Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 15, 2015

CCM WANAENDELEA KUPIGA KUSHOTO NA KULIA,MWIGULU NDANI YA KAHAMA ,USHETU NA MSALALA

"Nenda kamwambie Magufuli,Msalala na Shinyanga yote kura ni zake,Tunahitaji maendeleo ya huduma za jamii sio vyama vya siasa"."Wanamsalala,Nawaombeni mmpigie kura Magufuli,Huyu ndiye mgombea pekee ambaye anajua shida za Watanzania wote,katika Utumishi wake wa serikali kwa miaka 20 ameweka alama kwa kila Mkoa kwa kujenga barabara zilizofungua Uchumi wetu.Hivyo mpatieni ridhaa aweze kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi na alete mabadiliko ya kweli kwa Watanzania" Nchemba.

 
Mwigulu Nchemba akiwaaga wananchi wa Msalala mara baada ya mkutano wa hadhara.Muitikio wa Wanaushetu walipoulizwa watakompigia kura Dr.J.Pombe Magufuli.
Mwigulu Nchemba ameendelea kusisitiza kuwa wananchi wajitokeze kupiga kura kwa wingi,Wakishapiga kura warejee makwao kwasababu hakuna atakayeruhusiwa kusubiria matokeo kituoni wakati wote wa zoezi la upigaji kura.Wana
ushetu"Si kwamba tunawachukia UKAWA,Lakini kwa ukweli ulio wazi Uchaguzi huu WANAUKAWA wamechanga karata vibaya,Watanzania wameshituka kama mtu aliyeitwa Fisadi na Mwizi kwa miaka 15,ghafla kwa siku moja akawa msafi na kuitwa Kamanda,Hii ni wazi Viongozi wa UKAWA wamekula DILI ilikumpatia nafasi ya kugombea Urais huyo mgombea wao"Mwigulu NchembaKura ya Mabadiliko ya kweli ni kwa Magufuli,Hakikisha unapopiga kura TIKI yako haitoki nje yakisanduku ilikuzuia uharibifu wa kura.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Kahama Jioni ya leo.Nchemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Kahama Mjini Ndg.Kishimba."CCM imewaletea Magufuli kwa Malengo,Hakikisheni mnachagua kwa Malengo,Magufuli anakwenda kubadilisha hali ya Utendaji serikalini,Magufuli anakwenda kupambana na mafisadi na walarushwa hapa Nchini,Nendeni mkamchague Magufuli kwaajili ya KAZI TU"Wanakahama wakishangilia na Kuunga Mkono kumpigia kura Dr.J.Pombe Magufuli kwenye Uchaguzi wa mwaka huu.Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Kahama Mjini mara baada ya mkutano wake wa hadhara wa kampeni wa kuomba kura za Chama cha Mapinduzi.

Picha na Sanga Festo Jr.

No comments:

Post a Comment