Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 6, 2011

Mfanyabiashara Abri atoa msaada kwa jeshi la polisi Mufindi

Mfanyabiashara Abri atoa msaada kwa jeshi la polisi Mufindi

Mfanyabiashara maarufu mkoani Iringa Bader Saleh Abri akimkabidhi msaada wa pikipiki mkuu wa polisi wilaya ya Mufindi.
Na Francis Godwin,Iringa
MFANYABIASHARA mjini Iringa Bader Saleh Abri ajitolewa msaada wa pikipiki moja kwa ajili ya kulisaidia jeshi la polisi wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ili kuzidi kuendeleza kazi nzuri ya ulinzi .
Akikabidhi msaada huo wa pikipiki moja leo kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mufindi (OCD)Peter Kakamba ,Abri alisema kuwa amevutiwa zaidi na utendaji kazi wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa na hivyo kuamua kutoa pongezi zake kwa jeshi hilo kwa kulisaidia kitendea kazi kama njia ya kuhamasisha wafanyabiashara na wananchi wengine kuendelea kuwa jirani na jeshi la polisi.
Abri alisema kuwa pamoja na kazi nzuri inayofanywa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa chini ya kamanda wa polisi Evarist Mangalla na ile inayofanywa Tanzania nzima chini ya mkuu wa polisi nchini (IGP) Said Mwema bado jeshi hilo linapaswa kupewa ushirikiano mkubwa na watanzania wote wenye mapenzi mema na amani ya Taifa hili.
Hata hivyo alisema kuwa bado wafanyabiashara ndani ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa wanapaswa kuendelea kujenga ushirikiano na jeshi la polisi katika maeneo yao huku asisisitiza kuwa misaada ya vitendea kazi kwa jeshi la polisi isilenge maeneo ya mijini pekee bali ielekezwe pia maeneo ya vijijni ambako kuna changamoto kubwa .
Kwa upande wake mkuu wa Polisi wilaya ya Mufindi (OCD) Kakamba akishukuru kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Iringa kwa msaada huo alisema kuwa ,msaada huo ni changamoto kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi .
Alisema kuwa pamoja na kuwa Abri ni mkazi wa Iringa mjini ila ameamua kutoa msaada wake wilaya ya Mufindi na kuwa huo ni mfano kwa wadau wengine kuendelea kuinga mfano wa mfanyabiashara huyo ambaye anatambua maana ya ulinzi na usalama wa Taifa hili na dhana iliyopo ya polisi jamii na ulinzi shirikishi pamoja na kauli mbinu ya jeshi la polisi ya ukamataji bila kushurutisha.

No comments:

Post a Comment