Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, November 11, 2011

Papademos Waziri Mkuu mpya Ugiriki

Papademos Waziri Mkuu mpya Ugiriki

Papademos
Papademos kupambana na janga la madeni
Makamu wa zamani wa rais wa benki ya Ulaya Lucas Papademos ametangazwa kuwa waziri mkuu mpya wa Ugiriki, kufuatia siku kadhaa za majadiliano.
Taarifa ya kuthibitishwa kwa nafasi ya Bw Papademos imetoka katika ofisi ya rais wa Ugiriki.
Viongozi wa vyama vikuu vitatu vinavyounda serikali ya umoja wa kitaifa wamekuwa wakikutana na rais waUgiriki kujaribu kufikia makubaliano.
Waandishi wa habari wanasema Wagiriki watakuwa na imani kuwa taarifa hizi zitaleta utengamano kuwasiadia kukabiliana na janga la madeni.
Bw papademos atahitaji kuongoza serikali ya mpito inayoundwa, kuhakikisha nchi hiyo yenye deni kubwa inapata fedha za kuisaidia, na kuidhinisha fungu la dharura la dola bilioni 177 la kimataifa kutoka katika nchi wanachama wanaotumia sarafu ya Euro pamoja na Shirika la Fedha Duniani IMF.
"Rais, baada ya mapendekezo kutoka kwa viongozi wa kisiasa waliohudhuria mkutano, wamemtaka Lucas Papademos kuunda serikali mpya," taarifa ya ofisi ya rais imesema, baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa kisiasa na Bw Papademos.
Serikali mpya itaapishwa adhuhuri ya Ijumaa, amesema afisa mmoja wa ofisi ya rais.
Bw Papademos atachukua nafasi ya waziri mkuu anayeondoka George Papandreu ambaye alitangaza kuwa anajiuzulu baada ya kutaka kuitisha kura ya maoni kuhusu fungu la kusaidia deni kutoka eneo la euro.
Waziri mkuu mpya atapigiwa kura ya kuwa na imani naye bungeni, siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa kituo cha TV cha serikali.
Soko la hisa la Ugiriki lilipanda ghafla baada ya Bw Papademos kuwasili katika ikulu ya rais kuijunga na majadiliano siku ya Alhamisi asubuhi.

No comments:

Post a Comment