Pages

Monday, November 7, 2011

Boateng ajiuzulu kuchezea Black Stars

Kiungo wa timu ya taifa ya Ghana Kevin-Prince Boateng ametangaza kujiuzulu kuichezea timu hiyo.
Kevin - Prince Boateng ajiengua timu ya taifa ya Ghana
Kevin - Prince Boateng ajiengua timu ya taifa ya Ghana
Boateng mwenye umri wa miaka 24 aliyewahi kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani chini ya umri wa miaka 19, alibadilisha utaifa mwaka jana ili aweze kuichezea Black Stars.
Kiungo huyo anayechezea klabu ya AC Milan, ameshaichezea Ghana kwa miezi 18, amesema kuumia mara kwa mara ndio sababu ya kuchukua uamuzi wake.
Taarifa ya Chama cha Soka cha Ghana imesema: "Chama cha soka cha Ghana kimepokea barua kutoka kwa Kevin-Prince Boateng kutokana na uamuzi wake wa kujiuzulu kuichezea Black Stars."
"Kwa mujibu wa Kevin, kutakiwa kucheza kwa kiwango cha juu katika klabu na nchi kimesumbua afya yake.
"Mchezaji huyo pia ameeleza ili aendelee kubakia mwenye afya njema na kuepuka kuumia mara kwa mara, ameshauriana na madaktari pamoja na familia yake juu ya suala hilo na ameamua kuchukua uamuzi wa kujiondoa katika timu ya taifa kwa vile yupo kwenye mazoezi maalum na kwa maana hiyo hawezi kuvuruga utaratibu huo wa mazoezi.
"Hadi sasa chama cha soka cha Ghana hakijasema lolote kuhusiana na uamuzi huo wa Kevin-Prince Boateng."
Boateng ameshacheza mechi nane akiwa na timu ya taifa ya Ghana na alifunga bao moja wakati Ghana ilipoilaza Marekani mabao 2-1 mwaka jana nchini Afrika Kusini katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Kombe la Dunia.
Taarifa hizo zimeistua Black Stars, ambayo ina nia kubwa ya kutaka kunyakua Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon na Equatorial Guinea mwezi wa Januari.
Msimu huu kiungo huyo kiwango chake kimepanda katika klabu yake ya Italia, akiwa amefunga mabao matatu peke yake dhidi ya Lecce mwezi uliopita katika mchezo wa ligi.
Lakini uamuzi huo hauisumbui sana Ghana katika nafasi ya kiungo wakiwa na vijana Emmanuel Agyemang Badu, Kwadwo Asamoah, Andre Ayew pia wakongwe Michael Essien na Sulley Muntari bado wanahitajika katika timu ya taifa.

No comments:

Post a Comment