Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, October 31, 2015

NDEGE YA URUSI YAANGUKA IKIWA NA ABIRIA ZAIDI YA 200

Ndege ya shirika moja la ndege la Urusi, iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 200, imeanguka katika eneo la Sinai nchini Misri.Ndege hiyo aina ya Airbus A-321 ilikuwa imetoka mji wa Sharm el-Sheikh ikielekea mji wa St Petersburg nchini Urusi.Vyombo vya habari nchini Misri vinasema mabaki ya ndege hiyo yamepatikana na magari ya uokozi zaidi ya 20 zimetumwa katika eneo la ajali.Rais wa Urusi Vladimir Putin ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa za waathirika na kuagiza uchunguzi ufanyike, huku akitangaza kesho kuwa ni siku ya maombolezo.

No comments:

Post a Comment