Pages
▼
Saturday, January 5, 2013
HIZI NI VIDEO NYINGINE ZA WAKATI WA FUJO KWENYE SHOW YA DIAMOND MAISHA CLUB.
Hii video ya pili inaonyesha jinsi watu wakitoka nje ya ukumbi wa Maisha Club baada ya fujo kutokea ndani
KIJANA ALA KICHAPO MARA BAADA YA KUIBA KITIMOTO NA BIA JIJINI DAR
Kijana
mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akilia kwa
uchungu mara baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira
kali mara baada ya kudaiwa ameiba nyama ya Nguruwe (Kitimoto) pamoja na
Bia katika glosali jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya wasamalia wema akimtetea kijana huyo ambaye alipokea kichapo.
Akijitetea.
Akisaidiwa na wasamalia wema.
Kijana anaedaiwa kuiba nyama ya Nguruwe (Kitimoto) na bia katika glosali iliyopo Namanga jijini Dar es Salaam
YANGA YATOKA SARE NA ARMINIA BIELEFELD KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI NCHINI UTURUKI
Timu ya
Young Africans Sports Club imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya
Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo
jioni katika uwanja wa Adora Football pemebni kidogo ya mji wa Antalya.
Armini
Bielefeld ilianza soka kwa kasi kwa lengo la kujipatia bao la mapema
lakini umakini wa walinzi wa Yanga na mlinda mlango Ally Mustafa
'Barthez' ilikuwa kikwazo kwao kwani mashambulizi yao yaliishia mikononi
mwake.
Ikiwa ni
mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu Young African iliweza kuonyesha
soka safi katika kipindi cha kwanza hali iliyowashangaza wajerumani hao
na kipindi cha pili kuamua kufanya mabadiliko ya kikosi kizima.
Viungo wa
Yanga Frank Domayo, Haruna Niyonzima na Kabange Twite waliweza kutawala
mchezo kwa dakika 45 zote za kipindi cha kwanza huku baadhi ya
wajerumani waliokuwa wakishuhudia mchezo huo kushangazwa na kiwango cha
timu ya Yanga
Hadi mapumziko timu zote zilikwenda mapumziko , Young Africans 0 - Arminia Bielefeld.
Kipindi
cha pili Arminia Bielefeld iliamua kubadilisha kikosi chake chote cha
wachezaji kwa lengo la kuingiza nguvu mpya ili waweze kuikabili kasi ya
wachezaji wa Yanga ambao walionekana kuwa imara na bora zaidi.
Dakika ya
55 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Said Bahanuzi na David Luhende
na nafasi zao kuchukuliwa na Jerson Tegete na Saimon Msuva.
Jerson
Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 60 ya mchezo,
akiunganisha pasi safi aliypewa na Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa
Arminia Bielefeld na kumpa pasi Tegete ambaye aliukwamisha mpira wavuni
na kuhesabu bao la kwanza.
Kuona
hivyo wajerumani walikuja juu kusaka bao la kusawazisha, lakini bado
ukuta wa Yanga uliendelea kuonekana kuwa makini lakini makosa ya mshika
kibendera yaliipelekea Armini Bielefeld kupata bao la kusawazsiha dakika
ya 81 kupitia kwa Eric Agyemang amabaye alikua ameotea.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Young Africans 1 - 1 Armini Bielefeld.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema amefurahishwa na kiwango
walichokionyesha wachezaji wake na anaamini kadri siku zinavyokwenda
wanazidi kuimarika na kuwa bora, hivyo katika michezo mingine
wataendelea kuonyesha mabadiliko makubwa.
Young
Africans: Ally Mustafa 'Barthez, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub
'Cannavaro', Kelvin Yondani, Kabange Twite, Haruna Niyonzima/Nizar
Khalfan, Frank Domayo/Nurdin Bakari, Said Bahanuzi/Jerson Tegete, Didier
Kavumbagu, David Luhende/Saimon Msuva
DEMBA BA AANZA NA MBILI CHELSEA IKIUA 5-1 KOMBE LA FA.... MAN CITY YAPIGA MTU 3-0 BALOTELLI NDANI
![]() |
| Demba Ba akishangilia goli lake katika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Chelsea |
![]() |
| Demba Ba akishangilia goli lake katika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Chelsea |
![]() |
| Nimekuja kufanya kazi... |
![]() |
| Nataka msahau machungu ya kumkosa Drogba |
![]() |
| Ba akishangilia |
![]() |
| Ba akitupia goli la pili |
![]() |
| Hamkukosea kunisajili... Ba akishangilia |
![]() |
| Balotelli akishuhudia mechi yao dhidi ya Watford kutokea benchi leo. |
| MSHAMBULIAJI
mpya wa Chelsea, Demba Ba aliyejiunga jana akitokea Newcastle, ameanza
mechi yake ya kwanza na magoli mawili wakati alipoiongoza Chelsea
kushinda 5-1 dhidi ya Southampton katika mechi yaoya Kombe la FA
iliyochezwa leo. Mabingwa watetezi licha ya kutawala mechi, walijikuta wakitanguliwa kwa goli la dakika ya 22 lililofungwa na Jay Rodriguez aliyepachika bao lake la tano msimu huu kufuatia pasi kali ya kupenyezewa na Jason Puncheon. Msenegal huyo aliyekuwa amevaa jezi ya Chelsea kwa mara ya kwanza, aliisawazishia timu yake mpya katika dakika ya 35 akimalizia kuuvusha kwenye mstari mpira ulipigwa na Juam Mata ambao ungeweza kuokolewa na beki wa wenyeji. Muafrika mwenzake Ba, Victor Moses, raia wa Nigeria, aliifungia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 45 akipiga shuti zuri la mguu wa kushoto kutokea nje ya boksi kufuatia pasi ya nahodha wa kipindi cha kwanza, Ashley Cole. Beki Branislav Ivanovic aliongeza la tatu katika dakika ya 52, Ba akakamilisha mwanzo wake mzuri kwa kufunga la nne katika dakika ya 61 kabla ya Frank Lampard aliyeingia kutokea benchi kufunga la tano kwa penalti katika dakika ya 83. Katika mechi nyingine za leo, Man City ambayo ilimuanzisha benchi mshambuliaji mtata Mario Balotelli kabla ya kuingia katika dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Edin Dzeko, iliilaza Watford kwa magoli 3-0 yaliyofungwa na Carlos Tevez kwa 'fri-kiki' ya hatari kutoka umbali wa yadi 25 katika dakika ya 25, Gareth Barry (dk. 44) na Marcos Lopes (dk. 90+1). Tottenham ilishinda kwa magoli 3-0 dhidi ya Coventry yaliyofungwa na Clint Dempsey (dk. 14 na dk. 37) na Gareth Bale (dk. 33). MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZA KOMBE LA FA LEO Southampton 1 - 5 Chelsea Man City 3 - 0 Watford Tottenham 3 - 0 Coventry Wigan 1 - 1 Bournemouth QPR 1 - 1 West Brom Southend 2 - 2 Brentford Aldershot 3 - 1 Rotherham Aston Villa 2 - 1 Ipswich Barnsley 1 - 0 Burnley Blackburn 2 - 0 Bristol City Bolton 2 - 2 Sunderland Charlton 0 - 1 Huddersfield Crawley 1 - 3 Reading Crystal Palace 0 - 0 Stoke Derby 5 - 0 Tranmere Fulham 1 - 1 Blackpool Hull 1 - 1 Leyton Orient Leeds United 1 - 1 Birmingham Leicester 2 - 0 Burton Albion Luton 1 - 0 Wolves Macclesfield 2 - 1 Cardiff Middlesbrough 4 - 1 Hastings Utd Millwall 1 - 0 Preston Nottm Forest 2 - 3 Oldham Oxford Utd 0 - 3 Sheff Utd Peterborough 0 - 3 Norwich Sheff Wed 0 - 0 MK Dons | |
PICHA HII NOMA:UREFU WA SHIKOKOTI WAWADATISHA WAAMUZI NI JANA KWENYE MAPINDUZI CUP TUSKER V SIMBA
![]() |
| waamuzi mechi ya jana kati ya simba na Tusker wakimshanga Kapteni na mlizi wa timu ya Tusker ya kenya kwa urefu alionao |
KWELI MOMBASA RAHA....HIKI NDO KITUO CHA TV KENYA K24 KIFUNDISHACHO JINSI YA KUFANYA MAPENZI KWA WANAWAKE.Angalia JINSI WANAVYOFUNDISHA
PATA MAFUNZO KATIKA KIPINDI CHA MOMBASA RAHA POSITION KIENDESHWACHO NA SON KANEKE KUPITIA KITUO CHA K24 CHA NCHINI KENYA
Boti ya Mv Yarabi Tunusuru imezama na watu 9 wamefariki dunia. -ANGALIA VIDEO
Watu tisa wamekufa , kumi na wawili hawajulikani walipo na sitini na wanne wameokolewa baada ya boti ya Mv Yarabi Tunusuru Waliyokuwa wakisafiria katika ziwa Tanganyika kutoka Kirando mkoani Rukwa kwenda Kongo DRC kupitia kupinduka na kuzama katika Kijiji cha Herembe wilayani Uvinza mkoani Kigoma Ijumaa usiku.
source ITV
MAMBO YANAENDA HOVYO UWANJANI NA NYUMBANI KWA AGUERO - AACHANA NA MKEWE MTOTO WA MARADONA
Sergio Aguero ameachana na mkewe na Giannina, ambaye ni mtoto wa Diego Maradona, baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka minne.
Giannina sasa anaaminika kwamba anaishi jijini Madrid na mtoto wao mwenye miaka mitatu Benjamin baada ya kuthibitisha kuachana kwake na Aguero kwenye mtandao wa Twitter.
Alisema 'tumeachana' kabla ya baadae kuongeza 'mwaka mgumu' na 'kumekuwepo na mabadiliko mengi'.
Kwenye Twitter, shabiki mmoja alimwambia Giannina: ‘Aguero hastahili kuwa nawe na mjinga' lakini akamjibu shabiki huyo 'Usiseme hivyo, ni baba wa mtoto wangu na hayupo kama ambavyo umesema.'
Sergio Aguero msimu amekuwa hayupo katika kiwango kizuri akiwa amefunga mabao nane tu na ligi ikiwa ipo katika awamu ya pili.
Giannina sasa anaaminika kwamba anaishi jijini Madrid na mtoto wao mwenye miaka mitatu Benjamin baada ya kuthibitisha kuachana kwake na Aguero kwenye mtandao wa Twitter.
Alisema 'tumeachana' kabla ya baadae kuongeza 'mwaka mgumu' na 'kumekuwepo na mabadiliko mengi'.
Kwenye Twitter, shabiki mmoja alimwambia Giannina: ‘Aguero hastahili kuwa nawe na mjinga' lakini akamjibu shabiki huyo 'Usiseme hivyo, ni baba wa mtoto wangu na hayupo kama ambavyo umesema.'
Sergio Aguero msimu amekuwa hayupo katika kiwango kizuri akiwa amefunga mabao nane tu na ligi ikiwa ipo katika awamu ya pili.












































