Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 9, 2011

HOTNEWS.....KAKA MTU AMCHINJA MDOGO WAKE BAADA YA KUMWAMBIA HAJUI KUSOMA

HOTNEWS.....KAKA MTU AMCHINJA MDOGO WAKE BAADA YA KUMWAMBIA HAJUI KUSOMA

IGP MWEMA

Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti likiwemo la kaka amkata kichwa mdogo wake wakati akichimba viazi,ambapo tukio lingine rafiki amchoma mwenzie na kisu baada ya kumwambia hajui kusoma huko wilayani sumbawanga katika mkoa wa Rukwa.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka mkoani Rukwa Elizabeth Ntambala anaripoti kuwa ,Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoani Rukwa Isuto Mantage, alisema kuwa matukio yote haya yametokea hivi karibuni wakati tukio la kwanza lilitokea huko kijiji cha kampala kata ya mkowe katika tarafa ya matai iliyohusisha leonard chipatu(5)kukatwa kichwa kwa bahati mbaya na kaka yake.

Kamanda Mantage alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi jioni wakati watoto hao wawili wakiwa shambani wakichimba viazi,ambapo mkubwa alikuwa ameshika jembe akichimba viazi wakati mdogo wake akimsaidia kuokota viazi na ndipo jembe lilimfikia mdogo kwa bahati mbaya na kumkata kichwani ambapo alianza kuvuja damu kwa wingi na kufariki dunia muda mfupi.

Inadaiwa kuwa wakati akiwa anapatiwa huduma ya kwanza akiwa hospitalini ndipo alifariki dunia kwani alikuwa amepata maumivu makali baada ya kukaa kwa muda huko shambani na kukosa msaada wa karibu hadi pale kaka mtu alipoanza kupiga kelele za kuomba msaada na kuwafanya wapiti njia kwenda kumuokota akiwa anagalagala chini hakiwa hajiwezi kwa lolote.

Katika tukio jingine lililotokea katika kijiji cha mfinga huko kwenye ukanda wa ziwa Rukwa(Didas Kayanda(18) mkazi wa hikijiji hicho alifariki dunia baada ya kuchomwa na kisu kifuani.

Awali vijana hao ambao walikuwa ni marafiki walikuwa wakisaidiana kuchimba kisima cha maji kwa matumizi ya ng’ombe ambapo walianza kutaniana.
Inadaiwa kuwa wakati marafiki hao wakiendelea kutaniana ndipo Didas alimtania Machia Honoli kuwa hajui kusoma wala kuandia,alikasirika na kuchukua kisu,kisha kumchoma mwenzake shingoni ambaye alidondoka chini na kufariki dunia palepale.

Mtuhumiwa alitoroka baad ya tukio mpaka hivi leo bado anatafutwa na jeshi la polisi ili atakapo patikana aje ajibu tuhuma zinazomkabili.

No comments:

Post a Comment