Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, October 24, 2015

Mambo Yatakayosababisha Kura Yako Iwe "Imeharibika" au "Sahihi"


Kura halali zitakazopigwa siku ya Jumapili kwa ajili ya kuwachagua viongozi kwenye Uchaguzi Mkuu zinaweza kuharibika ikiwa hazitapigwa kwa usahihi na kuondoa utata..

Kura iliyoharibika ni ile ambayo:
  1. Haina alama yoyote
  2. Imepigwa kwa wagombea zaidi ya mmoja
  3. Imeandikwa jina la mpiga kura
  4. Alama imewekwa nje ya kisanduku cha picha ya mgombea
  5. Haina muhuri wenye alama rasmi
Kura sahihi;
  1. Yenye alama ya ‘v’ kwenye kisanduku
  2. Yenye alama yoyote kwenye kisanduku/picha/ jina la mgombea


Utata
  • Kutakuwa na utata endapo utaweka alama iliyopitiliza kisanduku cha mgombea mmoja na kufika kwa mwingine. Epuka kuharibu kura. Kura yako, mustakabali wako

No comments:

Post a Comment