Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, December 8, 2015

MAJAMBAZI WAVAMIA NA KUPORA PESA CRDB NA DCB BANK CHANIKALeo eneo La Chanika, Dar es salaam mida ya saa 9 jioni majambazi wapatao zaidi ya 8 wavamia na kuziteka Bank mbili zilizo eneo moja kwa muda wa dakika 45. CRDB ambayo hata haijaanza kufanya kazi rasmi na DCB Bank

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Ulrich Matei, ameithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba majambazi hao wanasadikiwa kuwa walikuwa kati ya 6 hadi 8.


Amesema wahalifu hao walianza kuingia kwenye Benki ya DCB na kupora fedha zilizokuwa kaunta na muda mchache baada ya hapo walivamia Benki ya CRDB na kupora fedha ambazo hadi sasa haijajulikana thamani yake.
Aidha, amesema majambazi hao waliwaua askari wawili wa Suma JKT, waliotambuliwa kwa majina ya Ramadhani Halidi na Shane Rajabu.


"Tumeanza upelelezi ikiwemo kuelekea katika maeneo ya Mkuranga ambapo ndiko tunakoamini kwamba hawa wahalifu wameelekea, tutakapowakamata tutawapa taarifa kamili" Alisema Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala.

CHANZO: JAMII FORUM

No comments:

Post a Comment