Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 5, 2013

DOWNLOAD NA SIKILIZA NYIMBO MPYA YA ROMA 2030

HIZI NI VIDEO NYINGINE ZA WAKATI WA FUJO KWENYE SHOW YA DIAMOND MAISHA CLUB.

Hii video ya pili inaonyesha jinsi watu wakitoka nje ya ukumbi wa Maisha Club baada ya fujo kutokea ndani

KIJANA ALA KICHAPO MARA BAADA YA KUIBA KITIMOTO NA BIA JIJINI DAR



Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akilia kwa uchungu mara baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali mara baada ya kudaiwa ameiba nyama ya Nguruwe (Kitimoto) pamoja na Bia katika glosali jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya wasamalia wema akimtetea kijana huyo ambaye alipokea kichapo.
Akijitetea.
Akisaidiwa na wasamalia wema.
Kijana anaedaiwa kuiba nyama ya Nguruwe (Kitimoto) na bia katika glosali iliyopo Namanga jijini Dar es Salaam

YANGA YATOKA SARE NA ARMINIA BIELEFELD KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI NCHINI UTURUKI




Timu ya Young Africans Sports Club imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo jioni katika uwanja wa Adora Football pemebni kidogo ya mji wa Antalya.
Armini Bielefeld ilianza soka kwa kasi kwa lengo la kujipatia bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Yanga na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' ilikuwa kikwazo kwao kwani mashambulizi yao yaliishia mikononi mwake.

 Ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu Young African iliweza kuonyesha soka safi katika kipindi cha kwanza hali iliyowashangaza wajerumani hao na kipindi cha pili kuamua kufanya mabadiliko ya kikosi kizima.
Viungo wa Yanga Frank Domayo, Haruna Niyonzima na Kabange Twite waliweza kutawala mchezo kwa dakika 45 zote za kipindi cha kwanza huku baadhi ya wajerumani waliokuwa wakishuhudia mchezo huo kushangazwa na kiwango cha timu ya Yanga
Hadi mapumziko timu zote zilikwenda mapumziko , Young Africans 0 - Arminia Bielefeld.
Kipindi cha pili Arminia Bielefeld iliamua kubadilisha kikosi chake chote cha wachezaji kwa lengo la kuingiza nguvu mpya ili waweze kuikabili kasi ya wachezaji wa Yanga ambao walionekana kuwa imara na bora zaidi.
Dakika ya 55 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Said Bahanuzi na David Luhende na nafasi zao kuchukuliwa na Jerson Tegete na Saimon Msuva.
Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 60 ya mchezo, akiunganisha pasi safi aliypewa na Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa Arminia Bielefeld na kumpa pasi Tegete ambaye aliukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao la kwanza.
Kuona hivyo wajerumani walikuja juu kusaka bao la kusawazisha, lakini bado ukuta wa Yanga uliendelea kuonekana kuwa makini lakini makosa ya mshika kibendera yaliipelekea Armini Bielefeld kupata bao la kusawazsiha dakika ya 81 kupitia kwa Eric Agyemang amabaye alikua ameotea.
 Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Young Africans 1 - 1 Armini Bielefeld.
 Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema amefurahishwa na kiwango walichokionyesha wachezaji wake na anaamini kadri siku zinavyokwenda wanazidi kuimarika na kuwa bora, hivyo katika michezo mingine wataendelea kuonyesha mabadiliko makubwa.
 Young Africans: Ally Mustafa 'Barthez, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani, Kabange Twite, Haruna Niyonzima/Nizar Khalfan, Frank Domayo/Nurdin Bakari, Said Bahanuzi/Jerson Tegete, Didier Kavumbagu, David Luhende/Saimon Msuva

DEMBA BA AANZA NA MBILI CHELSEA IKIUA 5-1 KOMBE LA FA.... MAN CITY YAPIGA MTU 3-0 BALOTELLI NDANI



Demba Ba akishangilia goli lake katika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Chelsea
Demba Ba akishangilia goli lake katika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Chelsea

Nimekuja kufanya kazi...

Nataka msahau machungu ya kumkosa Drogba

Ba akishangilia

Ba akitupia goli la pili

Hamkukosea kunisajili... Ba akishangilia

Balotelli akishuhudia mechi yao dhidi ya Watford kutokea benchi leo.




MSHAMBULIAJI mpya wa Chelsea, Demba Ba aliyejiunga jana akitokea Newcastle, ameanza mechi yake ya kwanza na magoli mawili wakati alipoiongoza Chelsea kushinda 5-1 dhidi ya Southampton katika mechi yaoya Kombe la FA iliyochezwa leo.

Mabingwa watetezi licha ya kutawala mechi, walijikuta wakitanguliwa kwa goli la dakika ya 22 lililofungwa na Jay Rodriguez aliyepachika bao lake la tano msimu huu kufuatia pasi kali ya kupenyezewa na Jason Puncheon.

Msenegal huyo aliyekuwa amevaa jezi ya Chelsea kwa mara ya kwanza, aliisawazishia timu yake mpya katika dakika ya 35 akimalizia kuuvusha kwenye mstari mpira ulipigwa na Juam Mata ambao ungeweza kuokolewa na beki wa wenyeji.

Muafrika mwenzake Ba, Victor Moses, raia wa Nigeria, aliifungia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 45 akipiga shuti zuri la mguu wa kushoto kutokea nje ya boksi kufuatia pasi ya nahodha wa kipindi cha kwanza, Ashley Cole.

Beki Branislav Ivanovic aliongeza la tatu katika dakika ya 52, Ba akakamilisha mwanzo wake mzuri kwa kufunga la nne katika dakika ya 61 kabla ya Frank Lampard aliyeingia kutokea benchi kufunga la tano kwa penalti katika dakika ya 83.

Katika mechi nyingine za leo, Man City ambayo ilimuanzisha benchi mshambuliaji mtata Mario Balotelli kabla ya kuingia katika dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Edin Dzeko, iliilaza Watford kwa magoli 3-0 yaliyofungwa na Carlos Tevez kwa 'fri-kiki' ya hatari kutoka umbali wa yadi 25 katika dakika ya 25, Gareth Barry (dk. 44) na Marcos Lopes (dk.  90+1).

Tottenham ilishinda kwa magoli 3-0 dhidi ya Coventry yaliyofungwa na Clint Dempsey (dk. 14 na dk. 37) na Gareth Bale (dk. 33).


MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZA KOMBE LA FA LEO

Southampton 1 - 5 Chelsea

Man City 3 - 0 Watford

Tottenham 3 - 0 Coventry

Wigan 1 - 1 Bournemouth

QPR 1 - 1 West Brom

Southend 2 - 2 Brentford

Aldershot 3 - 1 Rotherham

Aston Villa 2 - 1 Ipswich

Barnsley 1 - 0 Burnley

Blackburn 2 - 0 Bristol City

Bolton 2 - 2 Sunderland

Charlton 0 - 1 Huddersfield

Crawley 1 - 3 Reading

Crystal Palace 0 - 0 Stoke

Derby 5 - 0 Tranmere

Fulham 1 - 1 Blackpool

Hull 1 - 1 Leyton Orient

Leeds United 1 - 1 Birmingham

Leicester 2 - 0 Burton Albion

Luton 1 - 0 Wolves

Macclesfield 2 - 1 Cardiff

Middlesbrough 4 - 1 Hastings Utd

Millwall 1 - 0 Preston

Nottm Forest 2 - 3 Oldham

Oxford Utd 0 - 3 Sheff Utd

Peterborough 0 - 3 Norwich

Sheff Wed 0 - 0 MK Dons

PICHA HII NOMA:UREFU WA SHIKOKOTI WAWADATISHA WAAMUZI NI JANA KWENYE MAPINDUZI CUP TUSKER V SIMBA



waamuzi mechi ya jana kati ya simba na Tusker wakimshanga Kapteni  na mlizi wa timu ya Tusker ya kenya kwa urefu alionao

KWELI MOMBASA RAHA....HIKI NDO KITUO CHA TV KENYA K24 KIFUNDISHACHO JINSI YA KUFANYA MAPENZI KWA WANAWAKE.Angalia JINSI WANAVYOFUNDISHA

PATA MAFUNZO KATIKA KIPINDI CHA MOMBASA RAHA POSITION KIENDESHWACHO NA SON KANEKE KUPITIA KITUO CHA K24 CHA NCHINI KENYA

ANGALIA PICHA YA MTOTO ALIYEZALIWA AKIWA NA MIGUU SITA!


Mungu anatisha, sasa wewe fanya ujeuri wako tu kwa kukufuru kwa viungo kamili ulivyojaaliwa!

Boti ya Mv Yarabi Tunusuru imezama na watu 9 wamefariki dunia. -ANGALIA VIDEO

Watu tisa wamekufa , kumi na wawili hawajulikani walipo na sitini na wanne wameokolewa baada ya boti ya Mv Yarabi Tunusuru Waliyokuwa wakisafiria katika ziwa Tanganyika kutoka Kirando mkoani Rukwa kwenda Kongo DRC kupitia kupinduka na kuzama katika Kijiji cha Herembe wilayani Uvinza mkoani Kigoma Ijumaa usiku. source ITV

MAGAZETI YA JUMAMOSI YA LEO JAN 5 VICHWA VIKUBWA LEO MWANAJESHI ALIYEPIGA PICHA NA LEMA AKAMATWA,KIKWETE AMZIKA SAJUKI NA ULIMBOKA AWAGONGANISHA POLISI.



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

MAMBO YANAENDA HOVYO UWANJANI NA NYUMBANI KWA AGUERO - AACHANA NA MKEWE MTOTO WA MARADONA



Sergio Aguero ameachana na mkewe na Giannina, ambaye ni mtoto wa Diego Maradona, baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka minne.

Giannina sasa anaaminika kwamba anaishi jijini Madrid na mtoto wao mwenye miaka mitatu Benjamin baada ya kuthibitisha kuachana kwake na Aguero kwenye mtandao wa Twitter.

Alisema 'tumeachana' kabla ya baadae kuongeza 'mwaka mgumu' na 'kumekuwepo na mabadiliko mengi'.

Kwenye Twitter, shabiki mmoja alimwambia Giannina: ‘Aguero hastahili kuwa nawe na mjinga' lakini akamjibu shabiki huyo 'Usiseme hivyo, ni baba wa mtoto wangu na hayupo kama ambavyo umesema.'

Sergio Aguero msimu amekuwa hayupo katika kiwango kizuri akiwa amefunga mabao nane tu na ligi ikiwa ipo katika awamu ya pili.