Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, October 27, 2015

WILFRED LWAKATARE (CHADEMA) ATANGAZWA KUWA MBUNGE WA BUKOBA MJINIHatimaye Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare ameibuka kidedea na kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki. Matokeo hayo yalitangazwa jana usiku na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli. Kura za Udiwani Chadema/ Ukawa imeshinda Kata zifuatazo: Kahororo, Kagondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Hamugebe, Kashai, Bakoba na Bilele. CCM imepata Kata ya Rwamishenye, Buhembe, Miembeni, Nyanga na Ijunganyondo. Picha na Faustine Ruta, Bukoba

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli akitoa matokeo usiku wa jana majira ya saa 2:30 usiku mara baada ya kumalizika kuhesabu kura zilizopigwa jimboni hapo na kumtangaza Lwakatare kwamba ndie mshindi na Nafasi hiyo ya Ubunge Bukoba Mjini. 
Bw. Aron T. Kagurumjuli (Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini) akiendelea na zoezi la kutangaza matokeo usiku wa jana.

 
Mshindi wa nafasi ya Ubunge wa Bukoba Mjini Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akifurahia baada ya kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho baada ya kumwangusha mgembea mwenza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki jana usiku.

LICHA ya kuonekana kana kwamba hapakuwa na dalili zozote za fujo wakati wa zoezi la upigaji kura za Ubunge na udiwani, hali ilibadilika jana jumatatu asubuhi baada ya wafuasi wa chama cha Chadema kutaka matokeo mapema baada ya kupata matokeo hayo usiku wa kuamkia jana kuwa Chadema imeshinda katika Kata 9 kati ya 14 wafuasi hao waliandamana katika maeneo ya mji wa Bukoba wakitaka majibu yatolewe mapema. Kitu ambacho hakikufanyika na kupelekea kuleta ghasia jimboni hapo. Hali hiyo ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya wafuasi wa chama cha Chadema ambao mpaka usiku wa jana walikuwa wamejaa katika eneo la ofisi za Halmashauri ya Bukoba Mjini waishinikiza matokeo kutangazwa. Wafuasi wa chama cha Chadema walisababisha vurugu zikiwemo kurusha mawe na ndipo ndipo jeshi la polisi mjini hapo walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika Ofisi za Halmashauri. Hali hiyo ilitulia baada ya Viongozi wa Chadema kuwatuliza na ndipo Matokeo yakatangazwa. 

Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea hao wawili ambao ni Wilfred Lwakatare wa chama cha Chadema na aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia chama cha CCM Khamis Sued Kagasheki. Kitu kilichopelekea kurudiwa kuhesabiwa kwa kura zote na kupata uhakika wa kutosha.
Kura zilizokubalika ni 54,211 sawa na asilimia 98.54, kura zilizoharibika ni 805 sawa asilimia 1.46, Matokeo ni kama ifuatavyo TLP kura 81 sawa na asilimia 0.2, ACT kura 453, Khamis Sued Kagasheki wa CCM amepata kura 25,565 sawa na asilimia 47.2, Wilfred Muganyizi Lwakatare wa Chadema amepata kura 28,112 sawa na asilimia 51.9Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika katika Ofisi za Halmashauri Bukoba wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa huo wa Wabunge.
Waandishi wa habari na Makada wa Chama cha Chadema wakiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba wakisubilia matokeo kutangazwa.
Diwani wa Kata ya Kahororo Chif Kalumuna(kulia)  akiwa amembeba mshindi wa ubunge jimbo la Bukoba Mjini bw. Wilfred Lwakatare mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika kutaka kuvamia Ofisi za Halmashauri ya Bukoba kudai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge na Polisi walikuwa tayari kuwakabili vilivyo na kuzuia umati huo mkubwa.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo yatolewa baada ya kuchukuwa muda tangu asubuhi mpaka jioni hii.
Hali ilivyokuwa hapo jana jioni maeneo ya karibu na Ofisi za Halmashauri.
Hapa ikabidi kiongozi wa Chadema aliyeshinda katika Kata ya Kashai kupitia chama hicho awatulize kwamba matokeo yanaenda kutolewa jioni hii.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo ya Kiongozi wao.

No comments:

Post a Comment