Mazishi ya kanali Muammar Gaddafi, mwanae Mutassim na waziri wa ulinzi yamefanyika katika sehemu ya siri leo alfajiri.
Msemaji mmoja wa baraza la kitaifa la mpito (NTC) ameiambia BBC kuwa miili ya watu hao watatu imezikwa baada ya utata kuhusu pale watakapo zikwa.
Taarifa zingine zinamnukuu msemaji wa NTC Ibrahim Beitalmal akisema jamaa wachache wa familia ya Gaddafi walishiriki katika mazishi hayo na dua zilisomwa kulingana na utaratibu wa Kiislamu.
Baadhi ya watu mjini Misrata wanasema miili ya watu hao watatu iliondolewa usiku kutoka sehemu ilipohifadhiwa katika harakati za kupanga mazishi hay
No comments:
Post a Comment