Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 2, 2015

ALIKIBA AKIWA MBUGA YA KRUGER NATIONAL PARK HUKO SOUTH

Alikiba ndani ya South Africa,YES.hii sio safari ya kwanza kwenye siku za hivi karibuni japo safari za kwanza na hii ya sasahivi ziko tofauti kidogo.
Alikiba ana kazi nyingine iliyomfanya akatua South Africa kwa mara nyingine !!
Alikiba yuko South Africa toka November 29 2015 akiwa kama Balozi wa kupingana na ujangili… kilichompeleka South Africa ni ishu ya kushiriki kongamano linalowakutanisha watu mbalimbali ikiwemo Wakurugenzi mbalimbali kutoka China na Africa pamoja na viongozi wa taasisi za kijamii, na kati ya mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na njia bora za kusaidia utunzaji wa wanyamapori pamoja na hifadhi.
AC8U4832-1
Nchi yangu imepoteza tembo wengi sana ndani ya miaka michache iliyopita kwa sababu ya ujangili… ni lazima tuangalie njia za kushirikiana kuhakikisha tunazuia mauaji hayo na kulinda wanyamapori wetu.”- sentensi za kwanza za Alikiba kwenye ujumbe wake South Africa.

Sote tuna majukumu kuhakikisha tunalinda wanyamapori wetu, mimi kama msanii na mwanamuziki natumia nafasi yangu kusimamia suala hili na kuhimiza watu wengine wengi zaidi waunge mkono hizi jitihada.”- Alikiba.

 
Alikiba ni Balozi wa WildAid Campaign ambayo inapiga vita ujangili ambapo mwanzo wa November 2015 alikuwa Marekani ambako alikutana na Mabalozi wengine kama akinaFergieLupita Nyong’o, na mastaa wengine wakubwa Duniani… ziara hii ya Alikibaitaendelea mpaka December 03 2015 na kati ya maeneo ambayo atatembelea ni pamoja na hifadhi ya wanyama ya Kruger National Park… Kila la heri mtu wetu #KingKiba.

No comments:

Post a Comment