Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, March 9, 2014

DR. SHEIN AKIENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU DODOMA

D92A4316Makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein akiongoza kikao maalum cha kamati Kuu ya CCM kilichomjadili ili kumpitisha mgombea Uchaguzi kwa tiketi ya CCM jimbo la Chalinze Bwana Ridhiwani Kikwete.Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alitoka nje kwa mujibu wa kanuni za CCM wakati wa kikao hicho kwasababu ana uhusiano wa moja kwa moja na mgombea.Bwana Ridhiwani Kikwete alishinda kura za maoni wiki iliyopita na hivyo kumpa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye kinyang’anyiro hicho kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo la Chalinze Marehemu Saidi Bwanamdogo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana.

D92A4287Baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu ya CCM wakiwa katika kikao maalum mjini Dodoma leo (picha na Freddy Maro).

No comments:

Post a Comment