Pages
▼
Monday, October 17, 2011
SOMA KWA MAKINI NA UMPE MWENZIO
Kijana mmoja aliyekuwa akijiandaa kwa mahafali ya kuhitimu chuo kikuu, kwa
muda mrefu alikuwa akiitamani gari moja ya kifahari ya kimichezo iliyokuwa
ikiuzwa katika duka moja la magari, na akijua dhahiri kuwa baba yake ana
uwezo wa kununua gari hilo na kumpa yeye kama zawadi yake kwa kuhitimu
masomo vyema, na alimwambia baba yake kuwa hicho ni kitu alichokipenda
Mno.
Kadri siku zilivyokuwa zikisogea kuelekea mahafali kijana huyo alisubiri
kwa hamu kuona dalili za baba yake kumnunulia gari hilo . Siku ya siku
ikafika na asubuhi ya siku hiyo ya mahafali, baba yake alimwita kwenye
chumba chake cha kusomea na kumwambia ' Najivunia kuwa na mtoto bora kama
wewe' na pia akamwambia ni kwa kiwango gani anampenda. Akamkabidhi
kijifurushi cha zawadi kilichofungwa vema kwenye karatasi safi za kufungia
zawadi. Akiwa mwenye hamu kubwa lakini akiwa amekatishwa tamaa alifungua
kifurushi hicho na kukuta ni Biblia nzuri yenye jalada la ngozi na juu yake
kumeandikwa jina la kijana huyo kwa maandishi nadhifu yaliyonakshiwa kwa
dhahabu. Kwa hasira akamfokea baba yake akisema ' Yaani pamoja na pesa zako
zote
unanipa biblia?'akatoka hima ndani ya nyumba hiyo na kuiacha
biblia.
Miaka mingi ikapita na kijana akawa ni mtu wa mafanikio sana kibiashara.
Alikuwa na nyumba nzuri na familia bora, lakini akagundua baba yake ni mzee
sana sasa, na akadhani ni muhimu kwenda kwake... Na alikuwa hajawahi kumuona
tena toka siku ile ya Mahafali. Kabla mipango yake haijatimia, akapokea
waraka wa simu ukimtaarifu kuwa baba yake amefariki dunia, na amemrithisha
kila kitu alichokuwa nacho kijana wake wa pekee. Hivyo alitakiwa kurudi
nyumbani haraka kusimamia mali za
babayake.
Alipofika nyumbani kwa baba yake , alipata uchungu na majuto ya hali ya juu
rohoni. Akaanza kupekua baadhi ya nyaraka muhimu za baba yake ndipo!
alipoikuta ile biblia ikiwa vile vile kama alivyoiacha miaka kadhaa nyuma.
Huku akilia alifungua kurasa za biblia. Baba yake kwa umakini mkubwa
alipigia mistari maneno yaliyopo katika Mathayo 7:11, yanayosema ' basi
ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema,je! Si
zaidi sana Baba yenu aliye Mbinguni atawapa mema wao
wamwombao?. Wakati akisoma maneno hayo, funguo za gari zikadondoka kutoka
katika kurasa za mwisho za biblia. Ikiwa na jina pamoja na alama ya
lile duka la kuuza magari ya kifahari ya kimichezo aliyokuwa akiyapenda sana . Kukiwa na tarehe ile ya siku yake ya mahafali huku imeandikwa ...
IMELIPIWA PESA KAMILI.
Mara ngapi tumezikosa baraka za mwenyezi mungu eti kwa sababu hazijafungwa
tutakavyo? Naamini umefurahia hili somo la leo. Peleka ujumbe huu kwa
wengine. Usipoteze ulichonacho kwa kutamani
usichonacho: Lakini kumbuka ulichonacho sasa ni moja kati ya vitu ulivyo
vitamani huko siku za nyuma. IKIWA ZAWADI UPEWAYO HAIJAFUNGWA KWA KADRI
UTAKAVYO, NI KWA SABABU HIVYO NDIVYO HALI BORA KABISA YA UFUNGWAJI WAKE
ULIOPATIKANA! SIKU ZOTE SHUKURU VITU VIDOGO: KWANI HUWA NA VITU VINGINE
NDANI YAKE!
TAFADHALI TUMA UJUMBE HUU KWA WATU WASIOPUNGUA WAWILI ILI KUFANYA UJUMBE
HUU UENEE.
Every blessing!!
No comments:
Post a Comment