Pages

Saturday, October 8, 2011

Cabo snoop kusindikizwa na wasanii zaidi ya tisa

















JUMLA ya wasanii tisa, wanatarajia kumsindikiza mkali wa muziki wa staili ya Kuduro, Ivo Manuel Lemus a.k.a Cabo Snoop kutoka nchini Angola atakayetumbuiza katika siku ya familia (Family Day) kesho katika viwanja vya Leaders Club jijini.

Muangola huyo ambaye amejichukulia umaarufu kutokana na vibao vyake vya Prakatatumba na Windek ataanza kufanya tamasha hilo leo mjini Morogoro, kabla ya kuhamia jijini Dar es Salaam.

Cabo Snoop ambaye alianza kufanya ziara Afrika Mashariki wiki iliyopita katika tamasha la Tusker All Stars jijini Nairobi, atasindikizwa na wasanii kama Asley, Dogo Janja, Godzilla, Barnabas, Linah, Twanga Pepeta, Bob Junior na Diamond.

Waandaaji wa tamasha hilo Prime Time Promotion wamesema kuwa tamasha hilo limepangwa kufanyika siku mbili mjini Morogoro na Dar es Salaam.

"Tamasha litaanzia mjini Morogoro na baadaye jijini ambalo litakuwa ni la kifamilia zaidi. Tamasha litaanza mchana na linatarajiwa kumalizika mapema" walieleza.

Shoo ya mjini Morogoro itafanyika katika uwanja wa Jamhuri Stadium na kwamba shoo itaanza jioni ikiwahusisha watu zaidi ya miaka 18, huku ikiwahusisha pia baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.

Cabo Snoop ambaye amejizolea umaarufu mkubwa Afrika na nje ya Afrika kwa sasa, ana albamu yenye nyimbo 14 zenye mahadhi ya Kuduro. Baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na  “Pracatatumba”, “Vamos lá”, “Slow motion”, “Windeck”, “Walalipo” na “Zangala Guduma” .


No comments:

Post a Comment