Watumishi
wa PSPF wakitoa maelezo ya namna ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa
hiari (PSS) kwa waendesha bodaboda waliohudhuria kwenye tamasha la siku
ya bodaboda
| Meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) wa PSPF, Mwanjaa Sembe akitoa maelekezo ya namna ya kujaza fomu za kujiunga na PSS |
| Afisa mwandamizi wa fedha wa PSPF, Hidaya Mganga akimsaidia kujaza fomu mmoja wa waendesha bodaboda aliyejitokeza kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari wa PSPF |
| Afisa wa mpango wa uchangiaji wa hiari Mwajuma Ali akipitia fomu za usajili wakati wa tamasha hilo |
| Afisa wa uendeshaji PSPF, Halima Isaa akiwaelekeza namna ya kujaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS |
| Mtumishi wa PSPF akigawa vipeperushi kwa waendesha bodaboda vinavyoeleza namna ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari |
| Waendesha bodaboda wakisoma fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari kabla ya kujaza maelezo yao na kujisajili |
| Afisa fedha wa PSPF, Reginald Msafiri akigawa vipeperushi |
| Waendesha bodaboda wakisoma vipeperushi vya PSPF wakati wa tamasha |
![]() |
| Msanii Linex akifanya yake Viwanjani hapo |
Watumishi wa PSPF katika picha ya pamoja
Zaidi ya asilimia 90 ya waendesha bodaboda waliohudhuria tamasha la siku ya waendesha bodaboda lililopewa jina la siku ya waendesha bodaboda wamejiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) wa mfuko wa Pensheni wa PSPF. Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Mwanjaa Sembe amesema udhamini wao katika tamasha hilo ni moja ya mikakati yake ya kuwafikia watu mbalimbali walio kwenye sekta isiyorasmi ili wajiunge na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS).
Wakati tamasha hilo lililofanyika jumapili ya desemba 22 mwaka 2013 likiendelea waendesha bodaboda wengi walifurika kwenye banda la mfuko wa pensheni wa PSPF kujisajili na kujiunga na mpango wa hiari wa uchangiaji PSS.
|

No comments:
Post a Comment