Libya yawaachilia wafungwa

Nchini Libya mamia ya wafungwa wanaachiliwa huru kabla ya sikukuu ya Eid al-Adha, hapo kesho.
Serikali ya mpito ya Libya imekubali kuwafungua watu wanaoshukiwa walipigana upande wa Gaddafi.
Lakini
wakuu wamekiri kuwa wale wanaoshukiwa kuwa ni askari mamluki wa kigeni
bado wamebakizwa kizuizini ili wafikishwe mahakamani.
Mamia
ya wafungwa mjini Misrata, Tripoli na miji mengine wamekuwa
wakiachiliwa katika juma hili, ili kuadhimisha sikukuu ya mwanzo tangu
Libya kutangazwa kuwa imeshakombolewa mwisho wa mwezi Septemba.
Jamaa
wa wafungwa walikusanyika nje ya gereza ya Misrata, huku wakilia kwa
furaha, na kuwapa mkono walinzi wa jela waliokuwa wamewafunga.
Wengi wao walitekwa katika mapambano ya mwisho ya kukomboa eneo karibu na mji wa Sirte kutoka wafuasi wa Muammar Gaddafi.
Walishutumiwa kuwa walipigana au kuwapa hifadhi wanajeshi wa Gaddafi.
Wakuu
wa gereza la Misrata waliiambia BBC, kwamba askari wa kukodiwa
hawakufunguliwa...hao ni Waafrika, raia kutoka nchi kama Chad, Mali na
Niger.
Hakuna
dalili kuwa wataachiliwa huru karibuni; jambo ambalo linatia wasiwasi
mashirika ya kimataifa ya kupigania haki za kibinaadamu.
No comments:
Post a Comment