Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, October 16, 2015

UNICEF YAKABIDHI MAGARI KUMI( 10) YA KUBEBEA WAGONJWA MKOANI MBEYA

Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Unicef Dkt Jama Gulaid akitoa hotuba katika sherehe ya makabidhiano ya magari ya kubebea  wagonjwa Mkoa wa Mbeya15 Octobar  2015
Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Ndugu Prisca Butuyuyu akitoa taarifa ya huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika Mkoa wa Mbeya kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa 15 Octobar 2015.
Mwakilishi UNICEF Dkt Jama Gulaid kulia akimkabidhi Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Kastro Msigala taarifa muhimu za magari hayo yenye thamani ya shilingi mil 700 .



Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya pamoja na wageni waalikwa wakishiriki kikamilifu tukio la makabidhiano ya magari ya wagonjwa  Mkoa wa Mbeya 15 Octobar 2015 kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF.

Timu ya Uendeshaji wa huduma za za Afya Mkoa wa Mbeya

Kastro Msigala Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za makabidhiano ya magari kumi ya kubebea wagonjwa ambayo yametolewa na shirika la kimataifa la UNICEF Octobar 15 mwaka huu.

Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Kastro Msigala akikata utepe kuashiria kupokea rasmi msaada wa magari hayo kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF msaada ambao umegharimu kiasi cha shilingi Mil 700.


Meza kuu katika  picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mbeya na wawakilishi wa Shirika la UNICEF.

Meza kuu katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa mbeya .

Meza Kuu katika picha ya Pamoja na timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa wa Mbeya .

Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi shirika la UNICEF.


 
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa  linalo shughulikia watoto Duniani (UNICEF) limekabidhi msaada wa magari kumi  ya Kubebea wagonjwa yenye tahamni ya shilingi mil 700.7  kwa serikali ya Mkoa wa Mbeya .


Aidha shirika hilo lina mpango wa kuboresha vituo 184 vya kutolea huduma za afya katika mkoa huo wa mbeya ambavyo ni vituo afya na hospital 30 pamoja na zahanati 154  sanjali na kuvipatia vifaa muhimu vya kutolea mafunzo kwa watumishi wake.


Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Octobar 15 mwaka huu  Mwakilishi wa shirika la  UNICEF   nchini Tanzania Dkt Jama Gulaid  amesema shirika hilo limetenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya mradi huo.


Amesema mchango wa UNICEF katika sekta afya na lishe hapa mkoani mbeya imepanua wigo kutoka halmashauri mbili za mkoa huo hadi kufikia halmashauri zote katika kipindi cha miaka miwili .


Aidha Dtk, Jama amesema katika kukabiliana na magonjwa na vifo vya watoto na wanawake wajawazito ,UNICEF imechangia vifaa tiba muhimu ikiwa ni pamoja vile vya uchunguzi wa ujauzito ,upasuaji  sanjali na vifaa kuwasaidia watoto wachanga kupumua mara wanapo zaliwa na vifaa vingine vya utoaji wa huduma katika idara ya uangalizi maalumu  ICU.


Aidha  amewataka viongozi hao wa mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanaweka juhudi kubwa zaidi katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kuhakikisha kwamaba kina mama wajawazito wote wanapata huduma za afya bure kwa wakati.


Awali akisoma  taarifa ya huduma za afya ya uzazi na mtoto katika mkoa mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto Ndugu Prisca  Butuyuyu amesema toka shirika hilo la UNICEF  lianze kufanya mwaka 2012 huduma za afya zimeimalika kwa kiasi kikubwa hususani kwa kuweza kuzuia vifo vya uzazi na vya watoto wachanga.


Amesema kwa ujumla hali ya vifo hususani vilivyokuwa  vinatokea katika vituo vya huduma vimepungua kutoka 140  kwa mwaka 2012 na kufikia vifo 94 kwa kwa mwaka 2014 pamoja na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 602 kwa mwaka 2012 hadi kufikia 568  mwaka 2014 ambapo punguzo hilo ni sawa na asilimia 33.9 na 5.7 kwa watoto wachanga.


Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kaimu katibu Tawala Ndugu Kastro Msigala amelishukuru shirika hilo kwa msaada wa magari hayo sanjali na kutoa wito kwa viongozi  wa halmashauri ambao ni wakurugenzi na waganga wakuu kuhakikisha wanayatunza magari hayo ili yaweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi.


Msaada huo wa magari imegawanywa katika halmashauri zote mkoa huo wa mbeya ambazo ni Ileje,Mbozi,Mbeya vijijini,Rungwe,Busokelo,Mbarali pamoja na Kyela na Momba .

Mwisho

(Imeandaliwa na Jamiimojablog Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya  0759406070 )

No comments:

Post a Comment