Pages

Monday, October 24, 2011

MCHEZAJI WA TANZANIA AOMBEWA ITC YA KUCHEZA NCHINI POLAND

 
Katibu Mkuu wa Chama cha mpira wa miguu Poland PZPN, Zdzislaw Krecina katika picha.
Chama cha Mpira wa Miguu Poland (PZPN) kimetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Khatib Waziri Mzee ili aweze kucheza mpira wa miguu nchini humo.
PZPN imetuma maombi hayo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kumwezesha mchezaji huyo kuichezea timu ya LUKS Wierzbiecice ambayo hata hivyo haikuelezwa iko ligi ya daraja gani nchini humo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa PZPN, Zdzislaw Krecina, Mtanzania huyo aliyezaliwa Julai 30, 1974 ameombewa hati hiyo kama mchezaji wa ridhaa kwa maelezo kuwa hakuwahi kusajiliwa na klabu yoyote nchini.
TFF inafanyia kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya taratibu husika kukamilika.

No comments:

Post a Comment