Dalili, mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na dalili
zifuatazo, kwa mwanaume hutokwa na manii zilizochanganyika na damu, kukojoa
mkojo mweusi au uliochanganyika na damu, kutoa mkojo kidogo sana tena kwa
shida, kukojoa mara kwa mara na kushindwa kumaliza mkojo wote.
Wengine huona dalili za mkojo kujitokea wenyewe, hivyo
mhusika kujikojolea, kusikia maumivu wakati wa kukojoa au chini ya tumbo au
kwenye kinena, mkojo kutawanyika ovyo wakati wa kukojoa na uume kuvimba.
Daktari akiona moja ya dalili hizo mgonjwa anaweza
kuchunguzwa kwa vipimo tofauti kama vile kile cha kuchunguza mrija pamoja na
kibofu cha mkojo (cystoscopy), kuangalia kiasi cha mkojo kinachobaki katika
kibofu baada ya mkojo kutoka, X-ray ya mrija wa mkojo (Retrograde urethrogram)
atapimwa kama ana magonjwa ya zinaa kwa kumfanyia uchunguzi wa mkojo
(Urinalysis) pamoja na kuotesha mkojo (Urine culture).
TIBA Mrija unaweza kutanuliwa wakati wa kipimo cha
cystoscopy na hiyo ikawa ndiyo mojawapo ya tiba au dawa pekee ya uhakika ni
mgonjwa kufanyiwa upasuaji ambao unategemea eneo lilipo tatizo na ukubwa wa
tatizo.
Kwa mgonjwa ambaye amepata shida ya ghafla ya kushindwa
kutoa mkojo (acute retention of urine), matibabu ya dharura ya kumuwekea
catheter kupitia juu ya kinena hufanyika.
Hii husaidia kibofu kutoa mkojo nje kupitia kwenye bomba
lililowekwa chini ya tumbo. USHAURI Mgonjwa mwenye tatizo hili atibiwe haraka
maana tatizo likiachwa linaweza kusababisha kuziba kabisa kwa njia ya mkojo na
kusababisha mkojo kujaa katika kibofu, hali ambayo, pamoja na kuleta maumivu
makali kwa mgonjwa inaweza pia kusababisha figo kushindwa kufanya kazi.
Watu wajikinge na magonjwa ya zinaa ambayo yanasababisha
tatizo hili, wawe makini na kazi zinazoweza kusababisha kuumia sehemu nyeti na
kuzalisha tatizo hili.
Pata dondoo za afya za madaktari bingwa kwenye simu yako ya
Vodacom bure: Tuma DAKTARI kwenda 15542
No comments:
Post a Comment