Pages

Thursday, November 3, 2011

FERGUSON: Rio Ferdinand sio tena chaguo langu


Kocha wa manchester united alex ferguson, amesema mchezaji rio Ferdinand mwenye umri wa miaka 32, sio tena chaguo lake la kwanza ktk mabeki wa man u, kwa sababu amepoteza ubora aliokua nao, amepoteza spidi alizokua nazo mwanzoni.

Ferguson ameamplfy kwamba kuna mabeki wengi wenye umri mdogo lakini wana uwezo mkubwa kama chriss smalling na phil jones ambapo anaamini kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Ferdinand kwenda kucheza ligi ya marekani kama beckam au kwenda tottenham.

mchezaji Rio Ferdinand wa MAN U, ambae toka ajiunge nayo 2002 ameifungia magoli 6 tu na ameifungia timu ya taifa ya England magoli matatu tu toka ajiunge nayo 1996.

Hata hivyo chanzo kimoja cha habari, kimesema rio Ferdinand atabaki machester ingawa kuna stori za chini kwamba anataka kuihama man u miezi miwili ijayo, ili kukwepa kuwekwa benchi japo mkataba wake umebakiza miaka miwili.

Hata hivyo imefahamika kwamba RIO hafikirii kujiunga na spurs, mawazo yake makubwa ni kufanya mazoezi zaidi ili spidi ya zamani irudi aendelee kuwepo man united.

Ferguson amesisitiza kwamba mchezaji yoyote akifika umri wa miaka 32, spidi inapungua, na hapo ndio anatakiwa kubadilisha stile ya kucheza, kwa sababu hawezi kucheza na spidi aliyokua nayo miaka miwili, mitatu au mitano iliyopita kama ilivyo kwa ferdinand.

Ferguson amesema hata yeye alipotimiza umri wa miaka 32 akiwa mchezaji, aligundua mabadiliko kwenye kiwango chake, ikabidi abadili mara moja aina ya game alilokua anacheza.

No comments:

Post a Comment