Pages
▼
Wednesday, October 26, 2011
Ndege mpya ya shirika la Boeing aina ya 7-8-7 Dreamliner, imeanza safari yake ya kwanza kutoka Tokyo hadi Hong Kong.
Ndege hii ilitarajiwa kuanza safari zake miaka mitatu iliopita lakini ilichelewa kutokana shughuli za uundaji.
Licha ya gharama za kutengeneza ndege hiyo kugharimu mabilioni ya dola, Dreamliner imetajwa kuwa hatua kubwa katika miundo ya ndege.
Kwa mujibu wa shirika la Boeing,Dreamliner haitumii mafuta mengi na imetengenezwa kutokana mfumo wa nyaya za carbon na plastiki.
Shirika la ndege la All Nippon Airways la Japan-- likiwa la kwanza kutumia ndege hii limenadi viti sita vya abiria wa kiwango cha juu cha biashara katika safari ya kwanza na kupata dola elfu 34 ambazo linasema zitatumika kama misaada kwa mashirika ya mazingira.
No comments:
Post a Comment