Mahakama ya Hakimu Mkazi yatupilia mbali pingamizi la kuvuliwa uanachama.
Na Gladness Mushi, Arusha.
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi wa Arusha imetupilia mbali mashtaka na pingamizi
lililofunguliwa mahakamani hapo na aliyekuwa diwani viti maalumu kupitia
Chama cha TLP, Mwahija Choga dhidi ya uongozi wa chama hicho kuhusiana na kufukuzwa kwake uanachama pamoja na kutoa maamuzi ya kumvua uanachama na kusimamishwa udiwani.
Mahakama
ilitupilia mbali mashtaka hayo , jana baada ya upande wa washtakiwa
waliokuwa wakitetewa na Wakili Westgate Lumambo kujitosheleza katika
maelezo yake na hivyo mahakama kuridhia kutupilia mbali.
Akisoma
hukumu hiyo ,mahakamani hapo, Hakimu Mkazi wa Arusha,Anold Telekiano
alisema kuwa, mlalamikaji ambaye aliwafungulia mashtaka uongozi huo
mnamo June 23 ,2011 yenye namba 14/2011 pamoja na pingamizi namba 38
zote zikipinga yeye kufukuzwa uachama wa chama hicho kutoaka na kukiuka
sheria za chama hicho.
Hata
hivyo Hakimu huyo aliridhia maelezo yaliyotolewa na Wakili anayewatetea
washtakiwa, yaliyokuwa yakiwema kuwa, mlalamikaji kisheria haruhusiwa
kuwashatakiwa washatakiwa kwa vyeo vyao hivyo alivyofanya yeye nu
kinyume cha sheria.
Ambapo katika kesi hiyo namba 38 aliyoiwakilisha mahakamani ilikuwa
na pingamizi kuwa, uongozi wa chama hicho haurusiwi kumtangaza popote
hadi mahakama itakapotoa hukumu yake , huku akiwakilisha barua ya kufukuzwa uanachama kuwa ni batili .
Hata
hivyo katika mapingamizi hayo,yote mahakama ilitoa maamuzi ya kutupilia
mbalimbali mashtaka hayo kutokana na kuwa hayakukithi na yalikuwa na
mapungufu hivyo kumwamuru mshtakiwa huyo kusimamishwa uanachama ,pamoja
na kuondolewa katika nafasi ya udiwani wa viti maalumu pamoja na ukatibu
wa wilaya wa chama hicho.
Washtakiwa
waliofunguliwa mashtaka mahakamani hapo, ni Leonard Makanzo-Mwenyekiti
wa TLP mkoa, Mwamvua Wahanza –Katibu wa Tlp Mkoa, Mohamed Mahabadi
–Katibu Mwenezi Mkoa, Jacob Molle- Mjumbe kamati ya utendaji mkoa,
Salama Jumanne –Katibu wa wilaya Arusha, na Mjumbe wa kamati ya utendaji
mkoa –Deodatus Humay , na Mwenyekiti wa TLP Taifa , Augostino Mrema.
Hata hivyo,baada ya Diwani huyo kufukuzwa uanachama aliendelea kufanya shughuli za maendeleo na kuhudhuria vikao mbalimbali vya kichama ikiwemo baraza la madiwani pamoja na kuwa alikuwa tayari alishafukuzwa uachama na udiwani .
Ambapo
baada ya uchaguzi kumalizika , wajumbe walifanya vikao na kumchagua
Diwani Viti maalumu kuwa ni Mwamvua Wahanza lakini cha kushangaza jina
la diwani Mwahija Choga likapitishwa na kuwa diwani pamoja na kuwa
hakuchanguliwa na wajumbe .
Kutokana
na hali hiyo ilizua mtafaruku mkubwa sana , huku wakihoji chanzo cha
yeye kuwa diwani wakati aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo kisheria ni
Mwamvua Wahanza , na kila alipokuwa akihojiwa alikuwa akijibu mkato , hali iliyopelekea kupelekena mahakamani ili kutafuta haki .
Baada
ya kutolewa kwa hukumu hiyo, baadhi ya wanachama wa chama hicho akiwemo
Mwenyekiti wa TLP mkoani hapa, Leonard Makanzo alisema kuwa amelipokea
jambo hilo
kwa furaha sana kwani lilikuwa likiwapa wakati mgumu sana , kwani
wajumbe waliomchagua Mwamvua Wahanza walishangazwa sana na kitendo hicho
cha kupewa udiwani Choga.
‘Kwa
kweli nashukuru sana jambo hili limeisha salama na kisheria zaidi
hivyop tunapenda umma na wanachama wetu wajue kuwa, diwani halali ni
Mwamvua Wahanza na hatumtambui tena Choga kwani sio mwanachana wetu tena
wala diwani na popote atakapokuwa akitumia chama chetu atachukuliwa hatua kali za kisheria’alisema Makanzo.
Diwani
wa chama hicho kata ya Sokon 1, Marko Kivuyo alisema kuwa Mkurugenzi wa
manispaa ya Arusha, Estomih Changa’h anapaswa kutambua kuwa, Diwani
aliyepitishwa rasmi na chama hicho nia Mwamvua Wahanza na sio Choga,
hivyo haruhusiwi kuhudhuria vikao vyovyote katika halmashauri hiyo na
watamwandikia barua ya kumtambulisha diwani huyo.
No comments:
Post a Comment