Pages
▼
Thursday, October 6, 2011
Ferguson awataka wachezaji wake kujiandaa kwa City
MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amewathadhalisha wachezaji wake kuwa katika kiwango cha juu watakapowakaribisha mahasimu wao Manchester City kwenye mchezo utakaowakutanisha vinara hao wa ligi hapo Oktoba 23.
Mabingwa United na City zinafungana kwa pointi, na United inaongoza kwa tofauti ya bao moja tu.Kocha huyo mwenye miaka 69, ambaye amewaita majirani zao hao kuwa 'wapinga kelele', alisema hakushangazwa na City walivyoanza msimu kwa kishindo.
"Nilishasema kabla kwamba hili litatokea," Ferguson aliliambia gazeti la klabu hiyo Jumanne iliyopita."Wanatimu nzuri ya kuwafanya kuendelea kubaki kwenye nafasi ya juu.
"Sergio Aguero amekuwa na mafanikio tangu alipotua katika Ligi Kuu, kwa sababu anauwezo mkubwa wa kufunga na ni mchezaji hatari kwenye eneo la penalti. Pia, David Silva ni mchezaji mzuri.
"Tunachotakiwa ni kuhakikisha tunakuwa tayari kwa ajili ya City wakati tutakapokutana nao."
Timu zote United na City hawajapoteza pointi katika Ligi Kuu msimu huu, wakiwa na rekodi ya kushinda mechi sita na kutoka sare moja, na Ferguson amekiri mechi ya watani wa jadi imebadilika tangu alipoingia bilionea Sheikh Mansour wa Abu Dhabi.
"Mechi zote za mahasimu ni kubwa sasa, hakuna mchezo rahisi," alisema Ferguson."City sasa ni timu kubwa, imefanya usajili wa nyota bora na ukiongeza fedha zao za kuvutia wachezaji wengi bora duniani hiyo ndiyo iliyobadilisha mechi hii hivi sasa.
"Kupata pointi si kitu muhimu sana katika mchezo, lakini jinsi Manchester City walivyoweza kubadilisha soka na ndicho tunachotakiwa kushindana kwa hilo."
No comments:
Post a Comment