Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, December 10, 2015

TAZAMA PICHA NA VIDEO:::RAIS DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKITANGAZA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa.

Hatimaye rais Magufuli atangaza baraza lake la mawaziri ambapo baraza hilo lina wizara chache kama alivyoeleza hapo awali.

Rais Magufuli ameagiza fedha zilizotengwa kwaajili ya semina elekezi kwa mawaziri zielekezwe kwajili ya matumizi mengine.

Rais Magufuli amewataka mawaziri wapya kufanya kazi kwa bidii kwaajili ya manufaa ya wananchi wote bila kujali tofauti zao.
---
Baraza jipya la Mawaziri hili hapa limetangazwa na rais John Magufuli mapema leo.

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri - George Simbachawene na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.


Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri - Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri - Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri - William Ole Nasha

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani

Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri - Ashantu Kizachi

Wizara ya Nishati na Madini
Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.
Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.

Wizara ya Katiba na Sheria,
Waziri - Harrison Mwakyembe

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri - Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri - Dk. Hussein Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri - Charles Kitwanga.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri - William Lukuvi
Naibu Waziri - Angelina Mabula

Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Charles Mwijage.

Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri - Ummy Mwalim
Naibu Waziri – Dkt. Hamis Kigwangala

Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri - Nape Nnauye
Naibu Waziri - Anastasia Wambura.

Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu Waziri– Inj. Isack Kamwela
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana kwa furaha na wanahabari mara baada ya kutangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na wanahabari waliofika kumsikiliza wakati akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa walioketi vitini ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akirejea ofisini baada ya kutangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue

PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment