Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 2, 2011

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KUDHAMINI MASHINDANO YA KOMBE LA CECAFA TUSKER CHALLENGE KWA 823/- MILIONI.

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KUDHAMINI MASHINDANO YA KOMBE LA CECAFA TUSKER CHALLENGE KWA 823/- MILIONI.



Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki (CECAFA) Nicolas Musonye (kulia), akipokea mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 823 kutoka kwa Richard Wells Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam asubuhi hii, katikati ni Jaji Mark Bomani Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa (CECAFA) wakati alipotangaza udhamini wa shilingi milioni 823 kwa ajili ya mashindano ya Tusker Challenge Cup 2011 yatakayofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni, wanaofuatia katika picha ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) na Ritah Mchaki Meneja wa kinywaji cha Tusker.
Katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya mpira wa Miguu Afrika Mashariki Nicholas Musonye akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya New Afrika wakati alipokuwa akitangaza kufanyika kwa mashindano hayo Tusker Challenge Cup 2011 yakiambatana na Maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, wanaofuati ni Leodger Tenga Mwenyekiti wa CECAFA na Rais wa TFF, Jaji Mark Bomani Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Richard Wells Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) na Ritah Mchaki Meneja wa kinywaji cha Tusker.
Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries limited (SBL), kampuni inanyokua kwa kasi hapa nchini, kupitia bia yake ya Tusker, leo wametangaza udhamini kwa mashindano ya kombe CECAFA Tusker Challenge mwaka huu.
Udhamini huu ni wa kiasi cha fedha za kitanzania shillingi milioni 823. Fedha hizi zitagharamia mahitaji kama vile: tiketi za ndege kwa msafara wote wa CECAFA pamoja na wahusika wakuu wa CECAFA, malazi, usafiri wa magari hapa nchini, watoa huduma, fedha za washindi, malipo ya CECAFA ndani na nje ya nchi. Kodi ya uwanja wa mpira, ulinzi na sehemu za mazoezi kwa wachezaji. Hali kadhalika, fedha hizi zitatumika kuratibu waandishi wa habari na mahitaji mengine ya utawala. Mashindano haya yanategemewa kuanza tarehe 25 Ocktoba hadi tarehe 10 Disemba 2011.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhiana hundi ya udhamini huo, iliyofanyika jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa SBL Bw. Richard Wells, alisisitiza kwamba hii ni mojawapo ya malengo yaliyowekwa na kampuni hiyo yakiwa na nia ya kukuza nakuendeleza mchezo huu nchini. Vile vile kukuza na kuinua vipaji vilivyopo mashariki na magharibi mwa Afrika. Udhamani huu unadhihirisha msimamo wa SBL kuwa kampuni inayowajibika kwa jamii inayoizunguka nchini na nchi jirani za kiafrika.
‘Tunatengeneza Tusker nchini Tanzania sasa, na kinywaji hiki kinapatikana katika eneo zima la Afrika Mashariki. Tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa CECAFA na tunashukuru kupewa heshima hii na CECAFA pamoja na TFF’. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa kampuni ya bia ya Serengeti kudhamini mashindano haya. Mwaka jana, ilitumia kiasi cha shilingi milioni 675, ambapo timu ya Taifa, Tanzania bara Kilimanjaro stars iliubuka mshindi.

No comments:

Post a Comment