Pages

Tuesday, October 4, 2011

nsajigwa nje taifa stars


Jackson Odoyo na Vicky Kimaro
KOCHA Jan Poulsen amekirili kuumia kwa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa ni pigo kwa kikosi chake kinachojiandaa na mechi dhidi ya Morocco.

Nsajigwa ameondolewaa katika kikosi hicho baada ya jana kuumia nyonga (groin) kwenye mazoezi ya timu hiyo  yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.Kwa mujibu wa daktari wa Taifa Stars, Mwanandi Mwankemwa, maumivu hayo yatamweka Nsajigwa nje ya uwanja wiki mbili hadi nne.

Akizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam Poulsen alisema kuumia kwa Nsajigwa ni pigo kubwa katika timu hiyo kiasi cha kuvuruga malengo lake.“Sio kitu kizuri na si cha kawaida timu kukosa nahodha wake, tena ukizingatia kwamba tunakabiriwa na mechi ngumu mbele yetu,”alisema Poulsen nakuongeza:

“Nsajigwa alikuwa mtu muhimu sana katika timu hii kwa sababu alikuwa na uwezo mkubwa wa kuwaunganisha wachezaji wenzake pamoja na kuwahamasisha, nilikuwa nikiwasiliana naye kwa karibu na kumpa maelekezo ambayo akiwaeleza wenzake wanaelewa kwa umakini zaidi”.

Na kuhusu kumteuwa nahodha mwingine wa timu hiyo alisema bado hajafanya maamuzi hayo kwa sababu sio maamuzi ya kukimbilia bali yanahitaji umakini mkubwa.

Kumteuwa nahodha inahitaji umakini kwa sababu ndiye kiongozi wa timu ndani na nje ya uwanja hivyo nilazima awe mtu mwenye sifa na mwenye uwezo kama alivyokuwa Nsajigwa ingawa wanaweza wasifanane kwa kila kitu, lakini mwenye kujua jukumu lake,”alifafanua Poulsen.

Kocha huyo tayari ameshamwita beki wa kulia wa Simba, Nassoro Masoud Said ‘Cholo kuziba pengo la Nsajigwa.

Akizungumzia suala hilo Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kuwa kutokana na ushauri wa daktari, kocha Poulsen amemuondoa kwenye kikosi hicho na sasa nafasi yake itazibwa na beki wa Simba, Nassoro Cholo.Kocha Poulsen alimuacha unahodha huo Nsajigwa ‘Fusso’ tangu alipochukua mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo mwaka 2010.

Nsajigwa amewahi kuwa nahodha mara kadhaa, lakini kuna wakati aliyekuwa kocha mkuu wa Stars, Maximo aliwahi kuwapa Henry Joseph na baadaye Salum Sued.Nsajigwa ndiye aliyekuwa nahodha wa Stars wakati iliposhiriki michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN) mwaka 2009 nchini Ivory Coast.

Stars itaondoka nchini kesho kutwa Oktoba 6 kuelekea  Casablanca, Morocco kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Oktoba 9.Stars inatakiwa kushinda mabao mawili au zaidi kama inataka kufuzu lakini pia itatakiwa iiombee Jamhuri ya Afrika ya ifungwe na Algeria.
Jamhuri ya Kati na Moroco zina pointi nane wakati Stars na Algeria zina pointi tano.Wakati huohuo; Wambura alisema wachezaji wanaocheza nje ya nchi walioitwa na kocha Poulsen wameanza kuwasili na tayari Idrissa Rajab anayechezea Sofapaka ya Kenya na Mbwana Samata wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili jana jioni.

"Henry Joseph wa Kongsvinger IL ya Norway), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) wanatarajiwa kuwasili leo usiku kwa ndege ya KLM," alisema Wambura.

Alisema kuwa washambuliaji Abdi Kassim na Dan Mrwanda wanaochezea timu ya DT Long An ya Vietnam ndiyo watakaokuwa wa mwisho kujiunga na kambi ya Stars ambapo watawasili nchini kesho saa 7 mchana kwa ndege ya Qatar Airways.kwa hisani ya gazeti la mwanainchi



No comments:

Post a Comment