Pages

Wednesday, November 16, 2011

CHAD WALIPOANGUA KILIO UWANJA WA TAIFA JANA


Kocha wa timu ya taifa ya Chad akinawa uso na msaidizi wake mara baada ya kuangua kilio vya kutosha kwenye uwanja wa taifa jana, baada ya timu yake kutolewa na Taifa Stars katika kinyang'anyiro cha kufuzu kombe la dunia litakalofanyika nchini Brazil mwaka 2014
Mmoja wa maafisa wa benchi la ufundi wa timu ya Chad akifuta machozi baada ya kushuhudia kocha wake aliyekaa kwenye benchi asijue la kufanya akilia kwenye uwanja wa taifa jana jioni, timu ya Chad ilitolewa na Taifa Stars katika kuwania kushiriki kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.
Golikipa pia alishindwa kujizuia na kumwaga kidogo chozi kama anavyoonekana akijifuta huku akitoka uwanjani.
Mmoja wa wachezaji wa akiba wa timu ya Chad akimsaidia kumtoa nje ya uwanja golikipa wa timu hiyo Brice Mabaya baada ya mpira kuisha.
Mashabiki wa Taifa Stars wakishangilia mara baada ya timu yao kusonga mbele katika hatua ya makundi baada ya kufuzu katika mchezo huo kwa sheria ya goli la ugenini , Taifa Stars ilifungwa goli 1-0 na Chad hata hivyo Chad iliaga mashindano.

No comments:

Post a Comment