Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 9, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI NA WANANCHI WA ENEO LAKE KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA, MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kufagia na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015. 

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay- Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco, kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi wa eneo hilo kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiingia kukagua eneo la kuhifadhia Taka lililopo eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco, wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi na wasanii mbalimbali waliojitokeza kushiriki naye katika zoezi hilo baada ya kuhitimisha zoezi la usafi eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam, leo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoka eneo la Morocco, baada ya kushiriki zoezi hilo na wananchi wa eneo hilo la kufanya usafi wa mazingira leo.
***********

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Anwani ya simu: “MAKAMU”, Barabara ya Luthuli,
Simu Na. +255 2116919 P.O Box 5380,
Fax Na. +255 2116990 Dar es Salaam. 
Barua Pepe: km@vpo.go.tz TANZANIA.

09/12/2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya Mtaa wa Oysterbay na Morocco stand katika wilaya ya Kinondoni katika kuadhmisha miaka 54 ya uhuru wa Tanzania Bara.



Akizungumza na wananchi waliojumika katika maeneo ya Morroco stand Makamu wa Rais amewaagiza viongozi wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam kutoa taarifa za wazabuni wa kufanya usafi ili ziweze kufuatiliwa.

“Haya makampuni yanapewa fedha kwa ajili ya kazi ya kufanya usafi; lakini inaonyesha hayafanyi kazi ipasavyo kwa sababu mji bado ni mchafu,” Alisema Mhe. Samia.

Alielezea kufurahishwa kwake kwa jinsi wananchi walivyojitokeza katika zoezi hilo ambalo alisema ni endelevu na kuwataka Wakuu wa wilaya na wenyeviti wa serikali za mitaa kupanga siku maalum kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo yao.

Makamu wa Rais alisema Watanzania hawawezi kujivunia miaka 54 ya uhuru ikiwa miji ni michafu na kuwataka wananchi kushirikiana kutekeleza kauli mbiu ya uhuru na kazi kwa kila mmoja kufanya kazi bidii mahali alipo aweze kuongeza tija ambayo italiwezesha Taifa kupata madawa na elimu bora. 

Pamoja na wananchi waliojumuika na Makamu wa Rais kufanya usafi katika Mtaa wa Oysterbay, kwa upande wa Morocco stand walikuwepo pia wafanyakazi wa benki ya DTB, Radio ya EFM na wasanii mbalimbali

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais

Dar es salaam

No comments:

Post a Comment