Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, January 28, 2016

MRADI MANJANO DREAM MAKERS WA KUKWAWEZESHA MANAWAKE WAJASIRIAMALI WAINGIA ZANZIBAR

 Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kupitia Tasinia ya Urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers waingia Zanzibar. Wataalamu kutoka Taasisi ya Manjano Foundation wataendesha mafunzo kuanzia tarehe  1 February 2016 kwenye ukumbi wa  Mtoni Marine Hotel Zanzibar. Wanawake 30 wa Zanzibar watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Wanawake wakazi wa Zanzibar wanaopenda kunufaika na mradi huo  wanaombwa kwenda kwa usaili na kujiandikisha siku ya Jumamosi tarehe 30 January 2016 kuanzia saa tatu asubuhi kwenye hoteli ya Mtoni Marine mjini Zanzibar.
Mafunzo yana lengo la  kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na 

 
kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba kwajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea .
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 759413234

No comments:

Post a Comment