Pages

Wednesday, November 2, 2011

AL-KIB waziri mkuu mpya LIBYA.


Baada ya kuhakikisha mwili wa kiongozi wa zamani wa kiongozi wa libya muammar gadafi umezikwa kusiko julikana na wengi, libya kumeanza kukucha sasa hivi, huku viongozi wa baraza la mpito wakiamini uhuru wa nchi hiyo umepatikana. Stori kamili kutoka libya sasa hivi, zinaamplfy kwamba Wajumbe wa baraza la taifa la mpito la nchi hiyo wamemchagua msomi Abdel Rahim al-Kib kuwa waziri mkuu mpya wa mpito wa nchi hiyo.

DW wamesema Msomi huyo kutoka Tripoli anachukua nafasi iliyoachwa na Mahmoud Jibril, ambaye amesema atajiuzulu muda mfupi tu baada ya Libya itakapotangazwa kuwa imekombolewa kutoka kwenye utawala wa Gaddafi.

 Waziri mkuu mpya anatarajiwa kutangaza baraza lake la mawaziri katika muda wa siku chache zijazo ambapo Baraza la taifa la mpito , NTC, limeahidi kukabidhi madaraka kwa bunge lililochanguliwa katika muda wa miezi nane.

Bunge litakua na nguvu na kazi ya kutengeneza katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa vyama vingi , ambao unatarajiwa kufanyika mwaka 2013. Hiyo ni hatua muhimu na sherehe kwa nchi zote zilizoshiriki kwenye vita ya kumuondoa gadafi ikiwemo marekani, ambayo inasema mwisho mbaya wa gadafi ni mfano mzuri kwa madikteta wengine duniani.

No comments:

Post a Comment