Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 14, 2015

Nay wa Mitego kufanya collaboration na msanii wa Nigeria Wizkid!

Nay wa Mitego amedai kuwa kwenye harakati za kufanya collabo na masupastaa wa Nigeria, Wizkid au D’Banj Akizungumza kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, Nay alisema tayari ameshafanya mazungumzo na uongozi wake pamoja na yeye mwenyewe Wizkid.

“Tupo kwenye process ambazo zinaelekea mwishoni,” alisema. “Unajua yule ni mtu ambaye ana menejimenti lakini this time tupo kwenye hatua fulani za kuanza kufanya kazi. Unajua mtu kama yule unapomtoka kufanya kazi kuna vitu anahitaji kuona ili ajue wewe ni mkubwa kiasi gani,” aliongeza.“Pia kuna baadhi ya gharama zinakuwepo lakini kiukweli pia wenyewe wanashtuka baada ya kuona umaarufu wako ndani ya nchi. Nilianza kuwasiliana naye kwa njia ya email kama ninavyofanya kwa wasanii wengine ingawa mwanzo alikuwa mgumu lakini alivyokaa na menejimenti yake alielewa nini nataka kufanya.”..

No comments:

Post a Comment