Historia ya Gaddafi
Kanali
Muammar Gaddafi ni kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani
Afrika na katika nchi za Kiarabu.
Gaddafi Ameongoza
Libya tangu alipompindua Mfalme Idris I, katika mapinduzi yasiyo ya kumwaga
damu, wakati huo akiwa na umri wa miaka 27.
Maarufu
kwa nguo anazopenda kuvaa, na walinzi wa kike wenye kubeba silaha, kiongozi
huyo wa Libya pia anadhaniwa kuwa na mbinu nzuri za kisiasa, kwa kuweza
kuirejesha Libya kutokana na kutengwa kidiplomasia duniani.
Baada
ya miongo miwili ya kutengwa katika jamii ya kimataifa, mwaka 2003, Tripoli
ilikiri kuwa walifanya shambulio la Lockerbie kwa kuiangamiza kwa mabomu ndege
ya Pam Am na hapo Umoja wa Mataifa ukaondoa vikwazo dhidi ya Libya.
Baada
ya miezi kadhaa, serikali ya Kanali Gaddafi ilisitisha mipango yake ya kuunda
silaha za maangamizi na hii ikarejesha ushirikiano na nchi za magharibi.
Hapo
ndipo mabadiliko halisi yalionekana kwa kuwa nchi hizo za magharibi zilibadili
mtazamo wao na kuacha kumtenga Gaddafi na kushirikiana naye hata kama alikuwa
hatabiriki.
Ni
mtu wa kipekee katika kauli zake, mienendo yake, tabia zake na mikakati yake,
kwa mujibu wa Saas Djebbar mtaalam wa siasa za Libya.
'Lakini
ni mwanasiasa mashuhuri; hakuna shaka lolote kuhusu hilo. Ni mwanasiasa
anayeweza kuhimili misukosuko ya kisiasa kwa hali ya juu sana.'
Asili
ya Mabedui
Muammar
Gaddafi alizaliwa jangwani karibu na Sirte mwaka 1942.
Alipokuwa
kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri na, Gamal Abdel Nasser,
alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa
Suez mwaka 1956.
Gaddafi
alipanga njama ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi
na aliwahi kupata mafunzo zaidi akiwa Uingereza kabla ya kurejea nyumbani
Libya, mji wa Benghazi, na kupanga mapinduzi ya tarehe 1 Septemba mwaka wa
1969.
Ghaddafi
alianza kujenga itikadi zake za kisiasa mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu
chake cha kijani kibichi.
Alikitumia
kitabu chake kuanzisha mfumo wa kisiasa iliyojumuisha kanuni za kiislamu na
mfumo uliyo tofauti na siasa za ujamaa au ubepari.
Mwaka1977
aliasisi mfumo ujulikanao kama 'Jamahiriya' au 'Taifa la Umma' ambapo raia ndio
wanaoendesha uongozi wa nchi yao kupitia 'kamati za umma'.
Mfumo
huo wa Gaddafi umevuka mipaka na hauhusishi mambo ya siasa tu, bali pia mambo
mengine.
Akiwa
safarini ng'ambo, huwa anakaa kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari
ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa
hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume.
Hema
hiyo pia hutumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano
na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.
Upekepeke
Benjamin
Barber, mtaalam wa kisiasa wa kujitegemea, kutoka Marekani amewahi kukutana na
Gaddafi mara kadhaa hivi karibuni na kuzungumza naye kuhusu mustakabali wa
Libya
Bw
Barber alisema kuwa Muammar Gaddafi anajihisi kuwa msomi aliyebobea.
Muammar
Gaddafi na Tony Blair waliwahi kuandaa mkutano wa viongozi kutoka nchi
mbalimbali tarehe 29 Mei 2007 kwenye hema hiyo ya Kibedui.
"Utashangazwa
kuwa ingawaje ni dikteta, ni mwanafalasafa na mwenye kutafakari jambo kabla ya
kuzungumza," aliiambia BBC.
"Namchukulia
sana kama mtu kutoka kabila la Waberber na mtu ambaye aliibuka kutoka tamaduni
za watu wa jangwani, kutoka kwenye mchanga na kwa namna fulani kuna tofauti
kubwa na uongozi wa kisasa, na kwa namna fulani hilo limemfanay awe
mstahamilivu na mwenye msimamo."
Kanali
Gaddafi amejitahidi kwa muda mrefu kutoa ushawishi wake nyumbani na ng'ambo.
Awali
alituma jeshi lake nchini Chad ambapo wanajeshi walidhibiti ukanda wa Aozou,
kaskazini mwa nchi hiyo, mwaka 1973.
Katika
miaka ya 80 aliandaa mafunzo kwa makundi ya waasi kutoka Afrika Magharibi
yaliyojumuisha wale wa Tuareg ambao ni Waberber.
Hivi
karibuni aliongoza jitihada za kuwapatanisha waasi wa Tuareg kutoka nchi za
Niger na Mali.
'Mbwa
kichaa'
Jumuiya
ya wanadiplomasia kuitenga Libya kulitokana na Kanali Muammar Gaddafi kuunga
mkono makundi yeneye silaha, ikiwemo Irish Republican Army na Palestine Liberation
Organisation
Rais
wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alimwita Gaddafi 'mad dog' yaani 'mbwa
kichaa' na Marekani ililipiza kisasi dhidi ya Libya kwa madai ya kuhusika na
mashambulio ya anga barani Ulaya kwa kuvamia miji ya Tripoli na Benghazi mwaka
1986.
Ilisemekana
kuwa Kanali Gaddafi alitikiswa na mashambulio ya mabomu hayo ambapo mtoto wake
wa kike wa kufikia aliuawa.
Aliposhindwa
katika jitihada zake za kuzipatanisha nchi za Uarabuni katika miaka ya 90,
Kanali Gaddafi alielekeza nguvu zake barani Afrika na kupendekeza 'Muungano wa
Nchi' za bara la Afrika.
Alianza
kuvaa mavazi yake binafsi, sare za michezo zilizo na ngao za bara la Afrika au
picha za viongozi kutoka bara hilo.
Wakati
wa mabadiliko katika karne ya 20, huku Libya ikiwa inapata tabu kutokana na
vikwazo dhidi ya nchi hiyo, alianza kurekebisha hali nchini mwake.
Mwaka
wa 2003, mabadiliko yakaanza kuonekana na baada ya miaka mitano mkataba wa
kulipa fidia kwa waathirika wa Lockerbire uliafikiwa na hii ikarejesha uhusiano
kati ya Washington na Libya.
'Hakutakuwa
na vita tena, mashambulio, na vitendo vya ugaidi' Kanali Gaddafi alisema
alipokuwa akiiherehekea miaka 39 aliyokaa madarakani.
Changamoto
za ndani
Kiongozi huyo wa Libya hujiona kama kiongozi wa kidini wa taifa hilo, akihakikisha kwa kile anachosema ni demokrasia.
Wanaompinga
wamekandamizwa kikatili na vyombo vya habari vinabaki katika udhibiti mkubwa wa
serikali.
Libya
ina sheria ambazo haziwaruhusi watu kukusanyika katika misingi ya kisiasa
zinazopinga mapinduzi ya Kanali Gaddafi.
Shirika
la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema serikali hiyo
imewatia mbaroni mamia ya raia kwa kukiuka sheria hiyo na baadhi yao kuhukumiwa
kifo.
Imeripotiwa
kumekuwa na matukio ya utesaji na hata watu kupotea
Inadhaniwa
kuwa Kanali Gaddafi anaandaa namna ya kukabidhi madaraka yake kwasababu ya umri
aliyofikia sasa lakini haijulikani ni nani atakayerithi uongozi wa Libya kutoka
kwa Gaddafi.
Kuna
hisia kuwa mwanawe Sayf Al-Islam Gaddafi ndiye atarithi uongozi kutoka kwa baba
yake na anaongoza katika kuleta mabadiliko.
Ingawaje
Sayf ametangaza kuwa anastaafu siasa lakini kuna wanaohisi kuwa hii ni mbinu ya
kuongeza ushawishi wake kisiasa.
Wakati
huo huo, Gaddafi ameahidi kuwa wizara za nchi hiyo zitafutwa pamoja na bajeti
zao
Utajiri
utakaopatikana kutokana na mafuta utakabidhiwa moja kwa moja kwa wananchi.
Licha
ya uchumi wa Libya kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje, mabadiliko bado
yanakwenda taratibu.
Walibya
wengi wana wasiwasi juu ya mabadiliko yanayotokea na kuhisi kuwa hawapati
manufaa kutoka rasilmali ya Libya, waangalizi wanasema kwani huduma za serikali
ni duni pamoja na ubadhirifu mkubwa wa mali.
'
Wanajihadhari sana katika mapambano hayo kwa kuwa hawataki mabadiliko
yatakayolegeza nguvu za umma,' alisema Saad Djebbar
'Lakini
wakati huo huo, Walibya wanafahamu kuwa wanahitaji kufanya mabadilko. Na ndio
maana wanaenda taratibu sana.
No comments:
Post a Comment