Pages

Friday, December 9, 2011

ASANTE KOTOKO YATUA TANZANIA KUIKABILI SIMBA.





VIONGOZI WA ASANTE KOTOKO WAKIWA NA MWENYEJI BI HELLEN MASANJA




TIMU ya soka ya Kumasi Asante Kotoko iliwasili jana kwa ajili ya mechi maalum dhidi ya Simba iliyopangwa kufanyika kesho kwenye uwanja wa Uhuru huku ikitoa tambo kibao dhidi ya wapinzani wao hao.
Kocha msadizi wa timu hiyo, Isaac Sarfo alisema kuwa wamekuja na kikosa cha wachezaji wanaofanya vyema katika ligi ya Ghana na kuwataka mashabiki kufika kwa wingi ili kuona mchezo huo.
Alisema kuwa kwa sasa wamekusajia jumla ya pointi 21 na wachezaji wake wamekuja kuendeleza wimbi la ushindi kwa timu yao na si vinginevyo.
“ Hakuna sababu ya kushindwa katika mchezo huo, tumejiandaa vilivyo na bila shaka tutaibuka na matokeo mazuri, ” alisema Sarfo.
Alisema kuwa wamefurahia sana kuwepo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Tanzania kwani waasisi wa mataifa yao Marehemu Kwame Nkurumah na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wameacha historia kubwa hapa duniani.
“Hatujasita kuja mara baada ya kuambia madhumuni ya mchezo huu, tutaomba chama chetu cha soka kuharisha mechi zetu ili kuja kujumuika na watanzania, nao walikubali ombi letu huku tukiwa tumebakiza mechi nne za ligi, hii ni mechi muhumu na ya kihistoria,” alisema.
Nahodha wa timu hiyo, Danielnii Adjei alisema kuwa Simba wasitarajie mteremko kutoka kwao kwani wamedhamilia kushinda kwa mabao mengi.
“Nashukuru kwa kupewa heshima hii, ni faraja kwetu kushiriki katika mechi kubwa ya kuadhimisha miaka 50n ya Uhuru, tumekuja kamili na tunashinda tu,” alisema Adjei.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Future Century, Hellen Masanja alisema kuwa maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na kabla ya mchezo huo, timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC itacheza na mechi ya utangulizi kwa kupambana na timu ya kombaini ya wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam, Mzizima Queen United.
Masanja alisema kuwa mchezo huo utaanza saa 8.30 na mashabiki wanaombwa kufika kwa wengi ili kuona vipaji vya wachezaji wa timu ya Kotoko na Simba.
Mwisho…
Wachezaji wa timu ya Asante Kotoko wakiwasili nchini jana tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya timu ya Simba kwenye uwanja wa Taifa. Mchezo huo umeandaliwa kwa ajili ya sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.

No comments:

Post a Comment