Watu wenye silaha wamewateka wafanyakazi watatu wa
kutoa misaada walioajiriwa na kampuni ya Denmark ya Demining Group
kaskazini ya kati ya Somalia.
Shirika hilo la kutoa misaada limesema raia wa Somalia alichukuliwa pamoja na wafanyakazi wengine wawili wa kimataifa- mwanamke wa Kimarekani na mwanamme raia wa Denmark.
Afisa mmoja wa usalama wa Somalia amewaambia waandishi wa habari kuwa walitekwa karibu na uwanja wa ndege kwenye mji wa Galkayo.
Mapema mwezi huu wafanyakazi wawili wa kutoa msaada wa Uhispania walichukuliwa kutoka kambi ya wakimbizi katika mpaka jirani na Kenya.
Tangu Septemba, kumekuwa na wimbi la utekaji nyara wa raia wa kigeni nchini Kenya, ambapo Nairobi imelilaumu kundi la Kisomali la al-Shabab.
Kundi hilo limekana kuhusika na matukio hayo.
Galkayo haiko chini ya udhibiti wa al-Shabab
Mapigano ya kikoo
Mji huo uko kwenye mpaka baina ya mji unaojitawala kaskazini mwa Somalia, Puntland na wilaya nyingine inayodhibitiwa na ukoo wa Galmudug, unaofungamana na serikali ya mpito ya nchi hiyo.
Ahmed Mohamed, afisa polisi huko Galkayo, ameliambia shirika la habari la AP wawili hao walipelekwa kusini mwa mji huo, huko Galmudug.
Waandishi wamesema Puntland ina usalama ukilinganisha na maeneo mengine Somalia, lakini kulikuwa na mapigano ya ukoo huko Galkayo mwezi uliopita.
Wafanyakazi wachache wa kigeni wa kutoa msaada husafiri kwenda Somalia kwa hofu ya kutekwa na wanamgambo wanaodai vikombozi vikubwa ili waachiwe huru
No comments:
Post a Comment