Pages

Tuesday, January 31, 2012

MADAKTARI WA JWTZ WAKATALIWA MUHIMBILI


.
LICHA ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutoa amri kwa madaktari wote wenye mikataba na Serikali kurejea kazini, bado wanataaluma hao jana waliendeleza mgomo baada ya kutia saini vitabu vya mahudhurio na kutoweka kusikojulikana huku wauguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakitoa msimamo mpya kwamba hawako tayari kufanya kazi na madaktari kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ).
Juzi, Waziri Mkuu Pinda alitoa onyo kwa madaktari hao akiwataka kurejea kazini kufikia jana kinyume chake ambaye angeshindwa angekuwa amejifukuzisha kazi na kwamba madaktari wa JWTZ wangechukua nafasi zao.
Agizo hilo la kwamba wangewatumia madaktari kutoka JWTZ jana liliamsha hasira za wauguzi Muhimbili ambao walitangaza msimamo wao wa kutofanya kazi nao.
Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Tawi la MHN, Paul Magesa alisema madaktari hao hawana uwezo wa kufanya kazi katika hospitali hiyo ya taifa ambayo ndiyo kubwa nchini kwa kuwa inahudumia wagonjwa walioshindikana katika hospitali wanazotoka.
“Sisi tulishafanya kazi nao mwaka 2005 na tunawafahamu wengi hawajui mambo mengi, watakuja kutuuliza na kutuongezea kazi za kufanya… tunaomba katika hili Serikali isikwepe tatizo, ilishughulikie kwa maslahi ya taifa,” alisema Magesa.
habari imeandikwa na gazeti mwananchi.

No comments:

Post a Comment