Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 2, 2015

WARAKA TOKA KWA MDAU:::CHADEMA Fanyeni Mikakati kuimarisha Chama Acheni Siasa za Kutumia matatizo ya Watanzania

Naamini viongozi wa CHADEMA wanafika hapa JF, lkn pia najua wanachama ana wafuasi wapo wengi hapa JF. Kwa muda mrefu CDM imetusaidia watanzania kutufumbua macho wakati ufisadi ukitamalaki. Yaliyopita si ndwele tigange yajayo.

Tangu uchaguzi umalizike CDM imekuwa ni chama cha matukio, kwa kizungu reactive to the incident. Tumeona CDM ilivyotumia msiba wa MAWAZO (MUNGU AMREHEMU) kwa sababu kama amekufa kwa sababu ya tofauti za kisiasa watanzania tunaelekea kubaya. Lakini CHADEMA kilitumia msiba huu kujipatia umaarufu km kwamba CHAMA CHA MAPINDUZI ndicho kiliwatuma waharifu kumuua kamanda MAWAZO, sitaki kuamini km CCM kama chama wana uwezo wa kufanya haya kwaani 

 
uchaguzi umeisha na walishinda kwa 95% kanda ya ziwa.
Kabla ya hili la mawazo CHADEMA walikuwa wanatafuta sympathy ya wananchi kwa kutumia kesi mbalimbali mfano ni kesi ya SHEKH PONDA aliyeshinda kesi hapo jana. Kuna wakati Fulani alikuwa akitetewa na wakiri maarufu wa CHADEMA pale Morogoro. Sijui kwa nini CDM waliingiliaje kesi hii kidogo wamuharibie mshitakiwa kwaani serikali ingeona kama vile alikuwa anatumiwa na CHAMA.

Jana baada ya kupata ushindi dhidi ya serikali niliona viongozi wote wa CDM wakiongozwa na aliyekuwa mgombea ubunge ndugu MARCUS ALBAN waliongoza waaumini kutoka eno la mahakama mpaka eneo la msikiti wa MUNGU MMOJA.
Wakati wa kampeni tuliskia aliyekuwa mgombea Urais kupitia CHADEMA Mheshimiwa Edward Lowassa kuwa kama angechukua dora basi angewaachia huru watuhumiwa mbalimbali wakiwamo Shekh Farid na Babu seya. Kwa kifupi kama hawana makosa wanastahili kuachiwa kwa mujibu wa sheria lakini siyo kwa mujibu wa matakwa ya mtu.

USHAURI KWA CDM NA UPINZANI:
Fanyeni vitu endelevu na vinavyoenekana, yaani sustainable and tangible la sivyo mtasahaulika, kumbukeni watanzania ni wepesi sana wa kusahau, jumrisha na kasi ya serikali ya awamu ya tano ambayo imezichukua sera za upinzania kuzifanyia kazi hasa ile ya ufisadi iliyotupwa baada ya kumpkea LOWASSA kitendo kilichoitwa na kubadili gear angani.

ACHENI KUTUMIA MATATIZO KATIKA JAMII KUTAFUTA UMAARUFU WA KISIASA.Chanzo Jamii Forum

No comments:

Post a Comment