Pages

Monday, February 6, 2012

Mali yarudia mapigano

Serikali ya Mali inasema kuwa wanajeshi wake wamewauwa wapiganaji kama 20 wa kabila la Tuareg, ambao wanataka kujitenga.
Mji wa Timbuktu, kaskazini mwa Mali
Serikali inasema mapigano yalitokea Ijumaa, katika eneo la Timbuktu.
Inaarifiwa kuwa wanajeshi wa serikali walitumia helikopta kushambulia maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji kaskazini mwa nchi.
Wizara ya Ulinzi ilieleza kuwa mapigano hayo yaliendelea kwa siku mbili, karibu na mji wa Niafunke.
Wapiganaji wanataka kuwa na taifa huru kaskazini mwa Mali.
Vita baina ya wapiganaji hao na serikali vimekuwako muda mrefu, lakini vilisita, na sasa vimerudi tena tangu mwezi uliopita.
Wapiganaji hao wamepata nguvu kwa vile wenzao wamerudi nyumbani, baada ya kupigana upande wa jeshi la Gaddafi nchini Libya.
Wapiganaji hao wameshambulia maeneo kadha, na kusababisha watu wengi kukimbia kutoka makaazi yao.

No comments:

Post a Comment