Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 15, 2015

MWILI WA MAREHEMU KIGODA WAWASILI NCHINI KUAGWA LEO

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli naye yupo kuungana na Watanzania wengine kuupokea mwili wa Kigoda. Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akijumuika na Watanzania wengine kuupokea mwili wa marehemu Kigoda.
Ndugu, Jamaa na marafiki wakiusubiri kuupokea mwili wa Kigoda.….Hudhuni ikitawala.

 
Ndugu, Jamaa na marafiki wakiusubiri kuupokea mwili.Hali ya majonzi ikitawala eneo loa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere Dar.
Mwili wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda aliyefariki juzi katika hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu, umewasili leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Emirates.
Mwili wa Waziri Kigoda utaagwa LEO viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment