambaye pia ni mkurugenzi wa Kituo cha Afrika cha Usalama na Mafunzo ya Kimkakati huko Nairobi.
"Kuna mengi katika ufanisi wa sera kuliko kuwaua tu washukiwa," alisema. "Serikali inapaswa kufanya utekelezaji sasa wa mabadiliko mengi ya polisi, ambalo pia linahitaji mabadiliko ya mtaala wa mafunzo katika vyuo vya mafunzo ya polisi."
Serikali inapaswa kuimarisha mikusanyiko ya kiintelijensia na mafunzo ya polisi, alisema, na maofisa wanapaswa kupewa motisha kwa malipo mazuri, vifaa vinavyofaa na kutambua mafanikio yao.
Maelekezo ya Kimaiyo yalizuia kushindwa kwa polisi kuandaa kesi ambazo zinaweza kushtakiwa, kwa mujibu wa Moses Omusula, mtaalamu wa usalama anayeishi Nairobi.
"Polisi wanaficha aibu zao kwa kushindwa kutoa ushahidi wa kuwatia hatiani kuwezesha mashtaka ya mahakama," Omusula aliiambia Sabahi. "Kuficah kuonekana kutokuwa na ufanisi kwao, wanaamua kuwaua washukiwa."
"Maagizo kama hayo kabla yameshindwa katika kushughulikia vurugu," Omusula alisema. "Maofisa polisi wazembe watakuwa wakitekeleza agizo na badala yake watapiga risasi badala ya kuwakamata na kutoa ushahidi kwa washtakiwa."

Kimaiyo: 'Wahalifu hawakutuachia chaguzi nyengine'

Lakini Katibu wa Baraza la Mawaziri Joseph ole Lenku aliunga mkono maelekezo ya Kimaiyo na kusema kwamba polisi watafuata sheria.
"Hakuna kitu kama mauaji nje ya mahakama," alisema mwezi Septemba wakati inspekta wa polisi alipotangazo agizo hilo. "Tuna wajibu wa kuilinda nchi. Polisi hawatakamata maguruneti kwa mikono yao na kuwapeleka gerezani kwa kisingizio cha kuzuia mauaji nje ya mahakama. Tutahakikisha kuwa wahalifu wenye silaha wanashughulikiwa kama wahalifu wenye silaha."
Kimaiyo pia alitetea maelekezo yake kwa kuonesha ongezeko la vurugu taifa zima kutoka kwa magengi ya wahalifu waliojipanga, wanamgambo wa kikabila na vikundi vya kigaidi.
"Amr hiyo haina uhusiano hata kidogo na mashtaka kwa sababu tunaheshimu mahakama, kwa sababu inatoa haki pale inapohitajika," aliiambia Sabahi.
"Tumekuwa tukiwashughulikia wahalifu kwa glavu za kitoto kwa muda mrefu," Kimaiyo alisema. "Tumefikiria chaguo za aina zote, ikiwa ni pamoja na kutoa msamaha kwa wahalifu, magaidi na wanamgambo wa kikabila ili waachane na vurugu, lakini ni machache sana yametiliwa maanani."
"NI uchaguzi mgumu lakini wahalifu hawakutuachia chaguzi nyengine," alisema.chanzo Sabahi online.

KESI YA KUPINGA TOZO YA KADI YA SIMU YA SH1,000 KWA KILA LINI KUSIKILIZWA OKTOBA 21 MWAKA HUU KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KANDA YA DAR ES SALAAM.


MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imekubali kampuni za simu nchini kujiunga pamoja na Chama cha Kutetea Walaji kwenye kesi ya kupinga tozo ya kadi ya simu ya Sh. 1,000 kwa kila laini na mtumiaji kwa kila mwezi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara ya Fedha baada ya kutupilia mbali pingamizi la awali la upande wa walalamikiwa. 
 
Uamuzi huo ulitolewa jana na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Mwenyekiti, Jaji  Aloysius Mujuluzi, akisaidiana na Lawrence Kaduri na Salvatory Bongole.

Jaji Mujuluzi alisema baada ya kupitia hoja zilizotolewa na pande zote mbili kuhusu pingamizi hilo, mahakama imeona upande wa walalamikiwa hauna sababu za msingi za kupinga kampuni za simu kujiunga kwenye kesi hiyo na kwamba inazitupilia mbali.

Aidha, baada ya uamuzi huo mahakama iliziamuru pande zote mbili kubadilishana nyaraka za majibishano ya kisheria kwa njia ya maandishi na kesi ya msingi itasikilizwa Oktoba 21, mwaka. 
Kampuni zilizojiunga kwenye kesi hiyo ni, Vodacom, Airtel, Mic Tanzania Ltd, TTCL na Zantel Tanzania. 
 
Jumatatu iliyopita, upande wa walalamikiwa ukiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, akisaidiana na Wakili wa Serikali Mkuu, Edson Mweyunge, Alisia Mbuya na Sara Mwaipopo, walipinga ombi la mawakili wa kampuni za simu la kutaka kujiunga kwenye kesi hiyo kwa kuwa hati ya kiapo ilikosewa kisheria.
Mweyunge alidai kuwa hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani  imeonyesha kutolewa na Tumaini Shija ambaye anawawakilisha walalamikiwa wengine zikiwamo makampuni za simu.
Hata hivyo, wakili wa kampuni  za simu, Fatuma Karume, alidai kuwa pingamizi la jamhuri halina sababu za msingi kwa sababu siyo kila mlalamikaji anatakiwa kuwasilisha kiapo chake  katika kesi moja kwamba mahakama itupilie mbali pingamizi la jamhuri halina msingi kisheria.
Katika kesi ya msingi Chama cha Kutetea Walaji kimewaburuza mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara ya Fedha kikitaka wapewe amri ya kusimamisha tozo ya kadi ya simu ya Sh. 1,000 kwa kila laini kwa watumiaji wa simu kila mwezi, baada ya kupitishwa na Bunge miezi michache iliyopita.
CHANZO: NIPASHE

Wenzetu Wanapoona Fursa za Kukua Watanzania Tunaona Matatizo -Ali Mfuruki

 
Mmoja wa wafanyabiashara wakubwa nchini na Milionea, Ali Mfuruki alipata nafasi ya kuongea katika kipindi cha Makutano na Fina Mango na kuzungumzia hofu waliyonayo Watanzania dhidi ya nchi wanachama wajumuiya ya Afrika Mashariki. Mfuruki ambaye amewekeza katika biashara mbalimbali kwenye nchi hizo alikosoa uoga wa Watanzania na kusema Tanzania inatakiwa kufungua milango kwa wawekezaji kwani fedha zinazopatikana zinaingia katika mzunguko wa uchumi na kusisitiza kuwekeza katika kuwanoa wataalam wa ndani badala ya kuogopa kupoteza ajira kwa wageni. Bofya kusikiliza zaidi http://www.youtube.com/watch?v=d6oPn1uG5eI

Polisi wamnasa jambazi anayejiita ‘Rais wa Nyololo’

 
JESHI la Polisi mkoani Iringa limemtia mbaroni mkazi wa Nyololo Wilaya ya Mufindi, Gwelino Mtonyole maarufu kama ‘Rais wa Nyololo’ kwa tuhuma za kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha na utekaji wa lori la mafuta.
Mtonyole anatuhumiwa kushiriki kuliteka lori aina ya Scania lililokuwa likisafirisha mafuta aina ya dizeli kutoka Dar es Salaam kwenda Ndola, Zambia mali ya kampuni ya E. Awadh. Co. Ltd.
Mtuhumiwa huyo na wenzake waliliteka gari hilo baada ya dereva kuteremka kwa lengo la kuangalia hitilafu zilizokuwa zikijitokeza na kusababisha kufuka moshi katika injini.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo maeneo ya Igumbilo, Septemba mwaka huu katika barabara ya Iringa - Dar es Salaam.
Alisema kuwa watu wanane walimvamia dereva na utingo wake na kisha kumfunga kamba miguuni, kitambaa usoni na kumweka vitambaa mdomoni kisha kumtelekeza katika pagale.
Mungi alisema harakati za kumsaka kiongozi huyo wa shughuli za utekaji wa magari mkoani Iringa, zilifanikiwa baada ya gari hilo kukutwa likiwa limetelekezwa Makambako huku mapipa 15 ya mafuta aina ya dizeli yakikutwa nyumbani kwake.
Mungi alisema Jeshi la Polisi linawasaka watu saba wanaodhaniwa kuwamo katika mtandao huo ili kudhibiti tabia za utekaji wa magari na kwamba tukio hilo ni la pili kutokea katika kipindi cha mwezi mmoja.
Alisema kuwa dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 945 CAS na tela lake lenye namba T 215 CFQ alijulikana kwa jina la Hassan Mapili (38).
Kamanda alifafanua kuwa mtuhumiwa huyo wakati anakamatwa nyumbani kwake Nyololo, alikutwa na zaidi ya lita 4,000 za mafuta ya dizeli zikiwa zimehifadhiwa katika madumu makubwa.
Alisema lori hilo hadi linapatikana Makambako, mkoani Njombe lilikuwa limebakia na lita 6,000 kati ya 36,000 za mafuta yaliyokuwa yamebebwa.
Chanzo: Tanzania Daima

Polisi DSM yathibitisha kuokolewa kwa wavuvi 11 Nyakatome


 Jeshi la Polisi Kanda maalum ya DSM limethibitisha kuokolewa kwa wavuvi wote 11 ambao Jahazi lao liliwaka moto asubuhi ya leo katika eneo la Nyakatome

ZIARA YA ZITTO KABWE KANDA YA MAGHARIBI,JIMBO LA IGALULA






Siku ya 5 ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetufikisha Jimbo la Igalula, wilaya ya Uyui. Tumekutana na wananchi katika vijiji vya Goweko, Loya, Miswaki, Miyenze na Kigwa.

Tumezungumza kuhusu changamoto ya usafiri wa Reli, wafugaji kunyanyaswa na watendaji wa kata na askari kwa kunyanganywa mifugo, zao la Tumbaku, maji safi na salama na suala la jumla la Katiba na mchakato wa kuandika katiba.

Kimsingi shughuli za kiuchumi za wananchi ni kubwa na hasa Kilimo na mifugo. Hata hivyo ukosefu wa miundombinu unafanya wananchi wasipate thamani ya mazao yao na jasho la kazi zao.

Nilipofika Kijiji cha Loya nimeona eneo kubwa lina miti ya mihama. Wananchi wanatumia tu mihama wakati wa njaa na mara nyingi matunda haya yanaharibika tu. Lazima matunda haya yana matumizi yake ya kiviwanda maana ‘kernel’ yake ina mafuta.
Na hili ni swali aliloacha Mh Zitto Kabwe
Nani anajua matumizi ya Mihama?


BOTI YAUNGUA MOTO NDANI YA BAHARI YA HINDI


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjeuJYA99Ck0zr3WPTGf4KpqoQTCovvhkOjUb6aFCF6hSAqtaxvcCfBjcxp0ZRj3Hxmcm34eveYGecCHjT-NBOYmvuccI5jAsjn8LyyY-a8Z6nc5Zxcqf_VFDOdDrcaEQhUnI7FJFcOMsI/s400/meliBoti moja iliyobeba mizingo kuelekea Zanzibar inawaka moto hivi sasa katika bahari ya hindi nje kidogo ya bandari habari kutoka Breking news ya Radio one leo asubuhi boti hiyo ni ile inayobeba mizigo ya wafanyabiashara jeshi la polisi pamoja na vifaa kadhaa vimelekea vkatika tukio ili kuwahi kuzima moto tutawaletea zaidi

MH. JANUARY MAKAMBA AIPA SHAVU SKYLIGHT BAND