Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 6, 2011

ARUSHA TECHNICAL COLLEGE YA SAINI MAKUBALIANO YA USHIRIANO (MoU) NA TAASISI YA PUM YA NCHINI UHOLAZI

ARUSHA TECHNICAL COLLEGE YA SAINI MAKUBALIANO YA USHIRIANO (MoU) NA TAASISI YA PUM YA NCHINI UHOLAZI

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Richard Masika akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano ya Ushirikano (MoU) ya Taasisi ya PUM ya nchini Uholazi
Baadi ya Wadau wa Mradi wa PUM katika Picha ya Pamoja
Na: Gasto Leseiyo
Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kimesaini Makubaliano ya Ushirikano (MoU) na Taasisi ya PUM ya chini Uholazi kwa lengo la kuongeza ujuzi kwa wakufunzi wanaofundisha programu za Uhandisi Umeme pamoja na Uhandisi Elekroniki na Mawasiliano Anga
Katika makubaliano hayo, Taasisi ya PUM itaisaidia ATC itatoa Wataalamu mbalimbali katika fani za Umeme na Electroniki na Mawasiliano Anga ili kujenga Ujuzi na Umahiri kwa Wakufunzi wa ATC.
Awali akizungumza mara baada ya kusaini Makubaliano ya Ushirikano, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusdha, Mhandisi. Dkt. Richard Masika alisema kuwa, kwa sasa ujuzi na umahiri unaohitajika katika viwanda vingi nchini hauendani na kile Wahitimu nwengi wa fani za ufundi wanakitoa hali iliyopekea kushirikiana na Taasisi ya PUM ya nchini Uholazi kwa lengo la kuongeza na kujenga Ujuzi na Umahari kwenye mafunzo kwa vitendo.
Aliendelea kusema kuwa, mradi huu wa PUM sio tu tutasaidia kuongeza Ujuzi zaidi kwa Wakufunzi bali pia kusaidia kujenga ushiriano na viwanda na Taasisi mbalimbali hapa nchini zinazoajiri wahitimu chuo cha Ufundi Arusha.
“Mradi huo wa PUM na Chuo cha Ufundi Arusha umelenga kuunda Mtahala na vyenzo mbalimbali za kufundishia pamoja na kutambua vifaa mbalimbali vya kufundishia vinayohitajika katika kwenye mafunzo ya vitendo. Pia umelenga kuongeza ushirikano na viwanda, Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Chuo chetu cha Ufundi Arusha ” alisema Dkt. Masika
Awalia akizungumza wa Wadau mbalimbali wa Ufundi Chuoni hapao, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya PUM, Bw. Thijs Van Praag alitoa changamoto kwa uongozi wa Chuo, kufanya utafiti kwa wahitimu wote wanaomaliza Chuoni hapo wanachukua muda kiasi hadi kupata ajira au kujiajiri wenyewe katika fani walizosemea.
“Kama wanafunzi inawachukua miezi sita au mwaka moja kupata ajira au kujiari, hii inamanisha kuwa kile kinachofundishwa akiendani na mahitaji ya soko na kama hivyo ndivyo, itakuwa ni jambo la busara kuangalia tena mitahala inayotumika na kuakikisha kuwa progaramu zinazofundishwa zina msaidia mwanafunzi na jamii kwa ujumla” alisema Bw. Praag

No comments:

Post a Comment