Pages

Wednesday, November 9, 2011

Kura zaanza kuhesabiwa Liberia


Kura zimeanza kuhesabiwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Liberia.
Idadi ya wapigaji kura waliojitokeza ilikuwa ndogo sana, huku baadhi ya makadirio yakidokeza kuwa waliopiga kura walikuwa chini ya asilimia 25.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema baadhi ya raia hawakupiga kura wakihofia kuzuka kwa vurugu, wakati wengine waliitikia wito wa upinzani wa kususia uchaguzi huo.
Mwandishi wa BBC katika mji mkuu, Monrovia, amesema kwamba katika kituo kimoja cha kupigia kura mjini humo, watu wanane pekee ndio waliojitokeza kupiga kura ikilinganishwa na mamia waliojitokeza mwezi uliopita, katika duru ya kwanza.
Mgombea wa upinzani, Winston Tubman, ambaye anawania kiti cha rais dhidi ya rais wa sasa Ellen Johnson- Sirleaf, amesema kwamba wafuasi wake watapinga matokeo yoyote yatakayo mpa ushindi rais Johnson-Sirleaf kuongoza muhula wa pili.

No comments:

Post a Comment