Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, March 12, 2014

TAARIFA KAMILI KUHUSU AJALI YA BASI LA HOOD:: LILILOPATA AJALI NA KUSABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA NA MAJERUHI 16


Basi la Kampuni ya Hood likiwa limepinduka na watu kuumiavibaya eneo la Same leo asubuhi
Basi la Hood linalofanya safari zake kutoka Arusha kwenda Mbeya, namba za usajili T.488 AXV aiana ya Scania imepata ajali mbaya leo, majira ya saa 3 asubuhi na kusababisha kifo cha Mtu mmoja na kujeruhi wengine 16.

Ajali hiyo imetokea katika, barabara ya Same - Mwanga, Kijiji cha Kiverenge wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo taarifa za awali zinasema  kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa tairi ya mbele.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema katika ajali hiyo alifariki Abiria mmoja aliyemtaja kwa jina la Joshua Likumbia, Raia wa Kenya, ambaye alikuwa akisafiri kuelekea jijini Mbeya.

Kamanda Boaz amesema majeruhi katika ajali hiyo ambao ni 16, akiwemo dereva wa Basi, Fadhili Hashim wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Same na Hospitali ya Rufaa mkoani Kilimanjaro, KCMC.

Kamanda Boaz ameendelea kufafanua kuwa majeruhi hao nane wamelazwa Same huku wengine 8 wakikimbizwa mjini Moshi katika hospitali ya KCMC kutokana na hali zao kuwa mbaya ambapo watatu kati yao wakia wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. 

No comments:

Post a Comment