Na Mwandishi
Wetu
MWIMBAJI nguli nchini aliyeihama bendi
ya African Stars 'Twanga Pepeta' na kutua Mashujaa Musica, Charles
Gabriel 'Chaz Baba', ameanza vibaya kutambulishwa katika bendi yake
mpya, kutokana na 'kufikikwa' na wanamuziki wenzake ambao wengi
wanatoka Jamhuri ya Kidemokarsia ya Congo.
Onesho hilo lililoshirikisha bendi
tatu mahasimu za Mashujaa Musica, Mapacha Watatu na Extra Bongo, lengo
likiwa ni kuungana 'kuiua' Twanga Pepeta, lilifanyika jana usiku kwenye
ukumbi wa Business, Dar es Salaam, likijaza mashabiki kochokocho ambao
wengi walikwenda kumuona Chaz Baba kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na
bendi hiyo.
Hata hivyo, tofauti na matarajio ya
mashabiki wengi kwamba Chaz Baba angeingia na mambo mapya, alijikuta
akifunikwa na waimbaji wenzake wa Mashujaa waliotawala jukwaa.
Waimbaji wa Mashujaa wakiongozwa na
Jado Field Force, Mirinda Nyeusi, Pasia Budansi 'BlackBerry', Raja
Radha, Kajo Litungu, Sauti ya Radi, Kelvin Ulaka, Maga One Star,
Thelathini na Tatu '33' na wengine, ndio waliong'ara katikla hilo
lililokuwa maalumu kumtambulisha Chaz Baba.
Chaz Baba aliingia ukumbini kwa
mbwembwe, huku akisindikizwa na mashabiki wake waliokuwa wamebeba bango
la kumkaribisha katika bendi hiyo inayomilikiwa na Mkurugenzi wa
Mashujaa Group, Sakina Mbange 'Mamaa Sakina' akishirikiana na mumewe,
Hoseah Hopaje 'Maisha'.
Awali, kabla ya Mashujaa kupanda
jukwaani, bendi ya Extra Bongo chini ya Ally Chocky ilipanda jukwaani
na kupiga nyimbo za Mtenda Akitendewa, Fisadi wa Mapenzi na Falsafa.
Kivutio kikubwa kwa Extra Bongo
alikuwa Ramadhan Masanja 'Banza Stone', aliyelimudu jukwaa vyema na
kuwafanya mashabiki wa muziki wa dansi kupagawa kutokana na uimbaji
wake.
Bendi ya Mapacha Watatu, ilipanda
jukwaani ikiwa na Khalid Chuma 'Chokoraa', Jose Mara, Kalala Junior na
walimkaribisha Chaz Baba kuimba naye.
Hata hivyo, mpangilio wa upangaji
ratiba ulionekana 'kuwaboa' baadhi ya mashabiki, huku washereheshaji
wakiongozwa na Meneja wa Mapacha Watatu, Hamis Dacorta, wakichombeza
majigambo mengi na kuinyima Extra Bongo nafasi ya kutumbuiza kwa
ufasaha, hali iliyomkera Chocky na kuondoka ukumbini mapema.
Chaz Baba alijiengua Twanga Pepeta
wiki iliyopita akidai kwamba alikuwa ikifanya kazi ya 'deiwaka', bila
kuwa na mkataba, lakini kwa sasa amesaini mkataba wa miaka miwili Mashujaa
inayodaiwa kumpatia sh. milioni 10 na gari aina ya Noah.
MAPINDUZI YA ZANZIBAR: KUMBUKUMBU TUKUFU.
-
Miaka sitini na moja, leo tunakumbuka,
Mapinduzi matakatifu, yenye historia adhimu,
Unguja na Pemba, visiwa vya thamani,
Walinyanyuka wananchi, kwa s...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment