Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, October 30, 2015

FIFA yatoa majina ya vigogo saba wanaowania Urais

Pin It
Shirikisho la kandanda duniani, FIFA limetangaza majina ya viongozi saba watakaowania urais.
151029004813_fifa_kinyanganyiro_640x360_bbc_nocredit
Majina hayo ni pamoja na Prince Ali bin al-Hussein, mwenye miaka 39 ambaye ni rais wa shirikisho la kandanda la Jordan. Mwingine ni Musa Bility raia wa Liberia mwenye umri wa miaka 48 akiwa ni rais wa shirikisho la soka nchini humo.
Yupo pia mtendaji mkuu wa zamani wa FIFA, Jerome Champagne, mwenye umri wa miaka 57, raia wa Ufaransa. Katika kinyang’anyiro hicho yupo pia katibu mkuu wa UEFA, Gianni Infantino, raia wa Italia mwenye umri wa miaka 45.
Rais wa shirikisho la kandanda la Asia Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, naye yupo kwenye mchuano huo akiwa na umri wa miaka 49.

 
Mwingine ni waziri wa zamani wa Afrika Kusini Tokyo Sexwale, mwenye umri wa miaka 62.
Wa mwisho ni Michel Platini rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) aliyesimamishwa kwa tuhuma za rushwa akipewa nafasi ya kugombea kiti hicho ikiwa adhabu yake ya kufungiwa itaisha kabla ya muda wa uchaguzi.
Uchaguzi mkuu wa FIFA unatarajiwa kufanyika Februari 26 mwakani.
CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment